Kiapo cha damu na aliyekuwa mpenzi wangu kinanitesa, sijui hata nifanyaje kujinasua na maagano

Kiapo cha damu na aliyekuwa mpenzi wangu kinanitesa, sijui hata nifanyaje kujinasua na maagano

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Habari zenu Wakuu!

Nina jambo ambalo linanitesa kwa muda sasa baada ya kupita kwenye mahusiano ya nyuma ambayo niliyaona kuwa ni kila kitu kwangu. Wakati ule tulikuwa vijana, damu inachemka, na tuliamini kuwa upendo wetu ulikuwa wa kipekee kuliko wa mtu mwingine yeyote hapa duniani.

Katika hali ya kupeana ahadi za kutokuachana, tulifikia hatua mbaya ya kufanya kiapo cha damu, tulifanya uamuzi ambao leo unaninyima usingizi; tulichanja chale kwenye kidole gumba cha kila mmoja wetu, tukalamba na kugusanisha damu ya kila mmoja, na kuapa kuwa "Yeyote atakayevunja ahadi hii na kuolewa au kuoa mtu mwingine, basi maisha yake asije akapata furaha na heri maishani." Wakati huo, tulicheka na kuona ni kielelezo cha juu kabisa cha uaminifu.

Baada ya muda, mambo yalibadilika na tukashindwa kuendelea. Kila mmoja alichukua hamsini zake, na nilidhani hayo yamebaki kuwa historia na utoto ule ulishapita. Lakini sasa, miaka kadhaa mbele, niko kwenye mchakato wa kuanza maisha mapya na mtu mwingine, ndipo vitu vya ajabu vimeanza kunitokea.

Kila hatua ninayopiga kuelekea kuhalalisha mahusiano yangu ya sasa, nakumbana na vikwazo visivyoelezeka, kuanzia ndoto za kutisha hadi hali ya hofu inayoniandama kila kukicha.

Najisikia mwenye hatia na wakati mwingine nahisi kama kile kiapo ndicho kinachonishika na kunizuia kusonga mbele.

Sijui hata nifanye nini kujinasua kwenye huu mtego niliouingia kwa hiari yangu mwenyewe.
 
Upuuzi mtupu.

Sasa kama hiko kiapo cha damu kina uwezo wa kukuharibia kwa sasa kilishindwa vipi kuwalinda kipindi hiko ili msiachane.

Embu punguza msongo wa mawazo,maisha haya hayahitaji userious sana maana PESA ni ngumu kuipata.
 
AI wa JF Ana hili la kusema

Habari PAYE,

Pole sana kwa yale unayopitia na kukutesa kwa muda mrefu. Ni kweli, mambo kama haya yanaweza kuleta hofu na wasiwasi mkubwa, hasa pale tunapohisi yameanza kuathiri maisha yetu ya sasa.

Kwanza kabisa, nataka kukuhakikishia kuwa wewe si wa kwanza wala wa mwisho kufanya maamuzi kama hayo ukiwa kijana. Damu inapochemka na hisia zikiwa juu, ni rahisi sana kuamini kuwa unafanya kitu sahihi kabisa kwa wakati huo, bila kujua athari zake za baadaye. Hivyo basi, usijilaumu sana kwa yaliyopita. Ulikuwa unajifunza na kukua.

Kuhusu kiapo chenyewe, ni muhimu kutambua kuwa kilifanyika katika wakati tofauti wa maisha yako na kwa mtazamo tofauti kabisa. Ingawa kinaweza kukuhisi kina nguvu kubwa kwa sasa, nguvu yake halisi mara nyingi inatokana na jinsi tunavyokiamini na kukipa nafasi akilini mwetu.

Hivi ndivyo unavyoweza kujinasua na kupata amani:

1. Msamaha wa Kujiamini: Jipe msamaha wewe mwenyewe kwa uamuzi ule wa zamani. Tambua kuwa ulifanya kulingana na uelewa wako wa wakati huo. Jifunze kutokana na hilo na songa mbele.
2. Maombi na Utakaso wa Kiroho: Kama una imani, ongea na Mungu wako au kiongozi wa dini unayemwamini. Waeleze hofu yako na uombe utakaso na kuvunjika kwa kila aina ya agano au laana unayohisi inakufunga. Mara nyingi, kuweka mambo haya mbele za Mungu au nguvu za kiroho unazoziamini kunaweza kukupa amani na uhuru mkubwa.
3. Ongea na Mtu Mwenye Hekima: Tafuta mzee wa busara au mtu mzima unayemwamini ambaye anaweza kukusikiliza na kukupa ushauri. Wakati mwingine, kueleza tu hofu zetu kwa mtu tunayemwamini kunaweza kupunguza mzigo mkubwa.
4. Zingatia Sasa na Baadaye: Badala ya kuruhusu hofu ya yaliyopita kukutawala, zingatia kujenga maisha yako ya sasa na yajayo kwa furaha na matumaini. Jenga mahusiano yako mapya kwa uaminifu na upendo. Kadri unavyoweka nguvu zako kwenye chanya, ndivyo nguvu ya kiapo hicho itakavyopungua akilini mwako.
5. Fanya Kitendo cha Kufunga na Kufungua: Kama unahisi unahitaji kitendo cha kimwili au cha kiishara, unaweza kuandika barua (ambayo hutaichapisha) ukiandika unavyovunja agano hilo la zamani na kisha uichome au uizike. Hiki kinaweza kuwa kitendo cha kisaikolojia kukusaidia kujihisi huru.

