Kiarabu ndio lugha ya asili ya sayansi, tiba, biashara na elimu kwa ujumla

Kichwa chako ni kigumu kuelewa au umeamua kupinga ukweli uliokuwa hukuujua hapo zamani.
Hatupingi habari za Aristotle isipokuwa tuanchosema Aristotle habari zake zisingejulikana kama si kazi ya Alkindi kwenye jumba la hikma la Baghad ambaye ni miongoni mwa waliozitafsiri kazi hizo.
Kwa ujumla wake walichofanya akina Aristotle na Socrates vilikuwa na kasoro kadhaa ambazo baada ya tafiti waislamu walikwenda mbali sana.

Nakupa mfano wa kukuonesha Waislamu hata baada ya kumjua Aristotle wameharibu sayansi.

Waislamu wameiandika habari ya mvua inavyopatikana kwa kuikosea, kwa juu juu, bila detail za process ya evaporation

Baada ya kuisoma kwa Aristotle aliyeiandika vizuri zaidi, aliyeongelea process ya evaporation, miaka 1,100 kabla ya kuandikwa kwa Quran.
 
nani kakwambia kuwa mvua hupatikana kwa evaporation.
 
Huu ni ukweli ambao wengi hawaujui kwani umejificha ya kuwa lugha ya kiarabu ndio lugha iliyotumika kuufikishia ulimwengu elimu karibu zote.

Lugha ya kiarabu ambayo ndiyo lugha iliyoteremshiwa Qur'an imetoa fursa za wazi kwa walimwengu dunia nzima na kuwapa ujanja wa kuishi na kuifaidi dunia.

Kwa ufupi kabisa ufunguzi wa ulimwengu kielimu ulianzia Baghdad wakati wa utawala wa bani Umayya na baadae utawala wa Abbasiya chini ya utawala wa Haroun Alrashid.

Tawala hizo ndizo zilijenga maktaba kubwa sana iliyoitwa baitul Hikma ambayo ilidumu kwa karne nyingi kabla kubomolewa katika vita kutoka watawala wa kikristo waliopitia bara hindi.

Chanzo cha maktaba hiyo ilikuwa ni wakuu wa koo za kiarabu waliopenda kuhifadhi Qur'an na hadithi za mtume Muhammad saw pamoja na mashairi mazuri ya koo zao.

Mara maktaba hiyo ikaanza kuweka vitabu vyengine vilivyopatikana katika tawala ambako majeshi ya waislamu yalikuwa yakienda wakati wa vita na kutoka misafara ya kawaida ya kibiashara.

Maandishi hayo hayakuwa katika mfumo wa vitabu vya kisasa yalipatikana kutoka tawala za kirumi,kigiriki na kihindi.Maandishi hayo yailetwa hapo na kutafsiriwa kuingizwa lugha ya kiarabu.

Maktaba hiyo kila miaka ilivyoongezeka ikapanuliwa na kuongezwa vitengo vya matawi mbali mbali ya kielimu ukiongezea na kitengo cha uchapishaji.

Hatimae teknolojia ya uchapishaji na uandishi kwa njia nyepesi uliochukuliwa kutoka mbali kama vile China ukaingizwa kwenye maktaba hiyo na kuongeza kasi za uandishi na tafsiri.

Vitengo vilivyonawiri zaidi katika kituo hicho ni vile vya elimu ya tiba,elimu ya anga na hesabati chini ya mwanahesabati Alkhwarizm ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha aljebra alichokiandika katika kutafsrii mahesabu yaliyomo ndani ya Qur'an juu ya mirathi.

Umaarufu wa maktaba hiyo ambao uligeuka kuwa kama chuo cha elimu uliwavuta watu wengi sana kutoka maeneo ya jirani ikiwemo Iran na majimbo ya Urusi kuja kujisomea au kwa kazi maalumu. Kulikuwa na wafanyakazi wa kila fani na kutoka maeneo mbali mbali.Walikuwepo waliokuwa na asili za kiyahudi na makabila mengineyo ya jirani.

Kituo hicho kilipobomolewa na kuchomwa moto,mto wa dijla ambao unajulikana sasa kama euphrates uligeuka rangi kuwa mweusi kutokana na wino wa vitabu hivyo.

