Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Kwanza kabisa nasikitika sana historia ya eneo hili kufichwa au kutokua wazi. Nimepita pita sana kila kona lakini sijawahi kuona hostoria yake.

Kanisa hili lilijengwa na Wajerumani kwa mawe miaka ya 1880. Ujio wa Wamisionari hawa ulitoa fursa kwa Kibosho kuwa na sehem ya ibada, kujengwa kwa hospitali kubwa ya Kibosho na seminari pamoja na sekondari.

Baada ya miradi hii Wamisionari hawa walienda kufia sehem moja inaitwa Kiweruweru ni makutano ya mito miwili Nsoo na Kilombanga hiyo sehem iliwekwa msalaba lakini ulivunjika miaka ya 2003(ni sehemu ya kihistoria pia).

IMG_20200706_141507.JPG

Kwa yeyote anaejua lolote kuhusu historia ya Kibosho karibuni.

Unaweza kuona maeneo hayo kupitia ramani hii👉
Google Maps

Kanisa hili linaweza kuwa kivutio kutokana na ukongwe wake na ujenzi wake na muonekano wake pia. Kwani kuna sehem nyingi kwa nchi zilizoendelea majengo kama haya yamekuwa vivutio vikubwa vya kitalii na kuingizia serikali mapato ya kutosha.

IMG_20200706_141429.JPG

Naamini hili eneo lingekuwa kwenye nchi zilizoendelea lingekuwa maarufu sana.
 
Kwa hiyo watu waache kusali ugeuzwe kuwa kivutio cha watalii, ILA unajua nini mwamba,wazungu wakije ga kitu kinadumu aseee
 
SaaMbovu una picha zake mkuu? Si ajabu haujafanywa kuwa kivutio? Yan pamoja na ukongwe wake bado umeshindwa kutangazwa? Dah [emoji24][emoji24][emoji24]inasikitisha sana asee huo msikiti ungekuwa Jordani watalii kibao
Picha ninazo Mkuu.
 
wazungu, maana una mentality za kikoloni.
Hao wachagga wenzako wa kirima, umbwe, sakaeni, kibosho kati, mwengu, sungu juu na chininndio watalii, nyie mnabeza wazungu et hawatutakii mema alafu mnataka waje kutaliii?
Wapi nimetaja mkuu🙄🙄? Au unataka ugomvi tu saivi?
 
wazungu, maana una mentality za kikoloni.
Hao wachagga wenzako wa kirima, umbwe, sakaeni, kibosho kati, mwengu, sungu juu na chininndio watalii, nyie mnabeza wazungu et hawatutakii mema alafu mnataka waje kutaliii?
Nadhani mtoa mada angepaswa kuhimiza wakibosho wenzie watumie kanisa hilo kwa ibada ila sio kushauri libadilishwe kuwa kivutio cha utalii. Mabeberu hawawezi kujenga kitu karne 3 zilizopita kisha warudi kuja kukishangaa maana hata huko kwao walijenga makubwa na mazuri kuliko hilo mapema kabla hawajaja huku.
 
Hili nalo kajenga nani? Mbona linaingiza watalii zaidi ya 6k kwa siku? Hao waliolijenga ndio wapo mpaka leo?

Una akili finyu sana
 
Attachments

  • Screenshot_20200706_092806.jpg
    Screenshot_20200706_092806.jpg
    668.2 KB · Views: 14
Back
Top Bottom