Poleni sana na msiba wa Kibonde.
Najaribu kuwaza, Kibonde ni MC wa masherehe mbali mbali. Kuna wakati tulitaka kumbook tukakuta imekuwa full booked kwa jumamosi za takribani miezi minne mbele.
Sasa najaribu kujiuliza, endapo marehemu alikuwa amepokea advance (kishika uchumba) kwaajili ya kuwa MC kwenye harusi za watu, je pesa hizo ndugu zake watarudisha? Waliolipa kwa Mpesa Tigo Pesa au bank atleast wapo salama. Je, vipi kwa waliolipa cash? Yani walionana na marehemu kisha wakalipa na hawakuandikishiana popote pale
Kwa uhodari na jina alilokuwa nalo Kibonde kwenye ushehereshaji basi yawezekana kabisa kuwa atakuwa amefariki na pesa nyingi za watu waliotoa advance.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using
Jamii Forums mobile app