Kiasi gani Wazungu wametuacha kiteknolojia

Kiasi gani Wazungu wametuacha kiteknolojia

Habari wanamember,

Kwanza kabisa nataka niweke bayana wazungu ambao nawazungumzia, hawa ni wazungu ambao walikuja huku kwetu Afrika na kututawala, kwa kesi yetu ya Tanzania nitawaongelea Wajerumani na Waingereza.

Kipimo nitakachokitumia kupima uwiano ni miaka, kwamba itatuchukua miaka mingapi kufika umahiri walionao wenzetu katika teknologia. Teknologia inatafrisiwa kama kutumia ujuzi wa kisayansi katika kufanya mambo yenye manufaa kwa jamii.

Kutokana na kufanyika mradi mkubwa wa reli SGR hapa tanzania nitatumia reli kama uwanja wa kutupima sisi watanzania na wazungu, haya ndo majibu yanayopatikana

WAMETUZIDI MIAKA >200+
Treni na reli kwa wazungu sio kitu kigeni kwani wanacho tokea miaka ya 1800, hivyo basi kutokana na sisi mpaka sasa kutokuwa na uwezo wa kutengeneza treni na reli yetu hivyo inatuonyesha ya kwamba ni miaka zaidi ya mia mbili wapo mbele.

Hii inamaanisha kama ni umri basi wao wapo mbele miaka mia mbili na zaidi hali hii inawafanya kuwa na uzoefu mkubwa sana kulinganisha na sisi, chukulia mfano mtu mwenye uzoefu wa miaka kumi alivyo kuwa mjuzi itakuwa vipi kwa mtu mwenye uzoefu miaka mia mbili na zaidi.

Kutokana na kuwa na jibu ambalo sio number kamili ( miaka mia mbili na Zzidi) nataka kutumia baathi ya nadharia ili kufanikisha adhimio langu la kupata miaka kamili ya kiasi ambacho tumepitwaa na wazungu hivyo natumia kigezo cha utambuzi wa majengo ya kihistoria ambapo kwa Tanzania jingo la utambuzi unaanzia miaka 1868 na kushuka chini, na ukiangalia Wajerumani nyumba zao za kihistoria zinanza miaka ya 1300 sasa kwa kufanya hesabu za kutoa. Tupapata tukitafutacho.

1868 – 1300 = 568

Hivyo basi napenda kuhitimisha mjadala wangu kwa kusema ya kwamba tumepitwa miaka mia tano na sitini nane.

Najua ya kwamba njia yangu ina mapungufu kaza wa kaza kwani jengo la zamani tanzania lilijengwa na sultani OLD BOMA na sio na wazawa. Hii miaaka ambayo inaonyesha tumepitwa inaweza kutasfiri katika Nyanja mbalimbali.

Tunakuwa vichekesho ambako tunasema wasituingilie mambo yetu ya ndani, ni kama umekuwa kaka unatoa ushauri kwa dogo asije akapotea kwa sababu umeona mengi na unawajibika kutoa ushauri.
Umeandika sana ila hoja ni kutaman maendeleo ya mataifa ya kibepari bila kujua wamefikaje au wamepataje ni ushamba wkt unawaza teknolojia mpya waza baada ya kuipata wanafanya nn je uko tyr wanaume kwa wanaume kuoana au kinyume chake bhas tusitaman tuwaze na changamoto zake
 
Anza kupinga hilo kwa kutopanda gari, kutotumia simu, kutoangalia tv n.k maana vyote hivyo ni vya mzungu. Maana hata siasa wametufundisha wao. Kila teknolojia ina changamoto zake. Mtoa mada big up sana, ambae hajawahi kujiuliza haya hana utashi wa kufikiri
 
Kwenye bulaki painter tumewazidi wazungu teknolojia sasa ukirudi duniani ni miaka laki elfu kuwafikia kimaendeleo.
 
