Watu ambao hawajafahamika wamevamia nyumbani kwa mkazi wa Kibaha kwa Mfipa Mkoa wa Pwani, Melkisedeck Sostenes na kupora gari, pesa na vitu mbalimbali kisha kuwatumbukiza wanandoa kwenye chemba za vyoo.
Watu hao wanaodaiwa kutekeleza tukio hilo saa 12 asubuhi pia wanadaiwa kuondoka na mtoto mchanga mwenye umri wa miezi saba.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Alhamisi Januari 16, 2025 Sostenes amesema kuwa watu hao walifika nyumbani kwake jana saa 12 asubuhi na walimvizia alipokuwa akitoka ndani kwenda kulisha kuku bandani.
View attachment 3204158
========
My Take
Kuna Baadhi ya Matukio binadamu wenzetu wanafanya unashindwa uanzie wapi kuduwaa.
Lakini nawashangaa zaidi wanaosema hukumu ya kifo Ifutwe badala ya kuangalia aina ya matukio ya kuyapa hiyo hukumu.
Ndio maana wakati mwingine Huwa napata kigugumizi sana kuwaonea huruma watu walioko jela licha ya usemi kwamba sio wote walioko jela Wana makosa lakini ni zaidi ya 90% wanakuwa na makosa tena ya Ukatili,hapo kiukweli Huwa inaniwia vigumu kumhurumia mfungwa.
Poleni sana mliofikwa na haya.