Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama walivyomtema nani?!Kama alivyotangulia kusema mchangiaji hapo juu. Anaenda Clouds watamtumia kisha watamtema hebu check Jose Mara,Fredwaa wapo wapo tu.
Kama walivyomtema nani?!
Sasa hapo tatizo ni Clouds au Fredua mwenyewe?! Inakuwaje mtu ambae alikuwa nyota kwenye radio ghafla aje kufunikwa na Kipanya ambae ana miaka kibao yupo nje ya game?!Mi sikubaliani na uamuzi aliochukua sababu anaenda kujimaliza.mfano mdogo tu ni kwa freduaa aliyekuwa redio free africa,huyu alikuwa mmoja wa watangazaji maarufu sana tz na alikuwa na kipindi chake peke yake ambacho alikimudu hasa lkn toka alivyohamia clouds,amepotea ,akina masudi kipanya wamemfunika kabisa.
Clouds wanachokifanya ni kumvurugia efm ili asiwepo wa kuwa challenge,mfano mdogo tu,muziki wa singeli ilikuwa ni code ya efm lkn toka wauvamie clouds imekuwa shida.
Ngoja tusubili na hiyo television ya efm sijui itakuwaje,maana naona clouds wanarundika tu watangazaji wengi wakati vipindi vichache, matokeo yake wanaishia kubanana kwenye kipindi kimoja.
Sasa Dina alitemwa au alienda maternity leave! Sasa wewe ulitaka wasiweke replacement hadi lini wakati martenity leave si chini ya 90 days na kile kipindi ni lazima kiende hewanu??! Na isitoshe ambae alim-replace alikuwa ni mwana-Clouds sema tu alikuwa hajapata fursa na alipoipata akaitumia kama ambavyo Carnnavaro wa Yanga alivyoitumia fursa ya Victor Costa kuwa majeruhi!!Dina Marios
Afadhari amehama akuze jina wengine tusingemjuaeti wanaume wa dar, huyo kicheko ndio nani?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yan mmmm...kila nikitaka kulisoma macho yanalegea chaaa...Duh!umeshusha gaazeti kabisa
Sasa hapo tatizo ni Clouds au Fredua mwenyewe?! Inakuwaje mtu ambae alikuwa nyota kwenye radio ghafla aje kufunikwa na Kipanya ambae ana miaka kibao yupo nje ya game?!
Hata kama Clouds watu wanaichukia lakini jamaa wanatoa sana fursa na ndio maana unakuta vipindi vyao vingi vimejaza watu... provided unaweza ku-deliver, Clouds watakubeba! Sasa ikiwa utaenda kufunikwa na uliowakuta au watakaokukuta that's your problem! Na utafunikwa kwa sababu inawezekana haukuwa competent kihivyo otherwise huwezi kufunikwa!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yan mmmm...kila nikitaka kulisoma macho yanalegea chaaa...
Ni usajili mzuri ambao Clouds Media Group wameufanya kwa kumchukua Kicheko. Kuanzisha mtindo fulani wa muziki na kuupromoti haina maana kwamba Redio zingine shindani zitashindwa kukupiku na kukiboresha kile ulichokiasisi. Ni kweli E fm wanaweza kuwa waanzilishi wa Singeli ila hata wao pia hawakufanya jitihada za dhati kabisa kuweka kuufikisha mbali huu mtindo mpya wa muziki wa " uswahili " na hapa sitawalaumu sana E fm kwani hata coverage yao tu nchini bado siyo kubwa.
Hivyo basi kutokana na coverage nzuri ya Clouds fm na jinsi wanavyojua kupromoti mambo yao nadhani Kicheko kwenda hapo amefanya la maana mno kwani sasa huu mtindo mpya wa muziki wa " uswazinyo " utasambaa nchi nzima na pengine hata kuweza kuibua vipaji vingi vilivyopo huko Mikoani ambavyo havijapata tu nafasi ya kuwa nurtured.
Nirudi kwa Kicheko. Kweli huyu kijana ni Animateur ( neno la Kifaransa linalomaanisha kuwa ni Mchangamshaji mzuri ) na ambaye anaweza kukufanya muda wote umfuatilie na umsikilize bila kuchoka lakini huku pia ukiburudika.
Hata hivyo SIPENDI niliache hili lipite hivi hivi na lazima niliseme hili ili kumsaidia Kicheko na kama kuna Mtu humu anajuana nae si vibaya pia akamfikishia huu ujumbe murua ambao naamini akiuchukua basi utamjenga sana na huko mbele atafika mbali na kufanya makubwa ambayo yatamtangaza vyema na kumpa mafanikio.
Kote alikokua na hadi akawa anafukuzwa Kazi na Waajiri wake huku akiwa haelewani na wenzie kuanzia East Africa Radio kisha E fm kulitokana na mambo haya nitakayoyaorodhesha hapa:
ANGALIZO.
- Kicheko ni " Mkorofi " naturally. Wale wenzangu ambao tokea huko nyuma huwa hatubanduki katika Vijiwe vyetu pale Mwananyamala Kona hadi kwa Kopa nadhani Kicheko siyo mgeni kwetu na isingekuwa " Masela " kuwa wanamtetea kila mara pindi akikamatwa basi leo hii angekuwa Segerea au Keko.