Sasa ww umekua bais maana umeelezea upande mmoja wa westen countries peke yake..mbona ukuongea kuhusu teknologia iliyokuwepo Africa kama ya chuma,majengo ya kilwa ya zamani au wajua kwamba Sudan kuna mapilamidi mengi kuzidi Egypt kabla hayajalipuliwa na hao wazungu.....?
 
Anza kupinga hilo kwa kutopanda gari, kutotumia simu, kutoangalia tv n.k maana vyote hivyo ni vya mzungu. Maana hata siasa wametufundisha wao. Kila teknolojia ina changamoto zake. Mtoa mada big up sana, ambae hajawahi kujiuliza haya hana utashi wa kufikiri
We kidato cha kwanza ndo maana na wala hujui uchum wa dunia unasemaje unadhan ipo siku utakuwa km marekani?
 
Kosa kubwa walilofanya hawa wapigania uhuru mimi nawaita wapigaji ( kumfukuza mkoloni na kula wao) wangedai usawa yaani haki sawa ya kushiriki shughuli za uchumi wakawaacha tukashirikiana nao tungekuwa mbali sana

Good point
 
Umeandika sana ila hoja ni kutaman maendeleo ya mataifa ya kibepari bila kujua wamefikaje au wamepataje ni ushamba wkt unawaza teknolojia mpya waza baada ya kuipata wanafanya nn je uko tyr wanaume kwa wanaume kuoana au kinyume chake bhas tusitaman tuwaze na changamoto zake

Wewe unaenda nje ya mada, same sex relationship sio takwa la kuwa na maendeleo ya teknolojia!
 
Wametuacha milele

Mpaka sasa eti tunahangaika na maji safi na salama alafu unawaza teknolojia na wazungu
Siku ile mh. Rais akikabidhiwa ripoti ya makinikia kuna mzee mmoja wa CCM anaitwa Butiku aliongea pale akasema wazungu wametuzidi kwa zaidi ya miaka LAKI MBILI ila nadhani ni sahihi zaidi wewe ulivyosema MILELE.
Yani kwa kifupi tukitaka kuwafikia wazungu kimaendeleo labda tuombe Mungu awaangamize wote (extinction) kisha miafrika tupambane.
 
Kuna tatizo sana la uelewa na namna ya kufikiri, tatizo ni kuwa watu wanaongea tuu kwa mihemko, ila kiukweli waliofika wanajua ni jinsi hani mtoa mada yupo sahihi na hapo ameongea partially tuu. Wametupita mno, mimi nilipokuwa kule niliwaza wakati wazee wa kule wanafanya yote yale huku machief na wafalme walikuwa wanafanya nn? Hata majengo ya kihistoria mnayoyaona mengi ni ya waarabu na sio wazawa asilia. Viongozi badala ya kujitahidi kujenga ushirikiano wenye maslahi na mataifa haya kwa exchange ya resources wao wanajigamba tuu kuwa sisi matajiri, sisi ni masikini sana. We need change of mentality kwa viongozi wetu km ambavyo Rwanda wanajitahidi na pia change of mindset kwetu Afrika. 1. Kujua uzalendo halisia na kujitoa kwa taifa na bara la Africa. 2. Management ya muda, Time management ni tatizo kwetu; wakati sisi tuna muda walioendelea wana saa. 3. Hard working spirit, sio kulala tuu na kuwaza ngono na kula, we need to really work very hard, kila mtu katika kila anachokifanya. 4. Kuzifanyia kazi ndoto sio kuendelea unaota ndoto unawaza mafanikio bila kuchukua hatua, use the available resources at hand and make a change. 5. Viongozi wabadilike, huu ni muda wa Demokrasia na sio kuburuzana kama mang’ombe wakati watu tuna akili timamu na tunajua mambo, viongozi wa Afrika ni wabinafsi sana na wanajali madaraka yao, mawazo yao na ubabe kwa wapinzani, badala yake wawe wanaongoza nansio kutawala, wakatibishe inclusion ya kuongoza na resource and technological sharing between us and the developed nations but isiwe Marekani, marekani na China ni mataifa jeuri watatumaliza, hawana ubinadamu wala urafiki wao kila kitu ni fursa yao na hasara for the other!
 
