Kicheko wa Efm achukuliwa Clouds

Kicheko wa Efm achukuliwa Clouds

Daah aiseee huyu kicheko majizo alimpokea na kumsaidia hapo alikuwa kashatemwa na comedy eatv
Sam love bado hajakimuudu kipindi cha genge inabidi hatafutwe mtu wa kumpa kampani
Labda chogo sijui nae atakiweza mana kile kipind unatakiwa kidogo hamnazo
 
Ni usajili mzuri ambao Clouds Media Group wameufanya kwa kumchukua Kicheko. Kuanzisha mtindo fulani wa muziki na kuupromoti haina maana kwamba Redio zingine shindani zitashindwa kukupiku na kukiboresha kile ulichokiasisi. Ni kweli E fm wanaweza kuwa waanzilishi wa Singeli ila hata wao pia hawakufanya jitihada za dhati kabisa kuweka kuufikisha mbali huu mtindo mpya wa muziki wa " uswahili " na hapa sitawalaumu sana E fm kwani hata coverage yao tu nchini bado siyo kubwa.

Hivyo basi kutokana na coverage nzuri ya Clouds fm na jinsi wanavyojua kupromoti mambo yao nadhani Kicheko kwenda hapo amefanya la maana mno kwani sasa huu mtindo mpya wa muziki wa " uswazinyo " utasambaa nchi nzima na pengine hata kuweza kuibua vipaji vingi vilivyopo huko Mikoani ambavyo havijapata tu nafasi ya kuwa nurtured.

Nirudi kwa Kicheko. Kweli huyu kijana ni Animateur ( neno la Kifaransa linalomaanisha kuwa ni Mchangamshaji mzuri ) na ambaye anaweza kukufanya muda wote umfuatilie na umsikilize bila kuchoka lakini huku pia ukiburudika.

Hata hivyo SIPENDI niliache hili lipite hivi hivi na lazima niliseme hili ili kumsaidia Kicheko na kama kuna Mtu humu anajuana nae si vibaya pia akamfikishia huu ujumbe murua ambao naamini akiuchukua basi utamjenga sana na huko mbele atafika mbali na kufanya makubwa ambayo yatamtangaza vyema na kumpa mafanikio.

Kote alikokua na hadi akawa anafukuzwa Kazi na Waajiri wake huku akiwa haelewani na wenzie kuanzia East Africa Radio kisha E fm kulitokana na mambo haya nitakayoyaorodhesha hapa:

  1. Kicheko ni " Mkorofi " naturally. Wale wenzangu ambao tokea huko nyuma huwa hatubanduki katika Vijiwe vyetu pale Mwananyamala Kona hadi kwa Kopa nadhani Kicheko siyo mgeni kwetu na isingekuwa " Masela " kuwa wanamtetea kila mara pindi akikamatwa basi leo hii angekuwa Segerea au Keko.
  2. Kicheko amezidisha sana Usela nnya. Tunajua kuwa Watoto wote wa Kitaa cha Mwananyamala ni Masela ila USELA wa Kicheko ni very extraodinary kitu ambacho kilimfanya karibia atengwe na Marafiki hapo alipokulia na aishipo Mwananyamala.
  3. Kicheko sasa apunguze au aachane kabisa na matumizi ya Vilevi hasa hasa Bangi na " Powder " ambayo alikuwa akiitumia ila tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu sasa ameacha lakini katika matumizi ya Cannabis Sativa Kicheko bado hajaacha na hii kitu ndiyo imekuwa ikimuharibu mno mdogo wangu huyu.
  4. Kicheko aache sasa Utemi wake wa Kitoto. Japo mnamwona hivyo alivyo " kimbau mbau " ila Kicheko ni Mtemi sana na uzuri wake ni kwamba ni mpenda Ungomvi halafu anajua pia kuutendea haki Ugomvi wowote anaouanzisha na mara nyingi huu Utemi wake umekuwa ukiwafukuzisha Marafiki zake wengi tu
  5. Kicheko aache sana kuwatolea Mabosi zake maneno ya Shombo. Msela wangu huyu huwa anashindwa kabisa kutofautisha kati ya Boss na Kapuku pindi awapo Ofisi yoyote. Kicheko kumpa " makavu " mubashara Boss wake ni kitu cha kawaida sana kwake na ni Mtu asiyejali pia.
ANGALIZO.

