Aisee.Katika moja ya duka kuna binti nilimweka alikuwa na uwezo wake wa kipekee, nilitokea kumkubali sana sio tu kwenye mauzo yaliyonishangaza lakini hata kwenye uaminifu, kunipa ideas, kuweza kuvutia wateja, n.k.
Akiwa na mimba ya miezi 7 nilimwacha aende kupumzika kwao huku nikiendelea kumlipa, niliweka replacement mwengine kwa muda huo.
shahara niliokuwa namlipa ni 150K, Aliporudi nikamuongezea mshahara uwe 200K, allowance nikapandisha elf 2,500 hadi elf 3, hana haja ya kupanda daladala au bajaji anaishi karibu mwendo wa dakika 5
Sasa tangu arudi kwa muda zaidi wa mwaka hadi sasa mambo yamekuwa hayaeleweki,
- udokozi wa kuuza kitu na kurekodi kwa bei pungufu kwenye daftari,
- mara kadhaa kuchukua pesa ya mauzo na kusingizia kakopesha,
- wateja wamepungua, kwa nilichoambiwa muda mwingi yupo bize na mtoto, pia kufunga duka akienda clinic, kwenda kutafuta pampas, tishu, dawa, n.k.
- kuna muda mazingira ya ndani ya duka yanakuwa rafu, tishu huku, michirizi ya uji kwenye meza, kitenge kule.
Anacheka na nyani.Biashara haihitaji huruma kabisa.
Kabisa nina ndugu yangu hata mwanae akiumwa ikahitajika pesa ya matibabu hatoi ya biashara kabisa , ni mgumu kuliko kawaida na bisahara zake zimeshibaAnacheka na nyani.
Soon ajiandae kuvuna mabua.
Muelezeee usimfanyie roho mbaya km mwanzo alifanya ubinadamu ubinadamu wake bado upo ndani yake ukimwelezea nini ni nini na kwanini kinakua nini ataelewa na kujirekebisha tu ni binadamu huyo sio mnyama kwamba yeye ni mbuzi haelewi kituKama ameanza udokozi
....
Anauza kitu bei hii anarekodi bei nyingine....
Fukuza hio ng'ombe.....
Huruma huruma huzaa dhambi atakufilisi....
Achana nae haraka sana, huyo ni mke wa mtu akalelewe huko!
Huyo ameshazaa mtoto, majukumu yameongezeka.... anaona posho na mshahara havimtoshi...ameanza udokoziMuelezeee usimfanyie roho mbaya km mwanzo alifanya ubinadamu ubinadamu wake bado upo ndani yake ukimwelezea nini ni nini na kwanini kinakua nini ataelewa na kujirekebisha tu ni binadamu huyo sio mnyama kwamba yeye ni mbuzi haelewi kitu
Hii sentensi imenikumbusha mbali sanaaa sitaki kutia maneno hapa lakini, mimi nilitoa uamuzi wa kumfukuza yule ndugu.kuna muda anauza kitu ila kurekodi kwa bei ya punguzo na kujikopesha hela ya mauzo, pesa huwa anazitumia kwenye matunzo na matibabu ya mtoto lakini kibiashara imekuwa ni tatizo.