Unaongelea watu ambao wanamikakati ya kuanzisha utalii nje ya sayari hii. Yaani mkaone mwezi, Mars n.k. Huwa nikiwafatilia hawa ndo naamini dunia inaenda kuwa kijiji na utawala wa nchi kama nchi unakuwa ni wa maigizo tu. Sasa mfano nchi zetu za Africa zina siri Gani dhidi ya mabeberu? Simu tu tunazotumia ni zao, wakiamua turudi zama za mawe tunarudi tu.
 
Umeandika sana ila hoja ni kutaman maendeleo ya mataifa ya kibepari bila kujua wamefikaje au wamepataje ni ushamba wkt unawaza teknolojia mpya waza baada ya kuipata wanafanya nn je uko tyr wanaume kwa wanaume kuoana au kinyume chake bhas tusitaman tuwaze na changamoto zake
Nimesema technology ni sehemu mojawapo ya mambo ambayo wametuzidi, hii stage ya kukataa ushoga walishapita long time ago, ndo maana nikasema wanapotuambia mambo tusizani wamewehuka bali n hekima walizopata kutokana na historia ndefu waliyonayo, nakadiria miaka mia ushoga litakuwa jambo la kawaida sana afrika
 
Sasa ww umekua bais maana umeelezea upande mmoja wa westen countries peke yake..mbona ukuongea kuhusu teknologia iliyokuwepo Africa kama ya chuma,majengo ya kilwa ya zamani au wajua kwamba Sudan kuna mapilamidi mengi kuzidi Egypt kabla hayajalipuliwa na hao wazungu.....?
Imebidi niwaweke wao ili kupata number ambayo italeta maana endapo ningesema niwaweke warumi au waigiriki tungepoteana humu. Kuhusu chuma ndo usiseme kabisa kwani german zama za chuma zipo miaka 800-450BC na ukija africa zama za chuma zipo 2-1000AD
Hivyo basi gape litakuwa
800+200 = 1000
Au
450 + 1000 = 1450
sasa ndugu umeona mwenyewe hamna pa kusingizia.
 
Wewe unaenda nje ya mada, same sex relationship sio takwa la kuwa na maendeleo ya teknolojia!
Nitakufundisha kwan ukitaja teknolojia unataja maendeleo na maendeleo huwa hayachagui halal wala haram kuwa na akili japo kdg
 
Nitakufundisha kwan ukitaja teknolojia unataja maendeleo na maendeleo huwa hayachagui halal wala haram kuwa na akili japo kdg
Same sex zimekuwepo hata kabla ya maendeleo na hata pasipomaendeleo zingalipo.Technology haina chain na homosexual
 
Kama tusingedai uhuru tungekuwa mbali Sana kiuchumi kuliko Latin america,Kosa kubwa ililofanya Africa baada ya uhuru ni kuacha sera za uchumi za magharibi na kufuata za mashariki zilizochochea ujamaa na udikteta
 
Malizia na kampeni za kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka washing room

Imagine mpaka karne hii bado tuna sumbuliwa na magonjwa ya milipuko kama kipindu pindu..it means sisi bado ni wachafu
Sisi ndio tuko kwenye kampeni ya kuhamasishana kujenga vyoo.

Bado sana!
 
Kwanini sisi hatukuwa pumbaza wao...Akili kubwa huitawala akili ndogo always
Hawajatuzidi kitu, sio washindani wetu.... walifanikiwa kutupumbaza na kutuondolea ufahamu wa asili yetu sasa tunahangaika tu.
 
Back
Top Bottom