Ni hivi , kama kuna Mwanaccm yeyote anayetegemea Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar kwa njia ya sanduku la kura basi ni vema akaendelea na shughuli zingine , kwa hali ilivyo Zanzibar tangu asubuhi ya leo , ambayo ndio siku ya uzinduzi wa kampeni za Maalim Seif wa ACT WAZALENDO hakuna namna yoyote ya Hussein Mwinyi kushinda , Hakuna!
Labda kama atatumia njia alizotumia baba yake ambaye ni Rais mstaafu , ikumbukwe kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar kwa njia ya kuteuliwa tu kwenye vikao vilivyofanyika Dodoma , hakuwahi kupigiwa kura na Wazanzibar.