Wakatokea baadhi ya wasomi na waliokuwa wafanyakazi wa kituo hicho wakachagua baadhi ya nakala walizoweza kuziokoa na kwenda nazo maeneo yao.Miongoni mwa hao ni Nasrudin Al tulsi wa Azerbajan ambaye alikwishajenga kituo chake cha anga huko kwao.Yeye alifanikiwa kuokoa vitabu zaidi ya 40,000 ambavyo alikuwa akivibeba kidogo kidogo kwa kutumia farasi na ngamia.

Pamoja na kupigwa vita,waislamu nao kwa fitna walikuwa na ugomvi baina yao wenyewe.Wako walionusurika vifo na kuamua kukimbilia maeneo ya mbali ambako tayari athari za tawala za kiislamu zilikwishatangulia.
Maeneo hayo ni kama vile kaskazini ya Afrika,Libya,Tunisia,Aljeria na Morocco mbali na maeneo ya ndani ya kama vile MalimChad na Niger.

Kwa upande wa Ulaya ya sasa waislamu walikwishatangulia Spain zamani. Mmoja ya waliofanikiwa kuhama na kuendeleza mfano wa tawala za Baghdad ni Abulrahmaan ambaye alikwenda kufanya makazi yake Cordoba chini ya himaya ya Ummawiyah. Miji mingi sana ndani ya Spain iliyojulikana wakati huo kama Andalus ilijengwa kwa nidhamu za tawala za kiislamu ambapo lazima kuwe na maktaba.Miji michache kati ya hiyo ni Granada,Sevile na Toledo.

Kwa mfano papa Sylvester (Gerbet) ni miongoni mwa wakristo wa mwanzo kusoma kwenye chuo kikuu cha kiislamu cha Granada na aliwahi kuhudhuria mafunzo chuo kikuu kikongwe zaidi duniani cha Alqarawiney ambacho kiko Fez nchini Morroco ambacho bado kinaendeshwa kwa mfumo ule ule maarufu kama madrasa.

Papa Syvester ambaye alivutiwa sana na utamaduni wa waislamu na elimu zao alipenda sana somo la hisabati na ndiye wa mwanzo kuingiza elimu hiyo nchini Italy wakati wa utawala wake ambapo mwenyewe alikuwa ni mwalimu pia pamoja na kazi za upapa (1095).

Maktaba ya Toledo ndiyo maarufu zaidi kwani hapo ndipo makabila mengi ya Ulaya kuanzia Ureno, Ufaransa,Italy na kote kwengineko walisoma na kutafsiri kazi hizo kutoka lugha ya kiarabu na kuingiza kwenye lugha zao za asili. Katika maktaba hiyo pia walikuwepo wafasiri walioweza kuingiza elimu hizo kwenye lugha ya kiyahudi ya kiebrania.

Ikumbukwe wakati ulimwengu wa kiisalamu ukiwa unairithisha dunia elimu kwa lugha zao kutoka kiarabu lugha maarufu za sasa kama vile kiiengereza na kifaransa hazikuwepo au ndio muda zilikuwa zinazaliwa na kuanza kujulikana.

Vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya kiarabu na kutumika kwenye vyuo vikuu vingi vya ulaya walivyojenga wenyewe ni vingi sana.Ngoja tutaje baadhi tu ya vitabu hivyo.

1. AL HAW. Ni kitabu cha tiba kiliandikwa na Abubakr Al Razi (864 -935)AD.Kinajumuisha vitabu vidogo (volumes) 23.Kilitafsiriwa kuingizwa lugha ya kilatin na myahudi aitwaye Faraj ben Salim kutoka visiwa vya Sicily mnamo mwakka 1276.

2. AL QANON FIY TTIB cha tiba kwa kiiengereza kinajulikana kama The canon of medicines. Kiliandikwa na Ibn Sina (980 -1037)AD.Kitabu hicho kimetumika kama rejea kubwa kwenye vyuo vikuu vya Ulaya mpaka mwaka 1650.Kilikuwa kikitoa ufafanuzi wa tiba na madawa kwa kutumia michoro kufahamisha vizuri.

3. KITAB AL TASIF cha Abul Qassim (936-1013)AD.Ni mkusanyiko wa vitabu vidogo 30.Abulcasis ndiye mvumbuzi wa vifaa zaidi ya 200 vinavyotumika mpaka leo kwenye vyumba vya upasuaji na vitabu vyake vimetumika kufundishia Ulaya kwa zaidi ya miaka 500.Aliishi na kufia mjini Cordoba ndani ya Spain.Nyumba yake mpaka leo ipo na imepewa thamani ya juu katika utalii wa majengo.

