Ndio maana kwenye graduation zao husisitizaga uzalendo na kuto tumia mafunzo vibaya..
Raia wa kawaida wa Tz 'layman & women' Ni waoga Sana wa bunduki na vurugu for sure watu walio pitia mafunzo ya JESHI hawaogopagi bunduki na waki be manipulated ndio balaa.
Uko ndio tunapoelekea unafikiri vijana wanapenda kukalishwa bila ajira zozote za kueleweka.
Vijana wa JKT wanarudishwa majumbani wale wasio na watu wa kuwashika mkono lakini watoto wa wakubwa ni mwendo wa kupigiwa simu tu za maelekezo na kuitwa.
Maafande wanajibu shit kuwa jeshi halitoi ajira etii muwe wazalendo hakuna uzalendo kwenye njaa.
Watoto wao wanawaweka kwenye system chap madogo wengine wanarudishwa kwao, madogo wengine wenye mioyo mepesi huishia kujinyonga.
Ubaya JKT wanaorudishwa kitaa wanazidi kuwa wengi na kitaa pakavu balaa life lime tight.
Hawa watu wanahitaji tu supplier wa silaha kuanzisha vikundi vya kiasi na ubaya nchi yetu rasilimali inazo tena za kutosha za kupigania.
Huwezi wapa vijana mafunzo utegemee watakuwa humble maisha yao yote huku wakiona viongozi wa chama na serikali na maafande wao pekee wakila mema ya nchi na kulindana.
JKT wanatengeneza bomu la vikundi vya kiasi sio vya kigaidi ni suala la muda serikali ijitafakari sana namna wanavyo iongoza hii Tanzania.
Watu wanaumia ndani kwa ndani tena hasa vijana kitu ambacho ni kibaya sana.
Hawa watu wanahitaji supplier tu wa silaha maana kama chuki dhidi ya serikali wanazo hawaitaji wa kuwaambia hiki na hiki kibaya serikali imefanya na inafanya.