Kichwa kinauma sana nimeshindwa kwa maana nimefail

Swensa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2,880
Reaction score
4,295
Habari za wakati huu ndugu zangu wa JF heri ya Pasaka kwenu , Natumaini mnamalizia pasaka vema, kwa wenye changamoto poleni sana,

Ndugu zangu wakati mkiwa mnasherekea na kumalizia sikukuu kesho pia ni kazini na vibaruani pia kwa Watoto wanaenda shule,

Nimeanzisha Uzi muda umekosa wachangiaji unasema Ushirikiano na Moyo Nina Hali ngumu kwa Sasa na mtoto anataka kwenda shule ila Nina deni nadaiwa shuleni linaniumiza kichwa sana kila siku ni ahadi walimu najua wameshanichoka

Naona nimefail kumpa mtoto elimu nimekata tamaa😢😭 nisaidie wadau🙏naona uchungu sana, kazi ni za kubangaiza lakini mtoto asomee
 
Kayumba si ni bure ada ni kidumu cha maji na ufagio au umeamua ushindane na majirani kupeleka watoto shule na bus za njano wakati uwezo mdogo
 
Habari za wakati huu ndugu zangu wa JF heri ya Pasaka kwenu , Natumaini mnamalizia pasaka vema, kwa wenye changamoto poleni sana,

Ndugu zangu wakati mkiwa mnasherekea na kumalizia sikukuu kesho pia ni kazini na vibaruani pia kwa Watoto wanaenda shule,

Nimeanzisha Uzi muda umekosa wachangiaji unasema Ushirikiano na Moyo Nina Hali ngumu kwa Sasa na mtoto anataka kwenda shule ila Nina deni nadaiwa shuleni linaniumiza kichwa sana kila siku ni ahadi walimu najua wameshanichoka

Naona nimefail kumpa mtoto elimu nimekata tamaa😢😭 nisaidie wadau🙏naona uchungu sana, kazi ni za kubangaiza lakini mtoto asomee
Hauko peke yako
 
Ishi kwa kipato chako , mpeleke kayumba huko! Ona sasa unadhalilika, unadhan utaaminika kizembe upewe hela ? Fanya kaz, ishi kulingana na pato lako
 
Pole na changamoto Mkuu. Kwanini unajipa stress kwa kitu unaweza kukitatua? Najua unatamani mtoto apate Elimu bora, ajue kuongea na kuandika Kiingereza. Lakini jikune pale unapopafikia.

Kwasasa kama mambo hayajakaa sawa, mpeleke shule ya Serikali. Ukishakaa sawa, utamtafutia huko tena. Hudhaliliki pekee shuleni, unamdhalilisha na mtoto pia. Fanya maamuzi magumu, Mwenyezi Mungu akutangulie.
 
LIKUD anaimba wimbo ule ule kila siku hammwelewi mpaka kenge atokwe damu ndio anasikia!
 
Niko tayari kukopeshwa ndugu zangu ata kuweka kitamburisho cha nida reani nipate ni sh elfu 50000 tu ntakuwa nalipa pole pole nipo tayari kwa lolote
 
Sawa upo tayari kukopeshwa issue wakopeshaji, je nao wapo tayari kukukopesha?
 
Niko tayari kukopeshwa ndugu zangu ata kuweka kitamburisho cha nida reani nipate ni sh elfu 50000 tu ntakuwa nalipa pole pole nipo tayari kwa lolote
Naona kama hauelewi somo..
Na hii ndio shida ya huku mtaani asilimia kubwa watu hawataki kuishi ndani ya uwezo wao..wanakopi maisha ya wengine au wanataka kuishi nje ya uwezo wao, ukiona jirani ana gari na wewe unataka ukope ununue gari, maisha sio kushindana na mtu, ona Sasa unapata shida na unampa mtoto shida ya Bure tu na kumdhalilisha huko shuleni
 
Back
Top Bottom