4.AL KITAB AL MUKHTASAR FIY HISAB ALJABR WAL MUQABALA.Kiliandikwa na Muhammad bin Mussa Alkharizm (780-850).Alikuwa ni mmoja ya wafanyakazi mashuhuri wa kitengo cha kutafsiri maandishi kwenye jengo la Baitul Hikma na baadae akawa ndiye mkurugenzi wa kituo hicho.

Pamoja na kazi nyingi alizozifanya alisoma na kutafsiri maandishi ya Euclid, mwanafalsa wa zamani wa kigiriki.Hata hivyo maandishi na hesabu zake za Aljebra ambazo ndizo zilizozalisha ujanja wote wa hesabu duniani haujaonekana kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na michoro ya maumbile ya Euclid.

Nakala halisi ya kitabu cha Alkhwarizm katika hati zake za kiarabu kinapatikana kwenye maktaba ya chuo kikuu cha Oxford nchini Uiengereza.
Kichwa Yako imejaa mapumba tupu kiarabu ndio lugha ya kisayansi Tweneke bebe.. "€¥<¢£€^°
 
Ushapingana na Quran yako mwenyewe kwa ubishi tu, unaelewa hilo?

Hiyo link inatuonesha Aristotle kawafundisha Waislamu.
Kichwa chako hakioni mbele.
 
View: https://web.facebook.com/zakirnaik/videos/the-quran-describes-the-water-cycle-in-great-detail-1400-years-ago-dr-zakir-naik/301972664384941/?_rdc=1&_rdr# msikilize Zakir Naik kuhusu kufanyika kwa mvua kama ilivyo ndani ya Quran.Ni zaidi ya Evaporation uijuawayo wewe pekee.

Aristotle aliandika haya mambo miaka 1,100 kabla ya Quran kuandikwa.

Hivyo kama wamekopi tu kwa Aristotle, si ajabu.

Haya mambo yalijulikana na kuandikwa na Wagiriki wa kale kina Aristotle na Anaxagoras miaka 1,100 kabla ya Quran kuyaandika.

Kwa hiyo Quran haikuwa imeandika kitu kipya hapo, by that time hiyo habari ilishakuwa old knowledge.
 
Aristotle al8andika haya mambo miaka 1,100 kabla ya Quran kuandikwa.

Hivyo kama wamekopi tu kwa Aristotle, si ajabu.

Haya mambo yalijulikana na kuandikwa na Wagiriki wa kale kina Aristotle na Anaxagoras miaka 1,100 kabla ya Quran kuyaandika.

Kwa hiyo Quran haikuwa imeandika kitu kipya hapo, by that time hiyo habari ilishakuwa old knowledge.
kama alikopiwa Aristotle mbona maelezo ni tofauti sana na alivyosema yeye na hata sayansi ya kisasa imethibitisha kuwa alichosema Aristotle ni tofauti na ni makosa kushusiana na mvua.Alipatia sehemu moja na akashindwa kuona mengine.
Hata waislamu wenyewe wa mwanzo hawakuelewa maana halisi ya ufafanuzi huo ulio sahihi zaidi.
 
Sasa unakataa kwamba Waislamu wamejifunza kwa Aristotle?
Na wewe jee unakataa kuwa waislamu ni watu wa elimu na huwa wanachukua elimu popote na kwamba habari za Aristotle zisingekufikia kama si waislamu
 
kama alikopiwa Aristotle mbona maelezo ni tofauti sana na alivyosema yeye na hata sayansi ya kisasa imethibitisha kuwa alichosema Aristotle ni tofauti na ni makosa kushusiana na mvua.Alipatia sehemu moja na akashindwa kuona mengine.
Hata waislamu wenyewe wa mwanzo hawakuelewa maana halisi ya ufafanuzi huo ulio sahihi zaidi.
Quran ina makosa mengi sana, hivyo haiwezi kuwa kitabu cha Mungu.

Ni kitabu cha watu tu waliokuwa wanabumbabumba enzi za giza.

Nikikuwekea makosa ya kwenye Quran huwezi kumaliza kuyatatua hapa.

