Kibosho Catholic Church lina umri wa miaka 130: Kwanini hili Kanisa lisiwe kivutio cha utalii?

Kabisa, mtoa mada hana exposure, ni sawa na yule anayejinadi kila uchao na interchange za ubungo, nahisi hajafika hata Nairobi akashangae na roho yake
 
Kanisa la kwanza kujengwa Kilimanjaro lilikuwa Ni Kanisa la Kilema (Mt. Bernadeta) mwaka 1890. Kwa taarifa yako ndio palikuwa makao makuu ya Jimbo hadi mwaka 1961 yalipohamishiwa Kristu Mffalme Moshi.
Ishu sio ukwanza hata muonekano pia
 
Kanisa Ni la kibosho umbwe au lipi maana kibosho makanisa mengi na yanafanana
Siyo kibosho umbwe ni kibosho msinga kanisa lipo karibu na hospital ya kibosho msinga hapo hapo kwa chini kuna chuo cha muda mrefu sana.
 
saivi parokia yetu ya otaruni inajengwa.
 
Nchi hii ina vivutio vingi vya kitalii tatizo sijui liko wapi?

Lkn kidogo nauona mwanga, maeneo mengine sasa yanatazamwa tulikuwa vipofu kwa kuaminishwa maeneo machache ndio utaliii.

Nenda KAREMA ziwani huko Tanganyika kuna kanisa linamiaka kibao.

Ona lile meli MV LIEMBA lina miaka kibao nahistoria yake ya kuvutia.

Tabora zile TRAIN za kutumia mvuke zimeharibiwa hivi majuzi kwa wivu tu!
 
Mtoa mada hapa nilipo yapo ya miaka ya 1700s na 1800s ila mengi sasa yamegeuza hosteli za wanafunzi na kutumika kwa matumizi mengine.

Ila kwa huko kwetu huo ni urithi mzuri unaosimama kama ushahidi wa mabadiliko na ujio wa tamadani zingine
 
Limefanana kama la kibosho umbwe

Niliwahi fika kuna chuo cha nursing kama sikosei nilikuwa naelekea mwika chuo cha utalii

Nisehemu nzuri yenye uwoto wa asili
 
Hayo yamejengwa kwa mawe na mabeberu,,,Kuna kanisa lipo huku ushirombo lilijengwa kwa miti na mababu ( watumwa) enzi na enzi. kilikuwa Ni kituo kidogo Cha watumwa toka Burundi , Uganda, Rwanda na Tanzania kabla hawajapelekwa tabora kituo kikuu then zenji.ukiliona kenchi zake na bolt zake kwa Sasa hakuna miti ya namna hiyo.
 
Nchi zilizoendelea makanusani yanauzwa na kuwa miskiti au lodge. Wewe uko dunia gani ?
 
Mkuu babu zetu walitumia bolt au mi sijaelewa[emoji848][emoji848]?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…