Ndugu yangu haya mambo ya maendeleo inategemea unatumia vigezo gani. Mimi pia niliwahi kwenda Afrika kusini ya Mandela mwaka 1995, 1996 na 1997 kwenye mikutano siku moja nikisafiri kwa treni nilishangaa na kusonononeka sana kupitia dirisha la treni ilikuwa alfajiri saa 11 niliona familia moja ya kiafrika baba, mama na watoto watano ikinyeshewa na mvua kwenye nyumba yao iliyojengwa kwa maboksi na kuezekwa na katarasi ya plastiki bahati mbaya kulikuwa na baridi kweli nilitamani kulia. Nitakuja kukueleza mengi niliyoyashuhudia nchi ya Mandela huyo unayemsifia.
Kwa hiyo kwa kuiangalia familia hiyo moja iliyokuwa ikipigwa baridi nje ukahitimisha kuwa the whole SA wako nje hivyohivyo wanapigwa baridi nje??
Ungemfanya vizuri na kueleweka kama ungejenga hoja yako ya kum - challenge mleta hoja kwa wewe sasa kutaja na kuchambua vigezo vya maendeleo na kuvi - relate na ulichoona huko SA vs Tanzania..
Baada ya hapo ulinganishe maendeleo ya TZ na SA Kisha utoe conclusion yako. Unfortunately, hujafanya hivyo..!
Lakini
all in all na bila kumung'unya maneno kabisa, kiwango cha maendeleo ya
Tanzania kwa miaka 63 ya uhuru viko chini sana na hatukupaswa kuwa hapa tulipo bali tulipaswa tuwe level moja na nchi kama Singapore, Malaysia nk..
Na tatizo kubwa na ambalo ndilo kikwazo cha Tanzania kupiga hatua za haraka za kimaendeleo kijamii na kiuchumi ni ukosefu wa
SIASA SAFI na
UONGOZI BORA.. toka
Chama Cha Mapinduzi - CCM ambao ndio wao tu tangu wakati huo wanatoa uongozi wa nchi hii..
Solution ni sisi wana wa nchi hii kubadili
mindset zetu na kuachana na mfumo huu wa utawala usiobadilika wala kubadilisha chochote tangu uhuru mwaka 1961..
Ifike time tuseme kwamba, TUNAKATAA ULOZI WA CCM ambao umewaloga watanzania wote na kuwa kama mazezeta...