Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Nadhani mtoa mada angepaswa kuhimiza wakibosho wenzie watumie kanisa hilo kwa ibada ila sio kushauri libadilishwe kuwa kivutio cha utalii. Mabeberu hawawezi kujenga kitu karne 3 zilizopita kisha warudi kuja kukishangaa maana hata huko kwao walijenga makubwa na mazuri kuliko hilo mapema kabla hawajaja huku.
Kabisa, mtoa mada hana exposure, ni sawa na yule anayejinadi kila uchao na interchange za ubungo, nahisi hajafika hata Nairobi akashangae na roho yake
 
Kanisa la kwanza kujengwa Kilimanjaro lilikuwa Ni Kanisa la Kilema (Mt. Bernadeta) mwaka 1890. Kwa taarifa yako ndio palikuwa makao makuu ya Jimbo hadi mwaka 1961 yalipohamishiwa Kristu Mffalme Moshi.
Ishu sio ukwanza hata muonekano pia
 
Huko Moshi ni kuzuri sana. Hili ni kanisa la kwanza kijengwa huko Kilimanjaro lipo Kilema. Wamissionari wa kwanza kabisa Moshi walishukia hapa Kilema.
 

Attachments

  • A7523143-AD7A-4667-B25E-EDDB5C1F2CBB.jpeg
    A7523143-AD7A-4667-B25E-EDDB5C1F2CBB.jpeg
    99.3 KB · Views: 16
Nchi hii ina vivutio vingi vya kitalii tatizo sijui liko wapi?

Lkn kidogo nauona mwanga, maeneo mengine sasa yanatazamwa tulikuwa vipofu kwa kuaminishwa maeneo machache ndio utaliii.

Nenda KAREMA ziwani huko Tanganyika kuna kanisa linamiaka kibao.

Ona lile meli MV LIEMBA lina miaka kibao nahistoria yake ya kuvutia.

Tabora zile TRAIN za kutumia mvuke zimeharibiwa hivi majuzi kwa wivu tu!
 
Mtoa mada hapa nilipo yapo ya miaka ya 1700s na 1800s ila mengi sasa yamegeuza hosteli za wanafunzi na kutumika kwa matumizi mengine.

Ila kwa huko kwetu huo ni urithi mzuri unaosimama kama ushahidi wa mabadiliko na ujio wa tamadani zingine
 
Limefanana kama la kibosho umbwe

Niliwahi fika kuna chuo cha nursing kama sikosei nilikuwa naelekea mwika chuo cha utalii

Nisehemu nzuri yenye uwoto wa asili
 
Hayo yamejengwa kwa mawe na mabeberu,,,Kuna kanisa lipo huku ushirombo lilijengwa kwa miti na mababu ( watumwa) enzi na enzi. kilikuwa Ni kituo kidogo Cha watumwa toka Burundi , Uganda, Rwanda na Tanzania kabla hawajapelekwa tabora kituo kikuu then zenji.ukiliona kenchi zake na bolt zake kwa Sasa hakuna miti ya namna hiyo.
 
Nchi zilizoendelea makanusani yanauzwa na kuwa miskiti au lodge. Wewe uko dunia gani ?
 
Hayo yamejengwa kwa mawe na mabeberu,,,Kuna kanisa lipo huku ushirombo lilijengwa kwa miti na mababu ( watumwa) enzi na enzi. kilikuwa Ni kituo kidogo Cha watumwa toka Burundi , Uganda, Rwanda na Tanzania kabla hawajapelekwa tabora kituo kikuu then zenji.ukiliona kenchi zake na bolt zake kwa Sasa hakuna miti ya namna hiyo.
Mkuu babu zetu walitumia bolt au mi sijaelewa[emoji848][emoji848]?
 
Back
Top Bottom