Kibinadamu ilinibidi nilimrudishe binti wa dukani baada ya kujifungua lakini kibiashara nahisi nilikosea heri ningempa mtaji

Kibinadamu ilinibidi nilimrudishe binti wa dukani baada ya kujifungua lakini kibiashara nahisi nilikosea heri ningempa mtaji

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Katika moja ya duka kuna binti nilimweka alikuwa na uwezo wake wa kipekee, nilitokea kumkubali sana sio tu kwenye mauzo lakini hata kwenye kujitoa, uaminifu, kunipa ideas, kuweza kuvutia wateja, n.k.

Akiwa na mimba ya miezi 7 nilimwacha aende kupumzika kwao huku nikiendelea kumlipa, niliweka replacement mwengine kwa muda huo.

Mshahara nilikuwa namlipa 150K, Aliporudi nikamuongezea mshahara uwe 200K, allowance nikapandisha elf 2,500 hadi elf 3, hana haja ya kupanda daladala au bajaji anaishi karibu mwendo wa dakika 5

Sasa tangu arudi kwa muda zaidi wa mwaka hadi sasa mambo yamekuwa hayaeleweki,
  • kuna muda anauza kitu ila kurekodi kwa bei ya punguzo na kujikopesha hela ya mauzo, pesa huwa anazitumia kwenye matunzo na matibabu ya mtoto lakini kibiashara imekuwa ni tatizo.
  • wateja wamepungua, kwa nilichoambiwa muda mwingi yupo bize na mtoto, pia kufunga duka akienda clinic, kwenda kutafuta pampas, tishu, dawa, n.k.
  • kuna muda mazingira ya ndani ya duka yanakuwa rafu, tishu huku, michirizi ya uji kwenye meza, kitenge kule.
Nawaza hapa ni bora nimpe mtaji tu maana biashara inakoelekea itakuwa inahumhudumia yeye na mtoto wake
 
Kama ameanza udokozi
....
Anauza kitu bei hii anarekodi bei nyingine....

Fukuza hio ng'ombe.....

Huruma huruma huzaa dhambi atakufilisi....

Achana nae haraka sana, huyo ni mke wa mtu akalelewe huko!
 
Katika moja ya duka kuna binti nilimweka alikuwa na uwezo wake wa kipekee, nilitokea kumkubali sana sio tu kwenye mauzo yaliyonishangaza lakini hata kwenye uaminifu, kunipa ideas, kuweza kuvutia wateja, n.k.

Akiwa na mimba ya miezi 7 nilimwacha aende kupumzika kwao huku nikiendelea kumlipa, niliweka replacement mwengine kwa muda huo.

shahara niliokuwa namlipa ni 150K, Aliporudi nikamuongezea mshahara uwe 200K, allowance nikapandisha elf 2,500 hadi elf 3, hana haja ya kupanda daladala au bajaji anaishi karibu mwendo wa dakika 5

Sasa tangu arudi kwa muda zaidi wa mwaka hadi sasa mambo yamekuwa hayaeleweki,
  • udokozi wa kuuza kitu na kurekodi kwa bei pungufu kwenye daftari,
  • mara kadhaa kuchukua pesa ya mauzo na kusingizia kakopesha,
  • wateja wamepungua, kwa nilichoambiwa muda mwingi yupo bize na mtoto, pia kufunga duka akienda clinic, kwenda kutafuta pampas, tishu, dawa, n.k.
  • kuna muda mazingira ya ndani ya duka yanakuwa rafu, tishu huku, michirizi ya uji kwenye meza, kitenge kule.
Aisee.

Mfukuze mara moja bila kusita.
 
Yaani wewe huyo katiwa mimba hapo kwako kaondoka unarudisha matatizo tena.
Huyo ni mke wa mtu akakae na hiyo ng'ombe imejaza mimba wale hata vitunguu watajijua.
Nimesomesha binti langu limeishia kujazwa mimba tu.
Sina hamu kabisa.
Nimemwambia utakula ulikopeleka mboga,kuanzia sasa wee kaa huko huko na mwanao na huyo fwala sitaki kusikia chochote tena.
 
Kama ameanza udokozi
....
Anauza kitu bei hii anarekodi bei nyingine....

Fukuza hio ng'ombe.....

Huruma huruma huzaa dhambi atakufilisi....

Achana nae haraka sana, huyo ni mke wa mtu akalelewe huko!
Muelezeee usimfanyie roho mbaya km mwanzo alifanya ubinadamu ubinadamu wake bado upo ndani yake ukimwelezea nini ni nini na kwanini kinakua nini ataelewa na kujirekebisha tu ni binadamu huyo sio mnyama kwamba yeye ni mbuzi haelewi kitu
 
Huyo ameshazaa mtoto, majukumu yameongezeka.... anaona posho na mshahara havimtoshi...ameanza udokozi
Sio wa kumchekea,,,, fukuza haraka sana
 
Mungu atakulipia Kaka, mtoto amekuja na baraka hivyo duka litaongezeka tuu usijali 😅
 
Alikosea kuzaa na mwingine ilihali boss wake unaemlipa anapendeza upo. Aende kwa mmewe
 
kuna muda anauza kitu ila kurekodi kwa bei ya punguzo na kujikopesha hela ya mauzo, pesa huwa anazitumia kwenye matunzo na matibabu ya mtoto lakini kibiashara imekuwa ni tatizo.
Hii sentensi imenikumbusha mbali sanaaa sitaki kutia maneno hapa lakini, mimi nilitoa uamuzi wa kumfukuza yule ndugu.
 
Back
Top Bottom