Kiarabu ndio lugha ya asili ya sayansi, tiba, biashara na elimu kwa ujumla

Hospitali ya wapi? Kupitia hiko kitabu kilifanya uchunguzi
 
Hospitali ya wapi? Kupitia hiko kitabu kilifanya uchunguzi

Kipande cha nyama ya nguruwe kwa siku 'chaweza kusababisha saratani '​


Source Chuo kikuu cha Oxford kupitia BBC news
 
Very myopic Uislamu kwako unaoujua ni wa Tanzania tuu.
Narudia, uislam na elimu wapi na wapi? Hata waislamu wenye itikadi kali lakini wanapenda elimu, huwezi kuwakuta wakienda kusoma nchi za Kiarabu, wote safari ni kwa makafiri. Hilo nalo unataka tubishane? Mwenye amekwenda kusoma uarabuni, akirudi hapa huwezi kumkuta ana practice professional yake, atakwenda kwenye siasa, ushehe au uganga wa kutabiri nyota tu. Nasisitiza, "Uislam na elimu wapi na wapi"?
 
Wanavyofanya hivi ni kama kuutangaza uislamu lakini uislamu na elimu mbalimbali.
Waarabu walipokuja Tanganyika walikuwa wanajenga msikiti, kisima cha kujitawazia na madrasa (kusoma kiarabu na elimu ya dini ya kiislamu).
 
Papa Sylvester ndio mkristo wa mwanzo wa ngazi za juu kupenda elimu.Alisoma madrasa na kufuzu hesabati ndio akazifundisha kanisani kwake..Hapo ni mwaka 1095 wakati waislamu washajenga vituo vya kuratibu mienendo ya nyota na sayari.
 
Mwanafalsafa Aristotle wa Ugiriki ya kale aliandika mambo mengi ya sayansi miaka kama 1,100 kabla ya kuzaliwa Muhammad, kabla ya hao bani Ummayad.

Aristotle hakujua Kiarabu.

Acheni ujinga nyie.

 
Meanafakdafa Aristotle wa Ugiriki ya kale aliandika mambo mengi ya sayansi miaka kama 1,100 kabla ya kuzaliwa Muhammad, kabla ya hao bani Ummayad.

Aristotle hakujua Kiarabu.

Acheni ujinga nyie.

View attachment 3223881
Ukimtaja Aristotole lazima uongeze kwa hisani ya waislamu.Kwani taarifa zake na kazi zake kwanzo zilikushanywa kule Baghdad na kutafsiriwa kwa lugha ya kiarabu.Hatimae zikafika Toledo na Cordova kule Uhispania ndipo hao lugha ndogo ndogo za Ulaya na makabila yakanukuu kazi zake mpaka zikawafikia hao Britanica.lugha ya kiiengereza ilikuwa ni miongoni mwa lugha ndogo ndogo ambayo baadae ikakuwa wakati huo kiarabu kimshawazomesha wazungu. kwa karne kadhaa.
Kigiriki ilikuwa ni moja ya lugha zilizotumiwa na wataalamu wa Baghadad kufahamu aliyofanya Aristotle na wenzake.
Waislamu wana maelekezo mengi ndani ya dini yao ya kutodharau elimu na lugha za watu wengine.
 
Waislamu gani mkuu nimekwambia Aristotle kaandika habari zake miaka 1,100 kabla Quran haijaandikwa.

Waislamu gani?
 
Waislamu gani mkuu nimekwambia Aristotle kaandika habari zake miaka 1,100 kabla Quran haijaandikwa.

