Quote:-
"Sidhani kama kuna mtanzania anayefurahia kuona mambo yanayotokea Kenya."
Jawabu ni hapana, lakini life has to go on, wa-Tanzania tuliwa-support Biafra, baadaye tukajirudi na kuwa friends na Federal government of Nigeria, ndio maana ya siasa na kuganga yajayo badala ya kulalia yaliyopita, Kibaki, ameshaapishwa kuwa the next president wa Kenya for the next Five years, leo nilikuwa ninaaangalia TVT jinsi viongozi wetu wa upinzani walivyojitokeza kukosoa uchaguzi huo, lakini mwishoni wote wamekubali kuwa baada ya kuapishwa kwa Kibaki, haitakuwa rahisi kubatili matokeo, na wamewaomba wananchi wa Kenya kuweka taifa lao mbele zaidi ya special interest zao, je ina maana hawa nao wanam-support Kibaki? Jawabu ni hapana isipokuwa kama politicians wanaelewa kuwa rais aliyekwisha apishwa labda kuna uwezekano wa 25% kuwa anaweza kubadilishwa,
FMES,
Msimamo wangu juu ya hili ni kwamba lazima Wakenya watumie nguvu kumwondoa Kibaki hata kama kuna watu watakufa. Hii dhana ya kwamba Mluo hawezi kuwa rais ikiachiwa ipite basi mauaji kama tunayoyaona sasa kuna siku tena yatatokea Kenya, hata kama ni miaka 20 ijayo, maana kuna Mluo mwingine atakuja kuchaguliwa kuwa rais na wataiba tena.
Kikubwa kwa Afrika ni kwamba ifike mahali turudishe haki zetu hata kama baadhi ya watu watakufa na hii itakuwa fundisho kwa wale wanaoiba haki za watu. Kama Romania walivyomnyonga rais wao, viongozi wa nchi zingine zote
Eastern Europe wakaona bora kuachia madaraka. Wakenya wakimwondoa Kibaki, viongozi wengi wa Afrika watafikiria mara mbili kabla ya kuamua kuiba kura.
Huwezi kutibu cancer kwa kuondoa makali hapa na pale, inabidi tuumeze mwarobaini mkali kwa ajili ya kuwaondoa hawa mafisadi.
Mimi kwenye hili kweli limeniudhi na japo ni mpenda amani sana lakini
siko tayari kuibiwa haki yangu. Mabara yote yanabadilika, sisi tunaendelea kuwa wajinga, kuwa maskini, shauri ya magenge ya watu wachache sana ambao pamoja na kupewa maslahi makubwa mno, bado wanaona lazima waendelee kuiba.