Kibajaji amvaa vikali Zitto Kabwe kumsema Magufuli, amuita muoga kwani wakati yupo hakusema?

Tusifikiri kumsema vibaya Magufuli kutasaidia kitu, hayupo na hawezi kujibu kitu, kama una tatizo naye maliza utakuja kukutana naye kwa Mungu.

Mtu akishatangulia kitabu chake kinafungwa, tunamuachia Mungu kuja kutoa hukumu.
Idi amini na hitler mpaka leo tunawasema sembuse ibilisi magufuli
 
Sasa kwani Mbowe na Lissu waliacha kumkosoa Jiwe? Mbona walikuwa wanamkosoa na hata huyo Zitto alikuwa anakosoa ila sasa hivi hamkosoi Samia. Ila wale wa kijani wakiwashwa kumkosoa Samia yatawakuta kama yaliyomkuta Ndugai.
Zitto mbaguzi, hawezi kumkosoa SSH hata kidogo. Sio kwa sababu SSH anafanya vizuri, ni kwa sababu wa dini yake.
 
Kwani anayosema kuhusu Magufuli Yana ukweli ndani yake!? Tuanzie hapo ili kulinda legacy kama ipo
 
Ukiambiwe ukazikwe pembeni ya mpendwa wako, unapataje ukweli nadni yake? Kuna nini cha kutafuta hapo?
 
Hakujawahi kupatapo kuwa na hayo majukumu sijui wewe umeyatoa dunia gani aina hiyo ya majukumu? Kilichopo hapo ni kuamua nani umkosoe na yupi umfumbie macho kasoro zake usimkosoe si kusema et kugawana majukumu ya kukosoa hakuna kitu kama hicho ni kituko.

Zitto kaamua kufumbia macho kasoro za washirika wake maana wamemzibulia mirija ila anafanya mashambulizi kwa aliyekuwa mziba mirija yake, basi ni hivyo tu kama asingekuwa mshirikina huyu Zitto pengine ningeamini wasemavyo watu kuwa Zitto ni mdini ila Zitto hana hiyo dini kutwa kujisifu ushirikina.

Hayo utajua ww.
 
Alijitokeza. Lusinde aliongea bungeni. Na ni wangapi walimkosoa na bado wako hadi leo. Mnamkuzia mambo marehem

Jitahidi kuvumilia ukweli, kwako ni marehemu, kwetu sisi wengine ni kiongozi muovu.
 
Zitto mbaguzi, hawezi kumkosoa SSH hata kidogo. Sio kwa sababu SSH anafanya vizuri, ni kwa sababu wa dini yake.
Yule sidhani kama ni mdini ni mshirikina tu yule, ukiangalia kipindi cha kikwete alikuwa anapiga hela na ukiangalia sasa hivi na chama chake ndio utaelewa kwanini ana hasira na Jiwe.
 
Leo bungeni mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde amemvaa vikali kiongozi mkuu wa ACT, Zitto Kabwe kwa kumsema Hayati Magufuli. Kibajaji amemuita Zitto muoga kupitiliza kwani wakati Magufuli yupo hai hakusema mpaka ameondoka.

Pia Kibajaji amesema wote wanaomsema Magufuli ni wanafki na hata Samia akiondoka nae watamsema vilvile. Amemsifu Nyalandu kwa kusema kwa vitendo hawezi kufanya kazi na Magufuli wakati yupo hai na kuachia nafasi yake ya ubunge.

========

Kibajaji: Nchi yetu imeweka vizuri sana masuala ya utawala bora kisheria lakini kuna baadhi ya vyama kwa mfano pale Zanzibar, ACT tunashirikiana nacho kwenye utawala bora, sisi tuna Rais, tuna Serikali wao wana makamu wa kwanza wa Rais lakini mmesikia kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto anamnanga mheshimiwa Magufuli kana kwamba Zitto hashiriki kwenye Serikali.

Magufuli aheshimiwe, Zitto aelewe kwamba suala la kufiwa ni suala kubwa. Haiwezekani kwenye utawala bora tuache suala la Magufuli kuzungumzwa vibaya na mimi sitaacha.

Leo nnapoongea Waislamu mmefunga, dini inawakataza kuwasema vibaya marehemu, Zitto ni muislamu anajua.

Mheshimiwa Zitto anatutaka tunaompenda mheshimiwa Magufuli tukazikwe nae. Zitto amewahi kufiwa na mama yake, mimi sitaki kufika huko, mama wa Zitto ni mama yangu mimi. Mimi nimewahi kufiwa na baba yangu lakini ACT wamewahi kufiwa na makamu wa kwanza wa Rais, Zitto anatulazimisha sisi tuanze kumsema vibaya Maalim Seif, hatuwezi.

