Kicheko wa Efm achukuliwa Clouds

Kicheko wa Efm achukuliwa Clouds

Watoto wa kishua bhana... eti EFM ndio wameanzisha Singeli!! Huku Ushenzini tupo na Singeli miaka na miaka sasa halafu mtu aseme EFM ndo wameianzisha!!! Ni kama mtu aseme Radio One ndio walianzisha Charanga hata kama ishakufa kibudu!!!!
 
Mi sikubaliani na uamuzi aliochukua sababu anaenda kujimaliza.mfano mdogo tu ni kwa freduaa aliyekuwa redio free africa,huyu alikuwa mmoja wa watangazaji maarufu sana tz na alikuwa na kipindi chake peke yake ambacho alikimudu hasa lkn toka alivyohamia clouds,amepotea ,akina masudi kipanya wamemfunika kabisa.
Clouds wanachokifanya ni kumvurugia efm ili asiwepo wa kuwa challenge,mfano mdogo tu,muziki wa singeli ilikuwa ni code ya efm lkn toka wauvamie clouds imekuwa shida.
Ngoja tusubili na hiyo television ya efm sijui itakuwaje,maana naona clouds wanarundika tu watangazaji wengi wakati vipindi vichache, matokeo yake wanaishia kubanana kwenye kipindi kimoja.
Sasa hapo tatizo ni Clouds au Fredua mwenyewe?! Inakuwaje mtu ambae alikuwa nyota kwenye radio ghafla aje kufunikwa na Kipanya ambae ana miaka kibao yupo nje ya game?!

Hata kama Clouds watu wanaichukia lakini jamaa wanatoa sana fursa na ndio maana unakuta vipindi vyao vingi vimejaza watu... provided unaweza ku-deliver, Clouds watakubeba! Sasa ikiwa utaenda kufunikwa na uliowakuta au watakaokukuta that's your problem! Na utafunikwa kwa sababu inawezekana haukuwa competent kihivyo otherwise huwezi kufunikwa!
 
Dina Marios
Sasa Dina alitemwa au alienda maternity leave! Sasa wewe ulitaka wasiweke replacement hadi lini wakati martenity leave si chini ya 90 days na kile kipindi ni lazima kiende hewanu??! Na isitoshe ambae alim-replace alikuwa ni mwana-Clouds sema tu alikuwa hajapata fursa na alipoipata akaitumia kama ambavyo Carnnavaro wa Yanga alivyoitumia fursa ya Victor Costa kuwa majeruhi!!
 
Hapa nimepata sababu kwanini Kicheko ameamua kwenda Clouds!!! Nimeona posts kadhaa zikihoji "kumbe Kicheko ni yule Massawe Mtata!" Yaani watu walikuwa hawamjui... lakini fujo za pungufu ya 2 za Clouds zimewafanya watu wengi zaidi wamfahamu Kicheko... hapo hata kazi yenyewe hajaanza!

In short, tuichukie tu Clouds kwa nguvu zetu zote kama tunavyomchukia Diamond kv Wabongo tuna aleji na vitu au watu wanaofanya vizuri... the same happened to Kanumba!!! Lakini Mtangazaji anayependa fursa lazima aende Clouds kv Clouds wanatoa sana fursa kwa Presenters wao... ni wewe tu ushindwe kuzitumia!!
 
Sasa hapo tatizo ni Clouds au Fredua mwenyewe?! Inakuwaje mtu ambae alikuwa nyota kwenye radio ghafla aje kufunikwa na Kipanya ambae ana miaka kibao yupo nje ya game?!

Hata kama Clouds watu wanaichukia lakini jamaa wanatoa sana fursa na ndio maana unakuta vipindi vyao vingi vimejaza watu... provided unaweza ku-deliver, Clouds watakubeba! Sasa ikiwa utaenda kufunikwa na uliowakuta au watakaokukuta that's your problem! Na utafunikwa kwa sababu inawezekana haukuwa competent kihivyo otherwise huwezi kufunikwa!

Mkuu, kutoa maoni si kwamba naichukia, mimi ni shabiki w clouds toka inaanzishwa na mpaka leo nasikiliza clouds japo siku hizi kuna redio station ambazo ni nzuri pia kama timez, na hio efm ambazo kwa kiasi kikubwa ziliweza kuichallenge clouds na ndiomana kuna kupindi ili shake.
Kumbuka unaweza kuwa competent lkn mazingira pia yakakunyima fulsa ya kuonyesha hiyo competence uliyonayo, mfano mdogo tu ni kwa dina marios baada ya kunyang'anywa kipindi cha leo tena.
 
