Bondia Hassan Mwakinyo ambae amekua gumzo nchini na nje ya nchi kwa ushindi wa kijecha jecha kazua tena tafrani baada ya kumtusi na kumtole maneno machafu legendary wa masumbwi nchini Rashid Matumla.
Matumla alikosoa mbinu za kocha wa Mwakinyo kama watu wengine wa kawaida na mwanamichezo wa kawaida, lakini kitendo hicho kimemkasirisha Mwakinyo na kuanza kufoka na kutupa matusi mazito mazito kwa Matumla kua yeye hajui lolote kuhusu ndondi ndio maana hajafika popote na hata watoto wake hawajafika popote kindondi. Mwakinyo kaenda mbali zaidi na kusema lazima Matumla akamuangukie kocha wake amuombe msamaha mara moja la sivyo bifu itakua kubwa na hakuna wakuizima. Mwakinyo amemkejeli Matumla kua alikua anapigwa kama mtoto na kupoteza mapambano mfululizo.
Hakika pata pesa na umaarufu tujue tabia zako, kijana huyu naona kawasahau watanzania kwanza katuita wapumbavu.
Ni muda sasa wakutupa kwenye dustbin huyu dogo asiekua na heshima kwa waliomtangulia, kama alikua hataki kukosolewa angeenda kupigania chumbani kwake