Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Acha uwongo haiwezi kuwa miaka hiyo
Sawa.
Nimefika kwenye msikiti huo. Nimepiga picha za ndani na kwenye Bango ambalo limeandika historia hiyo. Picha zipo kwenye laptop yangu. Nikipata muda nitaweka humu.
Then utajua kuwa mie ni muongo au la.
 
Zuri sana,hata mazingira yalivyo kama mbele kabisa.
 
Moshi yote cjaona kanisa la kale lenye mvuto kama hili, nilishasali hapa nikiwa kibosho hospital,,, ni moja ya hazina ya kanisa catholic Tanzania
Hakika tembea yangu sijaona kanisa la zamani kubwa na design ka ile,naona ulaya tu
 
Acha uwongo haiwezi kuwa miaka hiyo
Unaweza kusoma hilo Bango hapo. Then useme nani Muongo.
images-20.jpg
images-9.jpg
images-8.jpg
 
Kwanza kabisa nasikitika sana historia ya eneo hili kufichwa au kutokua wazi. Nimepita pita sana kila kona lakini sijawahi kuona hostoria yake.

Kanisa hili lilijengwa na Wajerumani kwa mawe miaka ya 1880. Ujio wa Wamisionari hawa ulitoa fursa kwa Kibosho kuwa na sehem ya ibada, kujengwa kwa hospitali kubwa ya Kibosho na seminari pamoja na sekondari.

Baada ya miradi hii Wamisionari hawa walienda kufia sehem moja inaitwa Kiweruweru ni makutano ya mito miwili Nsoo na Kilombanga hiyo sehem iliwekwa msalaba lakini ulivunjika miaka ya 2003(ni sehem ya kihistoria pia).

View attachment 1499102
Kwa yeyote anaejua lolote kuhusu historia ya Kibosho karibuni.

Unaweza kuona maeneo hayo kupitia ramani hii👉
Google Maps

Kanisa hili linaweza kuwa kivutio kutokana na ukongwe wake na ujenzi wake na muonekano wake pia. Kwani kuna sehem nyingi kwa nchi zilizoendelea majengo kama haya yamekuwa vivutio vikubwa vya kitalii na kuingizia serikali mapato ya kutosha.

View attachment 1499103
Naamini hili eneo lingekuwa kwenye nchi zilizoendelea lingekuwa maarufu sana.

Tanzania tumejikita kwenye utalii wa vitu natural tuu, wenzetu kama India wanapiga hela za utalii sana kutoka kwenye majengo ya kihistoria lakini pia wanajenga majengo unique ili kuvutia wataliii mfano India kuna lotus temple linavuta watalii mno!

Dubai wanajenga majengo vivutio kila leo, ni projects kabisa
 
Tanzania tumejikita kwenye utalii wa vitu natural tuu, wenzetu kama India wanapiga hela za utalii sana kutoka kwenye majengo ya kihistoria lakini pia wanajenga majengo unique ili kuvutia wataliii mfano India kuna lotus temple linavuta watalii mno!

Dubai wanajenga majengo vivutio kila leo, ni projects kabisa
Kuna mjinga humu kasema mzungu hawezi kushangaa alichojenga yeye....nimemdharau sana
 
Kuna mjinga humu kasema mzungu hawezi kushangaa alichojenga yeye....nimemdharau sana

Tumepishana uwezo wa kufikiri na mitizamo mkuu, mpotezee! Kikubwa hao ndiyo waswahili walivyo, kukatishana tamaa na kufelishana kabla ya kuanza kufanya jambo.

Ukikomaa ukafanikiwa wanageuka na kusema tulimshauri sisi mpaka katoboa😂😂😂

Kuna Wajerumani nilikutana nao miaka ya nyuma kidogo walikuja kuangalia Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), waliyasoma hayo majengo kwenye maandiko huko kwao na waliyajenga wao!

Hapo vipi?
 
wazungu, maana una mentality za kikoloni.
Hao wachagga wenzako wa kirima, umbwe, sakaeni, kibosho kati, mwengu, sungu juu na chininndio watalii, nyie mnabeza wazungu et hawatutakii mema alafu mnataka waje kutaliii?
Ww utakua umesoma Umbwe au Lyamungo maana umekariri chocho zote za Kibosho
 
Nadhani mtoa mada angepaswa kuhimiza wakibosho wenzie watumie kanisa hilo kwa ibada ila sio kushauri libadilishwe kuwa kivutio cha utalii. Mabeberu hawawezi kujenga kitu karne 3 zilizopita kisha warudi kuja kukishangaa maana hata huko kwao walijenga makubwa na mazuri kuliko hilo mapema kabla hawajaja huku.
Tena unakuta kuna mengine ya kale kweli halafu makubwa na adornment zake zimesimama mpaka leo, vioo vipo vilevile (mfano westminister abbey).

Mabeberu wenyewe wanashangazwa na engineering skills za wajenzi wa muda huo ukizingatia kulikuwa hakuna chuo cha masomo hayo.

Hayo makanisa ya miaka 100-200 yapo kibao sasa hivi watu wananunua wanageuza nyumba binafsi za kuishi sema awaruhusu tu kuvunja structure.
 
Back
Top Bottom