Jamaa inaonekana bado hajaridhika kutimuliwa. Sasa anamsema kila mtumishi mwenzake maarufu wa Tanzania japo kwa mafumbo.
Anasema mzee wa ubungo ni tapeli wa kutupwa na ni mtu wa system.
Kuhani Moses wa temboni anadai amewahi kufukia jeneza uwanjani Mbagala akaweka alafa kwenye mkutano akafukua kama amagundua uchawi.
Analalamika yeye ametimuliwa kwa sababu ameweka kiingilio cha 500K kumuona wakati jamaa wa Temboni anakiingilio hadi cha 5,000,000. Wengine 1,000,000.
Anadai hajafukuzwa na Serikali bali wenzake walimuonea wivu maana alikuwa anakaribia kuikausha kawe.
Wakuu hii imekaaje. Jamaa anaongea kana kwamba Injili yake inawataka watanzania tu kwingine kafeli. Je, Bongo ndio wateja wakubwa wa injili ya mwendokasi na wepesi kutoa pesa za upako?
mbona mimi niliwahi kumuona huyo kuhani Musa na sikudaiwa hiyo milioni 5 anayosema. niliingia bure kabisa kumuona na nikasaidiwa bure kabisa mpaka matatizo yangu yameisha. na kizuri zaidi kipawa na karama aliyopewa na kwangu imeanza kufanya kazi kwa sababu ilikuwa ni sehemu ya maombi yangu mwaka wa tano sasa.
hizo unazosikia milioni 5 mpaka laki tano ni kadi za huduma ya ujenzi unaendelea pamoja na vifaa vya mikutano mikubwa kwenye viwanja vya wazi. na ni hiyari sio lazima. uwe nayo usiwe nayo utamuona bila shida yoyote.
baraka za kujenga madhabahu ya kudumu na inayotembea ni kubwa mno.
wazungu walitujengea makanisa ndio maana wanafanya mambo makubwa. ukienda kwenye kanisa alilojenga mzungu, ukiomba chochote kabla Mungu hajakujibu wewe anamtazama aliemjengea madhabahu hiyo kwanza ndio unafuata wewe.
na ukijitolea chochote katika ujenzi Mungu anasema na mtumishi wake kuhusu wewe ili baraka zake zikujilie. na ndio maana mtumishi anamwambia mtu nione ofisini.
wengi hawajui kosa la pastor Dominique, kosa lake ni kusema vitu ambavyo havikutakiwa kwenda hewani kwenye radio au mitandao au TV.
alitaka kufichua vitu hadharani na wapinzani wake wachawi, waganga, mizimu, mashetani na washirikina wakamuwahi kwa kumstaki kwa waliompa kibali cha kuifanya huduma yake. hilo tu ndio kosa lake. Mungu alimpa karama akashindwa kuwa na hekima ndani ya huduma na utendaji wake.
yote kwa yote asianze kuwazushia wenzake, kila mmoja amepewa kipawa na Karama yake kwa jinsi Roho yule yule atoae apendavyo.
sioni haja ya wao kulumbana .
na asiendelee kumpa sababu shetani ya kufurahia