Ni usajili mzuri ambao Clouds Media Group wameufanya kwa kumchukua Kicheko. Kuanzisha mtindo fulani wa muziki na kuupromoti haina maana kwamba Redio zingine shindani zitashindwa kukupiku na kukiboresha kile ulichokiasisi. Ni kweli E fm wanaweza kuwa waanzilishi wa Singeli ila hata wao pia hawakufanya jitihada za dhati kabisa kuweka kuufikisha mbali huu mtindo mpya wa muziki wa " uswahili " na hapa sitawalaumu sana E fm kwani hata coverage yao tu nchini bado siyo kubwa.

Hivyo basi kutokana na coverage nzuri ya Clouds fm na jinsi wanavyojua kupromoti mambo yao nadhani Kicheko kwenda hapo amefanya la maana mno kwani sasa huu mtindo mpya wa muziki wa " uswazinyo " utasambaa nchi nzima na pengine hata kuweza kuibua vipaji vingi vilivyopo huko Mikoani ambavyo havijapata tu nafasi ya kuwa nurtured.

Nirudi kwa Kicheko. Kweli huyu kijana ni Animateur ( neno la Kifaransa linalomaanisha kuwa ni Mchangamshaji mzuri ) na ambaye anaweza kukufanya muda wote umfuatilie na umsikilize bila kuchoka lakini huku pia ukiburudika.

Hata hivyo SIPENDI niliache hili lipite hivi hivi na lazima niliseme hili ili kumsaidia Kicheko na kama kuna Mtu humu anajuana nae si vibaya pia akamfikishia huu ujumbe murua ambao naamini akiuchukua basi utamjenga sana na huko mbele atafika mbali na kufanya makubwa ambayo yatamtangaza vyema na kumpa mafanikio.

Kote alikokua na hadi akawa anafukuzwa Kazi na Waajiri wake huku akiwa haelewani na wenzie kuanzia East Africa Radio kisha E fm kulitokana na mambo haya nitakayoyaorodhesha hapa:

  1. Kicheko ni " Mkorofi " naturally. Wale wenzangu ambao tokea huko nyuma huwa hatubanduki katika Vijiwe vyetu pale Mwananyamala Kona hadi kwa Kopa nadhani Kicheko siyo mgeni kwetu na isingekuwa " Masela " kuwa wanamtetea kila mara pindi akikamatwa basi leo hii angekuwa Segerea au Keko.
  2. Kicheko amezidisha sana Usela nnya. Tunajua kuwa Watoto wote wa Kitaa cha Mwananyamala ni Masela ila USELA wa Kicheko ni very extraodinary kitu ambacho kilimfanya karibia atengwe na Marafiki hapo alipokulia na aishipo Mwananyamala.
  3. Kicheko sasa apunguze au aachane kabisa na matumizi ya Vilevi hasa hasa Bangi na " Powder " ambayo alikuwa akiitumia ila tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu sasa ameacha lakini katika matumizi ya Cannabis Sativa Kicheko bado hajaacha na hii kitu ndiyo imekuwa ikimuharibu mno mdogo wangu huyu.
  4. Kicheko aache sasa Utemi wake wa Kitoto. Japo mnamwona hivyo alivyo " kimbau mbau " ila Kicheko ni Mtemi sana na uzuri wake ni kwamba ni mpenda Ungomvi halafu anajua pia kuutendea haki Ugomvi wowote anaouanzisha na mara nyingi huu Utemi wake umekuwa ukiwafukuzisha Marafiki zake wengi tu
  5. Kicheko aache sana kuwatolea Mabosi zake maneno ya Shombo. Msela wangu huyu huwa anashindwa kabisa kutofautisha kati ya Boss na Kapuku pindi awapo Ofisi yoyote. Kicheko kumpa " makavu " mubashara Boss wake ni kitu cha kawaida sana kwake na ni Mtu asiyejali pia.
ANGALIZO.

Tafadhali sijayasema hayo mambo yote hapo juu labda kumchafua au kumuharibia Kicheko bali nadhani nilichokifanya hapo ni kumsaidia tu ili hapo alipo sasa aweze kuwa bora zaidi na sina wasiwasi wowote kuwa kutokana na Vichwa ninavyoviamini hapo Clouds Media Group nadhani kuanzia sasa tutaanza kumwona Kicheko mpya na wote tutamfurahia.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni japo Kicheko ana mapungufu yake na hana Elimu yoyote ile ya masuala ya Journalism and Broadcasting zaidi tu ya kutangaza kwa kuelekezwa ila Kicheko anawazidi sana Watangazaji ambao ni Wasomi na Weledi kabisa wa Tasnia kwani ni mbunifu, anapenda mno kujituma, hakati tamaa na siyo mvivu.

Nimalizie tu kwa kuwashauri Clouds Media Group kuwa kama wataweza wakati wakiwa nae basi wampeleke Shule ya Habari na Utangazaji kidogo Kicheko ili akapigwe " msasa " na akitoka huko akiwa ameiva na kwa Kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu nina uhakika Uongozi mzima wa Clouds Media Group utamfurahia na watafaidika nae sana na hata yeye pia " atatoboa " zaidi.