Tafadhali sijayasema hayo mambo yote hapo juu labda kumchafua au kumuharibia Kicheko bali nadhani nilichokifanya hapo ni kumsaidia tu ili hapo alipo sasa aweze kuwa bora zaidi na sina wasiwasi wowote kuwa kutokana na Vichwa ninavyoviamini hapo Clouds Media Group nadhani kuanzia sasa tutaanza kumwona Kicheko mpya na wote tutamfurahia.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni japo Kicheko ana mapungufu yake na hana Elimu yoyote ile ya masuala ya Journalism and Broadcasting zaidi tu ya kutangaza kwa kuelekezwa ila Kicheko anawazidi sana Watangazaji ambao ni Wasomi na Weledi kabisa wa Tasnia kwani ni mbunifu, anapenda mno kujituma, hakati tamaa na siyo mvivu.

Nimalizie tu kwa kuwashauri Clouds Media Group kuwa kama wataweza wakati wakiwa nae basi wampeleke Shule ya Habari na Utangazaji kidogo Kicheko ili akapigwe " msasa " na akitoka huko akiwa ameiva na kwa Kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu nina uhakika Uongozi mzima wa Clouds Media Group utamfurahia na watafaidika nae sana na hata yeye pia " atatoboa " zaidi.

Nitaomba pia radhi kwa wale ambao labda watajisikia vibaya au kukasirika kwa hayo madhaifu ya Kicheko niliyoyaorodhesha hapo juu ila naamini kwa namna moja au nyingine nitakuwa nimemsaidia ukizingatia kwamba hata Mimi mwenyewe nina " madhaifu / mapungufu " yangu ambayo mengine nimeweza kuyashinda baada ya kukosolewa na Wadau hivyo napenda sana kukosolewa ili niwe vizuri.

Hongera sana Kicheko na Mwenyezi Mungu azidi kukufungulia baraka na akufikishe katika kilele cha Mafanikio unayoyataka na nikuombe tu sasa usiwe na " majipu " a.k.a maringo kwani nina uhakika hapo Clouds Media Group sasa hivi unaenda kuwa na maisha mazuri kuliko ulikokota ambako ulikuwa ukinyanyasika na kudharaulika hadi kutengwa wakati Wewe umechangia mafanikio ya hiyo Redio. Malipo hapa hapa duniani usijali na piga Kazi sasa hapo.
 
Duh!umeshusha gaazeti kabisa
 
Mi sikubaliani na uamuzi aliochukua sababu anaenda kujimaliza.mfano mdogo tu ni kwa freduaa aliyekuwa redio free africa,huyu alikuwa mmoja wa watangazaji maarufu sana tz na alikuwa na kipindi chake peke yake ambacho alikimudu hasa lkn toka alivyohamia clouds,amepotea ,akina masudi kipanya wamemfunika kabisa.
Clouds wanachokifanya ni kumvurugia efm ili asiwepo wa kuwa challenge,mfano mdogo tu,muziki wa singeli ilikuwa ni code ya efm lkn toka wauvamie clouds imekuwa shida.
Ngoja tusubili na hiyo television ya efm sijui itakuwaje,maana naona clouds wanarundika tu watangazaji wengi wakati vipindi vichache, matokeo yake wanaishia kubanana kwenye kipindi kimoja.
 
Nimependa mkuu inaonekana unamjua vzr kumbe ata powder alikua anapiga kama kaacha vzr sana nilikua najuaga ni mtu wa mkoani kumbe mzaliwa wa dar shukrani mkuu mengi nilikua siyajui
 
Mi sikubaliani na uamuzi aliochukua sababu anaenda kujimaliza.mfano mdogo tu ni kwa freduaa aliyekuwa redio free africa,huyu alikuwa mmoja wa watangazaji maarufu sana tz na alikuwa na kipindi chake peke yake ambacho alikimuda hasa lkn toka alivyohamia clouds,amepotea ,akina masudi kipanya wamemfunika kabisa.
Clouds wanachokifanya ni kumvurugia efm ili asiwepo wa kuwa challenge,mfano mdogo tu,muziki wa singeli ilikuwa ni code ya efm lkn toka wauvamie clouds imekuwa shida.
Ngoja tusubili na hiyo television ya efm sijui itakuwaje,maana naona clouds wanarundika tu watangazaji wengi wakati vipindi vichache, matokeo yake wanaishia kubanana kwenye kipindi kimoja.
Efm wanataka kufungua na tv mkuu?
 
Back
Top Bottom