Kibiti mpaka laana ya Cabo Delgado: Part II

Andika tu mkuu, km wao wanawachafua wewe kwann usijisafishe ?
 
Kuna mwamba mmoja mshkaji wangu na yeye alikua miongoni mwa wanajeshi walioletwa kibiti baada ya operation oile kuwashinda polisi, kipindi hiko nakaa maeneo ya mkuranga. Mwamba ndio alikua ametoka mafunzo Israeli, e bwana eeh, alinambia mambo ya kutisha sana. Anasema nyie watu hamjui nini kinaendelea, haya mnayoyasoma ni sehemu ndogo sana ya kile ambacho kiuhalisia ndio kinaendelea.
 
peleka mikwara karume kwenye kahawa.
 
Katika nchi zetu hizi za Afrika, pale Utawala uliopo madarakani unaposhindwa ktk jambo fulani na kisha kusababisha Mgogoro au kero fulani kwa jamii, Utawala huo huwa unakimbilia kufanya Propaganda chafu (negative propaganda) ya kuwachafua wale Raia wote wanaoonekana kupinga au kukosoa Utawala uliosababisha kero hiyo kuibuka kwa kuwabatiza majina mabaya mabaya Kama vile Magaidi, waasi, wahaini, vibaraka wa mabeberu, nk, nk.

Kwa mfano, Jaribu tu kujiuliza Kama tatizo lililopo huko Cabo Delgado nchini Msumbiji ni Ugaidi wa Kiislamu, Je, kwa Nini Ugaidi huo upo katikà eneo hilo lenye machimbo ya gesi tu peke yake na wala siyo katika nchi yote ya Msumbiji?????? Why Cabo Delgado only and not other places?????

Turudi Tanzania, kwa nini Mauaji ya Watu yanayodaiwa kwamba yalifanywa na watu wasiojulikana kutoka katikà 'makundi ya kigaidi' yalitokea katika eneo moja dogo la MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji) pekee na wala siyo katika mikoa yote ya Tanzania ambayo Ina Waislamu wengi??? Kwa nini ilikuwa MKIRU peke yake?????

Nasikitika sana kusema kwamba hata hapa Tanzania nasi tumenusurika chupuchupu kukumbwa na janga kama hilo la huko Cabo Delgado nchini Msumbiji, kwa sababu scenario iliyopo huko jimboni Cabo Delgado ambayo imesababisha hizi vurugu zinazoendelea huko inafanana kwa karibu Sana na scenario kama hiyo iliyosababisha 'vurugu za Gesi' kule Mkoani Lindi na Mtwara miaka michache iliyopita. Rejea matukio ya vurugu za Gesi yaliyitokea huko Mtwara. Naamini kwa dhati kabisa kwamba endapo kama vurugu zile za Gesi zilizotokea kule Mtwara zingeendelea kwa muda mrefu, Basi Wananchi wa huko Mtwara na wao pia wangeitwa magaidi.
 
Una point mkuu.
Magaidi siku zoote wako kwenye mali tuuu 😂.
Na watu hawajiulizi!..
 
Ww unaweza kuwa jirani yangu kabisa
 
Umesema ukweli kabisa!
 
Funguka zaidi mkuu! Hii ni nchi yetu sote. Tuna haki ya kufahamu kila kitu!

Unaweza kutueleza zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…