Waislamu gani?
Waislamu wa Baghdad ndio waliozileta kazi za Aristotle hizo za miaka unayosema na hizo tarehe zale wakazidhibiti.
Sasa sijui ni kipi unachokipinga.
Waislamu waliziweka sawa kazi za watu wengine wa jamii ya kihindi halafu kuzichanganya na kutoa maarifa makubwa yaliyofika Ulaya kupitia Spain.
Kwa mafunzo ya uislamu tunaamini uislamu ndio dini ya mwanzo ya binadamu kabla hata Quran haijaanza kuandikwa kwa lugha ya kiarabu ambayo ndiyo Mungu kwa hekima zake aliyoichagua iandikwe kwayo.
Hivyo dini ya Aristotle na wenzake hatuwezi kukanusha kuwa haikuwa Uislamu.Ba kama walikuwa dini tofauti na Uislamu basi bado walikuwa ndani ya muongozo wa Mwenyezi Mungu.
 
Waislamu gani mkuu nimekwambia Aristotle kaandika habari zake miaka 1,100 kabla Quran haijaandikwa.

Waislamu gani?

Mkuu kiranga usipate tabu mimi nimesoma andiko la jamaa nikaishia Kusikitika.

Naomba unisaidie Kusikitika.
 
Waislamu wa Baghdad kina nani hao wasio na majina? Taja majina yao tuchunguze habari zao, tujue kama ni Waislamu kweli ama ni uzushi tu. Tujue ni wa mwaka gani.

Mbona unaongelea kivivuvivu na kijuujuu jambo la usomi?

Huoni hapo mimi nimekuwekea jina la mtu, nimekuwekea sehemu, nimekuwekea mwaka.

Sasa hao Waislamu wa Baghdad wa mwaka gani? Kina nani?

Baghdad imeanzishwa July 30, 762 CE.

Aristotle kaandika habari zake 500 BCE. Miaka 1262 kabla Baghdad haijaanzishwa.

Sasa Aristotle aliyeandika sayansi miaka 1262 kabla Baghdad haijaanzishwa itakuwaje awe kafundishwa sayansi na Waislamu wa Baghdad?

Wewe hata historia unaijua?
 
Mkuu kiranga usipate tabu mimi nimesoma andiko la jamaa nikaishia Kusikitika.

Naomba unisaidie Kusikitika.
Mtu anakwambia Waislamu wa Baghdad walimfundisha Aristotle sayansi.

Hata hajui kuwa Aristotle aliandika sayansi miaka 1262 kabla Baghdad haijaanzishwa.

Ukimsoma unaona huyu hata historia ndogo tu ya Baghdad haijui.
 
Kichwa chako ni kigumu kuelewa au umeamua kupinga ukweli uliokuwa hukuujua hapo zamani.
Hatupingi habari za Aristotle isipokuwa tuanchosema Aristotle habari zake zisingejulikana kama si kazi ya Alkindi kwenye jumba la hikma la Baghad ambaye ni miongoni mwa waliozitafsiri kazi hizo.
Kwa ujumla wake walichofanya akina Aristotle na Socrates vilikuwa na kasoro kadhaa ambazo baada ya tafiti waislamu walikwenda mbali sana.
 
Mtu anakwambia Waislamu wa Baghdad walimfundisha Aristotle sayansi.

Hata hajui kuwa Aristotle aliandika sayansi miaka 1262 kabla Baghdad haijaanzishwa.

Ukimsoma unaona huyu hata historia ndogo tu ya Baghdad haijui.
Sayansi ni maneno yatokanayo na hao waislamu wa Baghdad na wenzao na hatusemi kuwa walimfundisha Aristotle bali walithamini kazi zake na kuzifanyia kazi wakaacha alichokosea na kuchukua walichoona kapatia.
Huo ndio ubora wa uislamu katika elimu.
Kwanini ungangangania kuonesha kuwa Aristotle ni bora kielimu kuliko waislamu waliomtambulisha kwa ulimwengu.Kilichofanywa ni kuthamini elimu na kutunza historia kama tunavyofanya hapo kuhusiana na mchango wa uislamu na lugha ya kiaarabu katika maendeleo ya dunia
 
Mji wa Baghdad umeanzishwa mwaka gani na Aristotle kaishi mwaka gani mpaka mwaka gani?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Kwa hiyo unakubali kuwa sayansi ilikuwepo kabla ya hao Waislamu wa Baghdad na wao ndio walijifunza kwa Aristotle?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…