- Kicheko amezidisha sana Usela nnya. Tunajua kuwa Watoto wote wa Kitaa cha Mwananyamala ni Masela ila USELA wa Kicheko ni very extraodinary kitu ambacho kilimfanya karibia atengwe na Marafiki hapo alipokulia na aishipo Mwananyamala.
- Kicheko sasa apunguze au aachane kabisa na matumizi ya Vilevi hasa hasa Bangi na " Powder " ambayo alikuwa akiitumia ila tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu sasa ameacha lakini katika matumizi ya Cannabis Sativa Kicheko bado hajaacha na hii kitu ndiyo imekuwa ikimuharibu mno mdogo wangu huyu.
- Kicheko aache sasa Utemi wake wa Kitoto. Japo mnamwona hivyo alivyo " kimbau mbau " ila Kicheko ni Mtemi sana na uzuri wake ni kwamba ni mpenda Ungomvi halafu anajua pia kuutendea haki Ugomvi wowote anaouanzisha na mara nyingi huu Utemi wake umekuwa ukiwafukuzisha Marafiki zake wengi tu
- Kicheko aache sana kuwatolea Mabosi zake maneno ya Shombo. Msela wangu huyu huwa anashindwa kabisa kutofautisha kati ya Boss na Kapuku pindi awapo Ofisi yoyote. Kicheko kumpa " makavu " mubashara Boss wake ni kitu cha kawaida sana kwake na ni Mtu asiyejali pia.
Tafadhali sijayasema hayo mambo yote hapo juu labda kumchafua au kumuharibia Kicheko bali nadhani nilichokifanya hapo ni kumsaidia tu ili hapo alipo sasa aweze kuwa bora zaidi na sina wasiwasi wowote kuwa kutokana na Vichwa ninavyoviamini hapo Clouds Media Group nadhani kuanzia sasa tutaanza kumwona Kicheko mpya na wote tutamfurahia.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni japo Kicheko ana mapungufu yake na hana Elimu yoyote ile ya masuala ya Journalism and Broadcasting zaidi tu ya kutangaza kwa kuelekezwa ila Kicheko anawazidi sana Watangazaji ambao ni Wasomi na Weledi kabisa wa Tasnia kwani ni mbunifu, anapenda mno kujituma, hakati tamaa na siyo mvivu.
Nimalizie tu kwa kuwashauri Clouds Media Group kuwa kama wataweza wakati wakiwa nae basi wampeleke Shule ya Habari na Utangazaji kidogo Kicheko ili akapigwe " msasa " na akitoka huko akiwa ameiva na kwa Kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu nina uhakika Uongozi mzima wa Clouds Media Group utamfurahia na watafaidika nae sana na hata yeye pia " atatoboa " zaidi.
Nitaomba pia radhi kwa wale ambao labda watajisikia vibaya au kukasirika kwa hayo madhaifu ya Kicheko niliyoyaorodhesha hapo juu ila naamini kwa namna moja au nyingine nitakuwa nimemsaidia ukizingatia kwamba hata Mimi mwenyewe nina " madhaifu / mapungufu " yangu ambayo mengine nimeweza kuyashinda baada ya kukosolewa na Wadau hivyo napenda sana kukosolewa ili niwe vizuri.
Hongera sana Kicheko na Mwenyezi Mungu azidi kukufungulia baraka na akufikishe katika kilele cha Mafanikio unayoyataka na nikuombe tu sasa usiwe na " majipu " a.k.a maringo kwani nina uhakika hapo Clouds Media Group sasa hivi unaenda kuwa na maisha mazuri kuliko ulikokota ambako ulikuwa ukinyanyasika na kudharaulika hadi kutengwa wakati Wewe umechangia mafanikio ya hiyo Redio. Malipo hapa hapa duniani usijali na piga Kazi sasa hapo.
Wala sijasema unaichukia, nimesema "hata kama watu wanaichukia...!" Imetokea tu kwamba hiyo hoja imeambatana na post yako kv sikuona sababu ya kuandika independent post! Lakini hata wewe kama ni mfuatiliaji mzuri na msema ukweli, unaweza kukiri nilichosema kuhusu watu na Clouds ni kweli!!!Mkuu, kutoa maoni si kwamba naichukia, mimi ni shabiki w clouds toka inaanzishwa na mpaka leo nasikiliza clouds japo siku hizi kuna redio station ambazo ni nzuri pia kama timez, na hio efm ambazo kwa kiasi kikubwa ziliweza kuichallenge clouds na ndiomana kuna kupindi ili shake.
Kumbuka unaweza kuwa competent lkn mazingira pia yakakunyima fulsa ya kuonyesha hiyo competence uliyonayo, mfano mdogo tu ni kwa dina marios baada ya kunyang'anywa kipindi cha leo tena.
Mbinu chafu hizi za clouds...Huu mchezo hauhitaji hasira, mbona povu limekutoka Majizo?