Bisha.
 
Na wewe jee unakataa kuwa waislamu ni watu wa elimu na huwa wanachukua elimu popote na kwamba habari za Aristotle zisingekufikia kama si waislamu
Waislamu si watu wa elimu.

Waislamu ni watu wa imani.

Wangekuwa watu wa elimu wasingeikubali Quran yenye makosa chungu nzima.
 
Ni matumaini yangu kuwa umeelewa maudhui ya huu uzi mpaka umeshindwa kukanusha kuwa waislamu kupitia lugha ya kiarabu ndio waliosambaza elimu kwa dunia nzima.Baada ya kazi hiyo mpaka na wewe umeelimika japo hupendi kushukuru.
Habari za Qur'an ni mada nzito zaidi kwako na wote waliojaribu wamekwama.Wewe binafsi umekwama kutetea falsafa ya Aristotle iliyosahihiswa na waislamu na ambayo Quran imechambua kuliko wote hao. na kama inavyojulikana sasa kupitia sayansi.
 
Watu walikuwa na elimu tangu enzi za Mafirauni Egypt huko, wakajenga ma pyramid. Wakasambaza elimu kabla Uislamu haujajulikana ni nini.

Umeanza kusema Waislamu wa Baghdad wamemfundisha Aristotle, tukaja kuona Baghdad imeanzishwa miaka 1262 baada ya Aristotle kuandika sayansi yake, na actually Aristotle ndiye aliyewafundisha Waarabu wa Baghdad sayansi.

Nakwambia hivi, Quran imejaa ujinga na uongo.

Hivyo Uislamu hauwezi kuwa dini ya sayansi.

Nimekwambia bisha nikuwekee ushahidi hapa.

Kwanini hujibu kwa neno moja tu useme "nabisha" nikuwekee ujinga wa Quran ambao nina hakika huwezi kuuapangua hapa?

Andika "nabisha" tu, sitaki maneno mengi.
 
Kuhusu QUran usinilazimishe kusema unavyotaka ili utukane tu kama walivyofanya wenzako humu humu JF na wakashindwa kwa hoja.
Nimegundua hata maana ya sayansi huijui.Soma hapo chini.
Science is the systematic study of the structure and behaviour of the physical and natural world through observation, experimentation, and the testing of theories against the evidence obtained.
"the world of science and technology"
Kwa maana hiyo kabla ya kuteremka Quran na yaliyotendwa na waislamu pale Baghdad hakukuwa na sayansi.Kilichokuwepo ni falsafa ambazo zilikushanywa na waislamu na ikawa kama ni gia ya kuanzisha sayansi,
Kazi ya majaribio na uwekaji data kwa mara ya mwanzo ulifanywa na akina Avicenna na Ibnu Hayyan.Wanahistoria wote wa sayansi wanalijua hilo isipokuwa wewe kwa vile hujui hata maana ya sayansi
 
Huu ni ukweli ambao wengi hawaujui kwani umejificha ya kuwa lugha ya kiarabu ndio lugha iliyotumika kuufikishia ulimwengu elimu karibu zote.

Lugha ya kiarabu ambayo ndiyo lugha iliyoteremshiwa Qur'an imetoa fursa za wazi kwa walimwengu dunia nzima na kuwapa ujanja wa kuishi na kuifaidi dunia.

Kwa ufupi kabisa ufunguzi wa ulimwengu kielimu ulianzia Baghdad wakati wa utawala wa bani Umayya na baadae utawala wa Abbasiya chini ya utawala wa Haroun Alrashid.

Tawala hizo ndizo zilijenga maktaba kubwa sana iliyoitwa baitul Hikma ambayo ilidumu kwa karne nyingi kabla kubomolewa katika vita kutoka watawala wa kikristo waliopitia bara hindi.

Chanzo cha maktaba hiyo ilikuwa ni wakuu wa koo za kiarabu waliopenda kuhifadhi Qur'an na hadithi za mtume Muhammad saw pamoja na mashairi mazuri ya koo zao.

Mara maktaba hiyo ikaanza kuweka vitabu vyengine vilivyopatikana katika tawala ambako majeshi ya waislamu yalikuwa yakienda wakati wa vita na kutoka misafara ya kawaida ya kibiashara.

