Kicheko wa Efm achukuliwa Clouds

Watoto wa kishua bhana... eti EFM ndio wameanzisha Singeli!! Huku Ushenzini tupo na Singeli miaka na miaka sasa halafu mtu aseme EFM ndo wameianzisha!!! Ni kama mtu aseme Radio One ndio walianzisha Charanga hata kama ishakufa kibudu!!!!
 
Sasa hapo tatizo ni Clouds au Fredua mwenyewe?! Inakuwaje mtu ambae alikuwa nyota kwenye radio ghafla aje kufunikwa na Kipanya ambae ana miaka kibao yupo nje ya game?!

Hata kama Clouds watu wanaichukia lakini jamaa wanatoa sana fursa na ndio maana unakuta vipindi vyao vingi vimejaza watu... provided unaweza ku-deliver, Clouds watakubeba! Sasa ikiwa utaenda kufunikwa na uliowakuta au watakaokukuta that's your problem! Na utafunikwa kwa sababu inawezekana haukuwa competent kihivyo otherwise huwezi kufunikwa!
 
Dina Marios
Sasa Dina alitemwa au alienda maternity leave! Sasa wewe ulitaka wasiweke replacement hadi lini wakati martenity leave si chini ya 90 days na kile kipindi ni lazima kiende hewanu??! Na isitoshe ambae alim-replace alikuwa ni mwana-Clouds sema tu alikuwa hajapata fursa na alipoipata akaitumia kama ambavyo Carnnavaro wa Yanga alivyoitumia fursa ya Victor Costa kuwa majeruhi!!
 
Hapa nimepata sababu kwanini Kicheko ameamua kwenda Clouds!!! Nimeona posts kadhaa zikihoji "kumbe Kicheko ni yule Massawe Mtata!" Yaani watu walikuwa hawamjui... lakini fujo za pungufu ya 2 za Clouds zimewafanya watu wengi zaidi wamfahamu Kicheko... hapo hata kazi yenyewe hajaanza!

In short, tuichukie tu Clouds kwa nguvu zetu zote kama tunavyomchukia Diamond kv Wabongo tuna aleji na vitu au watu wanaofanya vizuri... the same happened to Kanumba!!! Lakini Mtangazaji anayependa fursa lazima aende Clouds kv Clouds wanatoa sana fursa kwa Presenters wao... ni wewe tu ushindwe kuzitumia!!
 

Mkuu, kutoa maoni si kwamba naichukia, mimi ni shabiki w clouds toka inaanzishwa na mpaka leo nasikiliza clouds japo siku hizi kuna redio station ambazo ni nzuri pia kama timez, na hio efm ambazo kwa kiasi kikubwa ziliweza kuichallenge clouds na ndiomana kuna kupindi ili shake.
Kumbuka unaweza kuwa competent lkn mazingira pia yakakunyima fulsa ya kuonyesha hiyo competence uliyonayo, mfano mdogo tu ni kwa dina marios baada ya kunyang'anywa kipindi cha leo tena.
 

Mkuu si kweli kwamba efm hawakufanya jitihada kuuendeleza muziki wa singeli.
Kumbuka efm ndio walioutoa muziki huo kutoka mtaani na kuuingiza redioni na hata kuupa vipindi maalum, na hata kufanya matamasha mbalimbali kuutangaza.
 
Wala sijasema unaichukia, nimesema "hata kama watu wanaichukia...!" Imetokea tu kwamba hiyo hoja imeambatana na post yako kv sikuona sababu ya kuandika independent post! Lakini hata wewe kama ni mfuatiliaji mzuri na msema ukweli, unaweza kukiri nilichosema kuhusu watu na Clouds ni kweli!!!

Halafu huyu Dina Marios wewe ni mtu wa pili nakusikia kwamba "alinyang'anywa kipindi cha Leo Tena!! Dina hakunyang'anywa kile kipindi! Dina alikuwa mjamzito kwahiyo alienda maternity leave! Je, ulitaka kipindi kisimame kimsubiri Dina?! Hell No, haiwezekani! Husna akachukua nafasi!! Yule Husna since then nae alikuwa Clouds sema alikuwa hajapata nafasi! Waswahili wanasema kufa kufaana; Husna aliposhika kile kipindi hakufanya kosa!! Sasa je, ulitaka baada ya kurudi likizo ya uzazi Husna angenyang'anywa kipindi wakati alikiendesha kwa ufanisi kwa muda wote?! Hiyo isingekuwa fair! Na ndio maana baada ya Dina kurudi likizo ya uzazi, akapelekwa Clouds TV huku wakiwa na lengo aanzishe kipindi kipya. Clouds Media wanafahamu kwamba Clouds TV iko bado sana kwahiyo walitarajia uwezo na uzoefu wa Dina tangia anaanza na Leo Tena ungesaidia sana kuipaisha Clouds TV endapo atakuwa na kipindi kitakachobamba kama ilivyokuwa Leo Tena!!

.. na kwa kauli yake yeye mwenyewe (Dina) alisema amepewa jukumu kubwa zaidi... kv walimuani anaweza, wakaone
 
Habari ndugu zangu ,

Kwa wale wakazi wa dar na wasikilizaji wa E-FM mtakuwa mnamjua huyu bwana anaitwa kicheko ambaye alikuwa anaendesha kipindi cha singeli nyakati za jioni pale E fm.

Sasa huyu jamaa bna kwa sasa ameshachukuliwa na Clouds FM ,na kusaini mkataba nao.

Sasa kwa sasa muda huu anahojiwa na clouda hawa wakina gea habib hapa na jamaa alivyo mjinga anapiga story zake za zamani jinsi alivyokuwaga mwizi. Hivi kweli haoni kama anajiaibisha na pia anafanya watu tumuone kuwa ni mtu mbaya. Na je hajui kuwa hawa clouds wanamtumia tu??


Ama kweli ujinga ni maradhi makubwa sana. Yaani mtu ametolewa na akina majizo then leo hii anakuja kuwa kama kalogwa
 
Huu mchezo hauhitaji hasira, mbona povu limekutoka Majizo?
 
Mkuu Gentamycine alisema apa kua alikuaga mwizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…