Kiukweli, mahusiano yetu yalikufa kifo cha asili kutokana na umbali na mabadiliko ya maisha, ingawa yeye ndiye alianza kuonyesha dalili za kupoa na sijui huko aliko kama kupata mtu l
Bado hujajibu swali langu mkuu kati yako na yy nani ndo alimgwaya mwenzake lazima awepo mmoja wao aliyeanza kumgwaya mwenzakeKiukweli, mahusiano yetu yalikufa kifo cha asili kutokana na umbali na mabadiliko ya maisha, ingawa yeye ndiye alianza kuonyesha dalili za kupoa na sijui huko aliko kama kupata mtu mwingine
AsanteBaada ya Kaini kumuua Abeli, Mungu akamwambia Kaini umetenda nini maana damu ya ndugu yako inalia ikidai haki. Turudi kwenye mada: damu ni kiumbe na ukitamka chochote damu inakariri. Kwa hiyo damu mliyomwaga na kuunganisha ndiyo inayokuadhibu.
Moderators mbona sioni MEME ya kidole cha kati?Habari zenu Wakuu!
Nina jambo ambalo linanitesa kwa muda sasa baada ya kupita kwenye mahusiano ya nyuma ambayo niliyaona kuwa ni kila kitu kwangu. Wakati ule tulikuwa vijana, damu inachemka, na tuliamini kuwa upendo wetu ulikuwa wa kipekee kuliko wa mtu mwingine yeyote hapa duniani.
Katika hali ya kupeana ahadi za kutokuachana, tulifikia hatua mbaya ya kufanya kiapo cha damu, tulifanya uamuzi ambao leo unaninyima usingizi; tulichanja chale kwenye kidole gumba cha kila mmoja wetu, tukalamba na kugusanisha damu ya kila mmoja, na kuapa kuwa "Yeyote atakayevunja ahadi hii na kuolewa au kuoa mtu mwingine, basi maisha yake asije akapata furaha na heri maishani." Wakati huo, tulicheka na kuona ni kielelezo cha juu kabisa cha uaminifu.
Baada ya muda, mambo yalibadilika na tukashindwa kuendelea. Kila mmoja alichukua hamsini zake, na nilidhani hayo yamebaki kuwa historia na utoto ule ulishapita. Lakini sasa, miaka kadhaa mbele, niko kwenye mchakato wa kuanza maisha mapya na mtu mwingine, ndipo vitu vya ajabu vimeanza kunitokea.
Kila hatua ninayopiga kuelekea kuhalalisha mahusiano yangu ya sasa, nakumbana na vikwazo visivyoelezeka, kuanzia ndoto za kutisha hadi hali ya hofu inayoniandama kila kukicha.
Najisikia mwenye hatia na wakati mwingine nahisi kama kile kiapo ndicho kinachonishika na kunizuia kusonga mbele.
Sijui hata nifanye nini kujinasua kwenye huu mtego niliouingia kwa hiari yangu mwenyewe.
Hisia zako tu kiongozi, huenda bado unampenda huyo binti.Aise! Bora ulikwepa hii, kwani naona mateso yake leo
Swala lako si la nyama wala mwili, hapo umefanya maagano makubwa sana ya kiroho.imenilazimu nicheke kwa sauti
Sasa nyote mlivunja ahadi,vipi yule mwenzio naye yanamkumba mambo hayo?Kama hayamkumbi basi hiyo ahadi haina nguvuHabari zenu Wakuu!
Nina jambo ambalo linanitesa kwa muda sasa baada ya kupita kwenye mahusiano ya nyuma ambayo niliyaona kuwa ni kila kitu kwangu. Wakati ule tulikuwa vijana, damu inachemka, na tuliamini kuwa upendo wetu ulikuwa wa kipekee kuliko wa mtu mwingine yeyote hapa duniani.
Katika hali ya kupeana ahadi za kutokuachana, tulifikia hatua mbaya ya kufanya kiapo cha damu, tulifanya uamuzi ambao leo unaninyima usingizi; tulichanja chale kwenye kidole gumba cha kila mmoja wetu, tukalamba na kugusanisha damu ya kila mmoja, na kuapa kuwa "Yeyote atakayevunja ahadi hii na kuolewa au kuoa mtu mwingine, basi maisha yake asije akapata furaha na heri maishani." Wakati huo, tulicheka na kuona ni kielelezo cha juu kabisa cha uaminifu.
Baada ya muda, mambo yalibadilika na tukashindwa kuendelea. Kila mmoja alichukua hamsini zake, na nilidhani hayo yamebaki kuwa historia na utoto ule ulishapita. Lakini sasa, miaka kadhaa mbele, niko kwenye mchakato wa kuanza maisha mapya na mtu mwingine, ndipo vitu vya ajabu vimeanza kunitokea.
Kila hatua ninayopiga kuelekea kuhalalisha mahusiano yangu ya sasa, nakumbana na vikwazo visivyoelezeka, kuanzia ndoto za kutisha hadi hali ya hofu inayoniandama kila kukicha.
Najisikia mwenye hatia na wakati mwingine nahisi kama kile kiapo ndicho kinachonishika na kunizuia kusonga mbele.
Sijui hata nifanye nini kujinasua kwenye huu mtego niliouingia kwa hiari yangu mwenyewe.
Nitajaribu kubadili mindset yangu nione kama hii hali itatulia, maana nimechoka kuishi kwa hofu.Kinachokutesa wala sio kiapo. Ni hiyo Imani yako juu ya hicho kiapo. Badilisha unavyoamini hasa mtazamo wako. Maana kama kingekuwa na nguvu, kingewashikilia msingeachana.
Ukikua utaelewa.Upuuzi mtupu.
Sasa kama hiko kiapo cha damu kina uwezo wa kukuharibia kwa sasa kilishindwa vipi kuwalinda kipindi hiko ili msiachane.
Embu punguza msongo wa mawazo,maisha haya hayahitaji userious sana maana PESA ni ngumu kuipata.