Maandishi hayo hayakuwa katika mfumo wa vitabu vya kisasa yalipatikana kutoka tawala za kirumi,kigiriki na kihindi.Maandishi hayo yailetwa hapo na kutafsiriwa kuingizwa lugha ya kiarabu.

Maktaba hiyo kila miaka ilivyoongezeka ikapanuliwa na kuongezwa vitengo vya matawi mbali mbali ya kielimu ukiongezea na kitengo cha uchapishaji.

Hatimae teknolojia ya uchapishaji na uandishi kwa njia nyepesi uliochukuliwa kutoka mbali kama vile China ukaingizwa kwenye maktaba hiyo na kuongeza kasi za uandishi na tafsiri.

Vitengo vilivyonawiri zaidi katika kituo hicho ni vile vya elimu ya tiba,elimu ya anga na hesabati chini ya mwanahesabati Alkhwarizm ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha aljebra alichokiandika katika kutafsrii mahesabu yaliyomo ndani ya Qur'an juu ya mirathi.

Umaarufu wa maktaba hiyo ambao uligeuka kuwa kama chuo cha elimu uliwavuta watu wengi sana kutoka maeneo ya jirani ikiwemo Iran na majimbo ya Urusi kuja kujisomea au kwa kazi maalumu. Kulikuwa na wafanyakazi wa kila fani na kutoka maeneo mbali mbali.Walikuwepo waliokuwa na asili za kiyahudi na makabila mengineyo ya jirani.

Kituo hicho kilipobomolewa na kuchomwa moto,mto wa dijla ambao unajulikana sasa kama euphrates uligeuka rangi kuwa mweusi kutokana na wino wa vitabu hivyo.

Wakatokea baadhi ya wasomi na waliokuwa wafanyakazi wa kituo hicho wakachagua baadhi ya nakala walizoweza kuziokoa na kwenda nazo maeneo yao.Miongoni mwa hao ni Nasrudin Al tulsi wa Azerbajan ambaye alikwishajenga kituo chake cha anga huko kwao.Yeye alifanikiwa kuokoa vitabu zaidi ya 40,000 ambavyo alikuwa akivibeba kidogo kidogo kwa kutumia farasi na ngamia.

Pamoja na kupigwa vita,waislamu nao kwa fitna walikuwa na ugomvi baina yao wenyewe.Wako walionusurika vifo na kuamua kukimbilia maeneo ya mbali ambako tayari athari za tawala za kiislamu zilikwishatangulia.
Maeneo hayo ni kama vile kaskazini ya Afrika,Libya,Tunisia,Aljeria na Morocco mbali na maeneo ya ndani ya kama vile MalimChad na Niger.

Kwa upande wa Ulaya ya sasa waislamu walikwishatangulia Spain zamani. Mmoja ya waliofanikiwa kuhama na kuendeleza mfano wa tawala za Baghdad ni Abulrahmaan ambaye alikwenda kufanya makazi yake Cordoba chini ya himaya ya Ummawiyah. Miji mingi sana ndani ya Spain iliyojulikana wakati huo kama Andalus ilijengwa kwa nidhamu za tawala za kiislamu ambapo lazima kuwe na maktaba.Miji michache kati ya hiyo ni Granada,Sevile na Toledo.

Kwa mfano papa Sylvester (Gerbet) ni miongoni mwa wakristo wa mwanzo kusoma kwenye chuo kikuu cha kiislamu cha Granada na aliwahi kuhudhuria mafunzo chuo kikuu kikongwe zaidi duniani cha Alqarawiney ambacho kiko Fez nchini Morroco ambacho bado kinaendeshwa kwa mfumo ule ule maarufu kama madrasa.

Papa Syvester ambaye alivutiwa sana na utamaduni wa waislamu na elimu zao alipenda sana somo la hisabati na ndiye wa mwanzo kuingiza elimu hiyo nchini Italy wakati wa utawala wake ambapo mwenyewe alikuwa ni mwalimu pia pamoja na kazi za upapa (1095).

Maktaba ya Toledo ndiyo maarufu zaidi kwani hapo ndipo makabila mengi ya Ulaya kuanzia Ureno, Ufaransa,Italy na kote kwengineko walisoma na kutafsiri kazi hizo kutoka lugha ya kiarabu na kuingiza kwenye lugha zao za asili. Katika maktaba hiyo pia walikuwepo wafasiri walioweza kuingiza elimu hizo kwenye lugha ya kiyahudi ya kiebrania.