Kumbuka, wewe ni mkuu kuliko kiapo hicho cha zamani. Umebadilika, umekua, na una haki ya kuwa na furaha. Usiruhusu kivuli cha yaliyopita kuzuie nuru ya maisha yako ya sasa na yajayo. Utapata amani na utafanikiwa katika mahusiano yako mapya!

Tuko pamoja nawe. Pole sana tena.
 
Muone nabii nicolous suguye

Narudia tena, achana na ant christ wa humu jf, muone NABII NICOLOUS SUGUYE
anapatikana kivule matembele ya pili ndani ya kanisa la WRC/WRM

Haijalishi we ni wa dhehebu gani, dini gani, we nenda pale

UWE HAI, YESU YU HAI.
 
Baada ya Kaini kumuua Abeli, Mungu akamwambia Kaini umetenda nini maana damu ya ndugu yako inalia ikidai haki. Turudi kwenye mada: damu ni kiumbe na ukitamka chochote damu inakariri. Kwa hiyo damu mliyomwaga na kuunganisha ndiyo inayokuadhibu.
 
Upuuzi mtupu.

Sasa kama hiko kiapo cha damu kina uwezo wa kukuharibia kwa sasa kilishindwa vipi kuwalinda kipindi hiko ili msiachane.

Embu punguza msongo wa mawazo,maisha haya hayahitaji userious sana maana PESA ni ngumu kuipata.
Mkuu, hoja yako ni nzuri, lakini binadamu tunatofautiana, wengine tunaathiriwa na mambo ya psychology kutokana na makosa tuliyofanya nyuma. Inawezekana nguvu ya kiapo hicho haipo kwenye damu, bali ipo kwenye subconscious mind inayonihukumu
 
Habari zenu Wakuu!

Nina jambo ambalo linanitesa kwa muda sasa baada ya kupita kwenye mahusiano ya nyuma ambayo niliyaona kuwa ni kila kitu kwangu. Wakati ule tulikuwa vijana, damu inachemka, na tuliamini kuwa upendo wetu ulikuwa wa kipekee kuliko wa mtu mwingine yeyote hapa duniani.

Katika hali ya kupeana ahadi za kutokuachana, tulifikia hatua mbaya ya kufanya kiapo cha damu, tulifanya uamuzi ambao leo unaninyima usingizi; tulichanja chale kwenye kidole gumba cha kila mmoja wetu, tukalamba na kugusanisha damu ya kila mmoja, na kuapa kuwa "Yeyote atakayevunja ahadi hii na kuolewa au kuoa mtu mwingine, basi maisha yake asije akapata furaha na heri maishani." Wakati huo, tulicheka na kuona ni kielelezo cha juu kabisa cha uaminifu.

Baada ya muda, mambo yalibadilika na tukashindwa kuendelea. Kila mmoja alichukua hamsini zake, na nilidhani hayo yamebaki kuwa historia na utoto ule ulishapita. Lakini sasa, miaka kadhaa mbele, niko kwenye mchakato wa kuanza maisha mapya na mtu mwingine, ndipo vitu vya ajabu vimeanza kunitokea.

Kila hatua ninayopiga kuelekea kuhalalisha mahusiano yangu ya sasa, nakumbana na vikwazo visivyoelezeka, kuanzia ndoto za kutisha hadi hali ya hofu inayoniandama kila kukicha.

Najisikia mwenye hatia na wakati mwingine nahisi kama kile kiapo ndicho kinachonishika na kunizuia kusonga mbele.

Sijui hata nifanye nini kujinasua kwenye huu mtego niliouingia kwa hiari yangu mwenyewe.
Nani ndo alivunja hicho kiapo kati yako na yy nani ndo chanzo cha mahusiano yenu kufa tujue hilo kwanza then ndo tujue pa kuanzia
 
Ila binti huko alipo yuko fresh, hujioni kuwa ni ww n mwendawazimu?
Huko alipo kusema yuko fresh ni hisia tu, maana hatujaongea miaka mingi. Na hata kama yeye yuko sawa, haiondoi ukweli kwamba mimi nafsi yangu inanisuta.
 
Muone nabii nicolous suguye

Narudia tena, achana na ant christ wa humu jf, muone NABII NICOLOUS SUGUYE
anapatikana kivule matembele ya pili ndani ya kanisa la WRC/WRM

Haijalishi we ni wa dhehebu gani, dini gani, we nenda pale

UWE HAI, YESU YU HAI.
Naona unapambana kuongeza mapato hapo kanisani kwenu 😂
 
Nani ndo alivunja hicho kiapo kati yako na yy nani ndo chanzo cha mahusiano yenu kufa tujue hilo kwanza then ndo tujue pa kuanzia
Kiukweli, mahusiano yetu yalikufa kifo cha asili kutokana na umbali na mabadiliko ya maisha, ingawa yeye ndiye alianza kuonyesha dalili za kupoa na sijui huko aliko kama kupata mtu mwingine
 
Muone nabii nicolous suguye

Narudia tena, achana na ant christ wa humu jf, muone NABII NICOLOUS SUGUYE
anapatikana kivule matembele ya pili ndani ya kanisa la WRC/WRM

Haijalishi we ni wa dhehebu gani, dini gani, we nenda pale

UWE HAI, YESU YU HAI.
😅😅 imenilazimu nicheke kwa sauti
 
Naona unapambana kuongeza mapato hapo kanisani kwenu
Sijawahi kukanyaga huko.

Isipokuwa, humu ndani huwa natoa ushauri mbalimbali kuhusiana na mambo kama hayo..
Lakini roho yangu ina amani na inashuhudia kuwa nimempa ushauri ulio bora kuliko ushauri wowote ule niliowahi kutoa popote.

UWE HAI, YESU YU HAI.
 
Back
Top Bottom