Kibwana Shomari bado ni beki mzuri na mbishi hasa

Kibwana Shomari bado ni beki mzuri na mbishi hasa

Gamondi alinishangaza yaani anampa shavu la kulia Nkane mechi ngumu na wale Tabora huku Shomari akiwa kakalia mbao nilishangaa sana kwenye huu mpira bora aliondolewa aisee angeendelea kuua viwango vya wachezaji wengi tu.
Ila kabla ya kuonjeshwa asali mlishangilia Nkane alivyopangwa nafasi hiyo hiyo
 
Jana kwenye mechi ya Young African dhidi ya Tp Mazembe ndio kadhibitisha ubora wake kijana kacheza vizuri sana mbavu ya kulia unaweza kuzani Yao yupo uwanjani tu..
 
Jana kwenye mechi ya Young African dhidi ya Tp Mazembe ndio kadhibitisha ubora wake kijana kacheza vizuri sana mbavu ya kulia unaweza kuzani Yao yupo uwanjani tu..
Yao alivyoshuka kiwango msimu huu, ana kazi ya kufanya kumpokonya Kibwana hiyo namba. Nilitamani upande wa Kibabage nako kungekuwa na watu wenye viwango vikubwa zaidi ya hao wakina Kibabage
 
Jana huyu kijana kanikosha sana kwenye game na Al Hilal kipindi cha kwanza yule winger wa Al hilal Jean Claude Van Damme Girumugisha alionyesha kumsumbua sana mpaka professor Pacome akawa anashuka chini mara nyingi kumsaidia..
Lakini kipindi cha pili kilipoanza tu kijana aka change kabisa kaweka ulinzi wa kipolisi Jean Chaude van damme kila akigusa kijana yupo miguuni mpaka akaona isiwe tabu akahamia upande wa Boka lakini huko nako akakutana na mapafu ya mbwaa mbio zote na usumbufu vikafa.
 
Back
Top Bottom