Ikumbukwe wakati ulimwengu wa kiisalamu ukiwa unairithisha dunia elimu kwa lugha zao kutoka kiarabu lugha maarufu za sasa kama vile kiiengereza na kifaransa hazikuwepo au ndio muda zilikuwa zinazaliwa na kuanza kujulikana.

Vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya kiarabu na kutumika kwenye vyuo vikuu vingi vya ulaya walivyojenga wenyewe ni vingi sana.Ngoja tutaje baadhi tu ya vitabu hivyo.

1. AL HAW. Ni kitabu cha tiba kiliandikwa na Abubakr Al Razi (864 -935)AD.Kinajumuisha vitabu vidogo (volumes) 23.Kilitafsiriwa kuingizwa lugha ya kilatin na myahudi aitwaye Faraj ben Salim kutoka visiwa vya Sicily mnamo mwakka 1276.

2. AL QANON FIY TTIB cha tiba kwa kiiengereza kinajulikana kama The canon of medicines. Kiliandikwa na Ibn Sina (980 -1037)AD.Kitabu hicho kimetumika kama rejea kubwa kwenye vyuo vikuu vya Ulaya mpaka mwaka 1650.Kilikuwa kikitoa ufafanuzi wa tiba na madawa kwa kutumia michoro kufahamisha vizuri.

3. KITAB AL TASIF cha Abul Qassim (936-1013)AD.Ni mkusanyiko wa vitabu vidogo 30.Abulcasis ndiye mvumbuzi wa vifaa zaidi ya 200 vinavyotumika mpaka leo kwenye vyumba vya upasuaji na vitabu vyake vimetumika kufundishia Ulaya kwa zaidi ya miaka 500.Aliishi na kufia mjini Cordoba ndani ya Spain.Nyumba yake mpaka leo ipo na imepewa thamani ya juu katika utalii wa majengo.

4.AL KITAB AL MUKHTASAR FIY HISAB ALJABR WAL MUQABALA.Kiliandikwa na Muhammad bin Mussa Alkharizm (780-850).Alikuwa ni mmoja ya wafanyakazi mashuhuri wa kitengo cha kutafsiri maandishi kwenye jengo la Baitul Hikma na baadae akawa ndiye mkurugenzi wa kituo hicho.

Pamoja na kazi nyingi alizozifanya alisoma na kutafsiri maandishi ya Euclid, mwanafalsa wa zamani wa kigiriki.Hata hivyo maandishi na hesabu zake za Aljebra ambazo ndizo zilizozalisha ujanja wote wa hesabu duniani haujaonekana kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na michoro ya maumbile ya Euclid.

Nakala halisi ya kitabu cha Alkhwarizm katika hati zake za kiarabu kinapatikana kwenye maktaba ya chuo kikuu cha Oxford nchini Uiengereza.
Kama mwarabu wa uarabuni angeandika haya labda ningeona anapromote kilicho chake. Ila sasa ni mwarabu mweusi kama mkaa ndio anarukaruka hapa hata babu zake waliosababisha uwepo wake amewasahau 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuhusu QUran usinilazimishe kusema unavyotaka ili utukane tu kama walivyofanya wenzako humu humu JF na wakashindwa kwa hoja.
Nimegundua hata maana ya sayansi huijui.Soma hapo chini.
Science is the systematic study of the structure and behaviour of the physical and natural world through observation, experimentation, and the testing of theories against the evidence obtained.
"the world of science and technology"
Kwa maana hiyo kabla ya kuteremka Quran na yaliyotendwa na waislamu pale Baghdad hakukuwa na sayansi.Kilichokuwepo ni falsafa ambazo zilikushanywa na waislamu na ikawa kama ni gia ya kuanzisha sayansi,
Kazi ya majaribio na uwekaji data kwa mara ya mwanzo ulifanywa na akina Avicenna na Ibnu Hayyan.Wanahistoria wote wa sayansi wanalijua hilo isipokuwa wewe kwa vile hujui hata maana ya sayansi
Sayansi inaenda na evidence.

Quran inasema kuna Mungu, Allah ni Mungu.

Quran imetoa evidence gani kwamba huyo Allah yupo?
 
Back
Top Bottom