Katika moja ya duka kuna binti nilimweka alikuwa na uwezo wake wa kipekee, nilitokea kumkubali sana sio tu kwenye mauzo lakini hata kwenye kujitoa, uaminifu, kunipa ideas, kuweza kuvutia wateja, n.k.
Akiwa na mimba ya miezi 7 nilimwacha aende kupumzika kwao huku nikiendelea kumlipa, niliweka replacement mwengine kwa muda huo.
Mshahara nilikuwa namlipa 150K, Aliporudi nikamuongezea mshahara uwe 200K, allowance nikapandisha elf 2,500 hadi elf 3, hana haja ya kupanda daladala au bajaji anaishi karibu mwendo wa dakika 5
Sasa tangu arudi kwa muda zaidi wa mwaka hadi sasa mambo yamekuwa hayaeleweki,
- kuna muda anauza kitu ila kurekodi kwa bei ya punguzo na kujikopesha hela ya mauzo, pesa huwa anazitumia kwenye matunzo na matibabu ya mtoto lakini kibiashara imekuwa ni tatizo.
- wateja wamepungua, kwa nilichoambiwa muda mwingi yupo bize na mtoto, pia kufunga duka akienda clinic, kwenda kutafuta pampas, tishu, dawa, n.k.
- kuna muda mazingira ya ndani ya duka yanakuwa rafu, tishu huku, michirizi ya uji kwenye meza, kitenge kule.
Nawaza hapa ni bora nimpe mtaji tu maana biashara inakoelekea itakuwa inahumhudumia yeye na mtoto wake