Kibu Denis alipopewa uraia kwa njia ya mlango wa nyuma ilikuwa sawa ila ni kosa kwa Singida Black Stars kufanya kwa wachezaji wake

Wakuu em tuwekane sawa, anayeomba uraia ni mtu mwenyewe binafsi au Taasisi anayofanyia kazi?
 
Unauhakika gani na wakati ndugu zake wote mpaka mke wake na watoto wake wanaishi marekani
Kwa hili mkuu nadhani huna taarifa sahihi,kibu kakulia kwenye kambi za wakimbizi zilizopo hapa nchini hata na Geita gold mine wakati ipo ligi daraja la kwanza walimsajili kutokea kwenye kambi,na alipoanza kucheza geita timu za ligi daraja la kwanza zilianza kulalamika,kwa kuwa geita ni timu ya halmashauri wakafanya magumashi wakampa kitambulisho cha taifa,tatizo lilianzia hapo
 
Ili upate uraia uanatakiwa uishi Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi mfululizo.Kibu kaingia Tanzania akiwa mdogo kama mkimbizi kwenye kambi za wakimbizi Kigoma.

Timu ya Taifa chini ya mwalimu Paulsen ilikua inamuhitaji Kibu na Simba wakati huo pia inamsajili kutoka Mbeya City ikaongeza nguvu ili apewe uraia ili alete mafanikio kwa timu ya taifa na club yake mpya ya Simba.
 
Mara nyingi huwa naskip comments zako kwa sababu nakuchukulia kama mtu usije na hoja na msingi. Naona hata hili dogo umeshindwa kuficha ujinga wako
Kuficha ujinga wake ni lazima awe na akili inayofanya kazi hata kwa per cent ndogo.
Huyu mjinga hana hoja yeyote ya msingi.Ni miujiza anaweza kuingia JF na hata hapa labda anapata msaada wa kuingia.
 
Kunatofauti sana kibu denisi kakulia Tanzania,kasoma primary& secondary Tanzania,kaishi zaidi ya miaka kumi,akipewa uraia anakidhi vigezo vyote ondoa neno mlango wa nyuma ni kulingana na Sheria na taratibu ,hao kina bada na kayekhe wana miaka mingapi Tanzania?
 
Reactions: Tui
Iraia wa kibu ulikua na mashaka thus ukasibitishwa. Hao wengine ni total foreigners na hawajakaa nchi hata miaka miwili licha ya mitano inayotakiwa. Ajifunze kutofautisha
 
Kibu unamfananisha na mchezaji kafika Tanzania kwenye dirisha dogo..yaani ana miezi mwili Toka afike nchini..umeandika upuuzi
 
Unauhakika gani na wakati ndugu zake wote mpaka mke wake na watoto wake wanaishi marekani
Yani familia yake wanaishi Marekani yeye abakie huku ukimani, yani ata wewe mkeo na Wazazi wako wawe wanaishi Marekani halafu wewe uishi Bongo, Kuna mswahiili ambae hapendi kuishi Marekani Kama Raisi wa nchi na viongozi wake kila siku kiguu na njia wanaenda Marekani tena bila muahariko wowote kutoka kwa Viongozi wa leo zao, Raisi akipewa muhariko na RIHANA kutembelea studio yake Raisi atakimbia mbio kwenda uko Marekani, Sembuse Kibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…