Nitaomba pia radhi kwa wale ambao labda watajisikia vibaya au kukasirika kwa hayo madhaifu ya Kicheko niliyoyaorodhesha hapo juu ila naamini kwa namna moja au nyingine nitakuwa nimemsaidia ukizingatia kwamba hata Mimi mwenyewe nina " madhaifu / mapungufu " yangu ambayo mengine nimeweza kuyashinda baada ya kukosolewa na Wadau hivyo napenda sana kukosolewa ili niwe vizuri.

Hongera sana Kicheko na Mwenyezi Mungu azidi kukufungulia baraka na akufikishe katika kilele cha Mafanikio unayoyataka na nikuombe tu sasa usiwe na " majipu " a.k.a maringo kwani nina uhakika hapo Clouds Media Group sasa hivi unaenda kuwa na maisha mazuri kuliko ulikokota ambako ulikuwa ukinyanyasika na kudharaulika hadi kutengwa wakati Wewe umechangia mafanikio ya hiyo Redio. Malipo hapa hapa duniani usijali na piga Kazi sasa hapo.

Mkuu si kweli kwamba efm hawakufanya jitihada kuuendeleza muziki wa singeli.
Kumbuka efm ndio walioutoa muziki huo kutoka mtaani na kuuingiza redioni na hata kuupa vipindi maalum, na hata kufanya matamasha mbalimbali kuutangaza.
 
Mkuu, kutoa maoni si kwamba naichukia, mimi ni shabiki w clouds toka inaanzishwa na mpaka leo nasikiliza clouds japo siku hizi kuna redio station ambazo ni nzuri pia kama timez, na hio efm ambazo kwa kiasi kikubwa ziliweza kuichallenge clouds na ndiomana kuna kupindi ili shake.
Kumbuka unaweza kuwa competent lkn mazingira pia yakakunyima fulsa ya kuonyesha hiyo competence uliyonayo, mfano mdogo tu ni kwa dina marios baada ya kunyang'anywa kipindi cha leo tena.
Wala sijasema unaichukia, nimesema "hata kama watu wanaichukia...!" Imetokea tu kwamba hiyo hoja imeambatana na post yako kv sikuona sababu ya kuandika independent post! Lakini hata wewe kama ni mfuatiliaji mzuri na msema ukweli, unaweza kukiri nilichosema kuhusu watu na Clouds ni kweli!!!

Halafu huyu Dina Marios wewe ni mtu wa pili nakusikia kwamba "alinyang'anywa kipindi cha Leo Tena!! Dina hakunyang'anywa kile kipindi! Dina alikuwa mjamzito kwahiyo alienda maternity leave! Je, ulitaka kipindi kisimame kimsubiri Dina?! Hell No, haiwezekani! Husna akachukua nafasi!! Yule Husna since then nae alikuwa Clouds sema alikuwa hajapata nafasi! Waswahili wanasema kufa kufaana; Husna aliposhika kile kipindi hakufanya kosa!! Sasa je, ulitaka baada ya kurudi likizo ya uzazi Husna angenyang'anywa kipindi wakati alikiendesha kwa ufanisi kwa muda wote?! Hiyo isingekuwa fair! Na ndio maana baada ya Dina kurudi likizo ya uzazi, akapelekwa Clouds TV huku wakiwa na lengo aanzishe kipindi kipya. Clouds Media wanafahamu kwamba Clouds TV iko bado sana kwahiyo walitarajia uwezo na uzoefu wa Dina tangia anaanza na Leo Tena ungesaidia sana kuipaisha Clouds TV endapo atakuwa na kipindi kitakachobamba kama ilivyokuwa Leo Tena!!

.. na kwa kauli yake yeye mwenyewe (Dina) alisema amepewa jukumu kubwa zaidi... kv walimuani anaweza, wakaone
 
Habari ndugu zangu ,

Kwa wale wakazi wa dar na wasikilizaji wa E-FM mtakuwa mnamjua huyu bwana anaitwa kicheko ambaye alikuwa anaendesha kipindi cha singeli nyakati za jioni pale E fm.

Sasa huyu jamaa bna kwa sasa ameshachukuliwa na Clouds FM ,na kusaini mkataba nao.

Sasa kwa sasa muda huu anahojiwa na clouda hawa wakina gea habib hapa na jamaa alivyo mjinga anapiga story zake za zamani jinsi alivyokuwaga mwizi. Hivi kweli haoni kama anajiaibisha na pia anafanya watu tumuone kuwa ni mtu mbaya. Na je hajui kuwa hawa clouds wanamtumia tu??


Ama kweli ujinga ni maradhi makubwa sana. Yaani mtu ametolewa na akina majizo then leo hii anakuja kuwa kama kalogwa
 
Back
Top Bottom