Inakuwaje watu mnakuwa waoga, viongozi wakiwepo hamsemi wakiondoka ndio mnasema, huu ni uoga uliopitiliza. Mtu mmoja tu alisema kwa vitendo kwamba yeye hawezi kufanya kazi na Magufuli, Nyalandu.

Aliachia ubunge akaondoka lakini watu tuliobaki hapa ni watu wa Magufuli na tumefanya nae kazi na tulikuwa tunamsifu.

Hawa watu ambao sasa wanamsema Magufuli ni wanafiki wakubwa, Samia akiondoka watamsema vibaya hivyohivyo, ni bora mimi Lusinde ambae niko wazi na siwezi kuacha.

Pia, soma=> Zitto: Wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato, alikuwa Rais fisadi zaidi kuwahi kutokea Tanzania
Hapo kafunga lakini kaweza kumwaga hasira hizo,tusubiri akifungulia...
 
Huyo mbunge nae mnafiki tu, ameshindwa kuzungumzia unafiki wa SSH? Naye ni muoga tu na mnafiki, SSH alimsema JPM vibaya kabla ya Zitto.
 
Leo bungeni mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde amemvaa vikali kiongozi mkuu wa ACT, Zitto Kabwe kwa kumsema Hayati Magufuli. Kibajaji amemuita Zitto muoga kupitiliza kwani wakati Magufuli yupo hai hakusema mpaka ameondoka.

Pia Kibajaji amesema wote wanaomsema Magufuli ni wanafki na hata Samia akiondoka nae watamsema vilvile. Amemsifu Nyalandu kwa kusema kwa vitendo hawezi kufanya kazi na Magufuli wakati yupo hai na kuachia nafasi yake ya ubunge.

========

Kibajaji: Nchi yetu imeweka vizuri sana masuala ya utawala bora kisheria lakini kuna baadhi ya vyama kwa mfano pale Zanzibar, ACT tunashirikiana nacho kwenye utawala bora, sisi tuna Rais, tuna Serikali wao wana makamu wa kwanza wa Rais lakini mmesikia kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto anamnanga mheshimiwa Magufuli kana kwamba Zitto hashiriki kwenye Serikali.

Magufuli aheshimiwe, Zitto aelewe kwamba suala la kufiwa ni suala kubwa. Haiwezekani kwenye utawala bora tuache suala la Magufuli kuzungumzwa vibaya na mimi sitaacha.

Leo nnapoongea Waislamu mmefunga, dini inawakataza kuwasema vibaya marehemu, Zitto ni muislamu anajua.

Mheshimiwa Zitto anatutaka tunaompenda mheshimiwa Magufuli tukazikwe nae. Zitto amewahi kufiwa na mama yake, mimi sitaki kufika huko, mama wa Zitto ni mama yangu mimi. Mimi nimewahi kufiwa na baba yangu lakini ACT wamewahi kufiwa na makamu wa kwanza wa Rais, Zitto anatulazimisha sisi tuanze kumsema vibaya Maalim Seif, hatuwezi.

Inakuwaje watu mnakuwa waoga, viongozi wakiwepo hamsemi wakiondoka ndio mnasema, huu ni uoga uliopitiliza. Mtu mmoja tu alisema kwa vitendo kwamba yeye hawezi kufanya kazi na Magufuli, Nyalandu.

Aliachia ubunge akaondoka lakini watu tuliobaki hapa ni watu wa Magufuli na tumefanya nae kazi na tulikuwa tunamsifu.

Hawa watu ambao sasa wanamsema Magufuli ni wanafiki wakubwa, Samia akiondoka watamsema vibaya hivyohivyo, ni bora mimi Lusinde ambae niko wazi na siwezi kuacha.

Pia, soma=> Zitto: Wanaompenda Magufuli wakazikwe naye Chato, alikuwa Rais fisadi zaidi kuwahi kutokea Tanzania
Pumbavu utamsemaje Maalim Seif kwa ubaya wakati hata siku moja hakudhulumu haki za wanyonge kama Magufuli, Lusinde jiheshimu tafadhali.
 
Hata hivyo, zitto hawezi kubadirisha uamzi wa wanaomkubali JPM, ila yeye namhurumia na Uisilamu wake!
Jihurumie wewe na dhambi zako acha Zitto Kabwe awalipue mlizidi sana, utekaji, udhulumaji, majivuno, kuhujumu chaguzi, kuwafanyia jinai viongozi wa vyama vya upinzani za kishenzi, mkaleta ukabila na ukanda pumbavu nyie.
 
Back
Top Bottom