Sasa ndugu zangu, issue ambayo imeibuliwa hata na Shivji na wengine inawezekana iko sahihi kwa kuangalia sheria - kwamba kuna ukiukwaji wa Katiba. Lakini sisi sote kuamua hivyo au kuona hivyo hakufanyi kuwe hivyo. Ni maoni yetu tu kwa kadiri tunavyoelewa. La maana na kubwa ni kuwa Assad kama anaamini Magufuli hakuwa na madaraka au hakufuata mchakato wa kumuondoa madarakani kesho anatakiwa arudi kazini na kusema kuwa hajaondolewa kwa utaratibu uliowekwa kikatiba. Anaenda Mahakamani na kupinga kuondolewa kwake madarakani. Mahakama inaweza kuweka injunction CAG mteuliwa asiende kazini hadi hoja ya msingi ya Kikatiba iamuliwe. Nje ya hapo, kuna vipengele vingine vya Katiba ambavyo vinaweza kuonekana kumpa Rais madaraka ya kufanya alivyofanya