Kidato cha nne kuanza mitihani kesho, 309,986 hawajulikani walipo

Kidato cha nne kuanza mitihani kesho, 309,986 hawajulikani walipo

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Wanafunzi 595,816 wanatarajia kuanza mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari kuanzia kesho Jumatatu, Novemba 17, 2025, ikiwa ni kukamilisha safari yao ya miaka minne.

Idadi ya watahiniwa wanaotarajiwa kuketi hiyo kesho ni sawa na asilimia 65.63 ya wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.

Hiyo ikiwa na maana kuwa wanafunzi 309,986 hawakuweza kufikia udahili wa kufanya mtihani huo, idadi ambayo huenda ikaongezeka, kwani wengine huenda wasifanye mtihani huo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taita (NECTA), Dk Said Mohammed, leo Jumapili, Novemba 16, 2025, inaeleza idadi ya watahiniwa wa mwaka huu ni ongezeko la asilimia 7.67 ikilinganisha na mwaka 2024.

Watahiniwa hao wanatoka katika jumla ya shule za sekondari 5,868 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 813, kati yao

569,914 ni watahiniwa wa shule na 25,902 ni watahiniwa wa kujitegemea.

Kati ya watahiniwa wa shule 569,914 waliosajiliwa mwaka 2025, wavulana ni 266,028 sawa na asilimia 46.68 na wasichana ni 303,886 sawa na asilimia 53.32.
 
Kuna wengi wao hapo wamesha uawa na wadunguaji kutoka Zanzibar.

😢😢😢😭😭😭
 
Wabongo bwanaa. Yaani hao wasiokuwepo tayari washaunganishwa na tukio kwamba waliuawa kwenye machafuko wakati lengo ni kueleza kwamba licha ya kwamba waliandikishwa wengi mwaka wa 2022, wengi wameishia njiani kwasababu mbalimbali ikiwemo mimba, utoro, nk.
Nimeona pia Nyumbu mmoja kule twita kapost wameuliwa vijana laki tatu!
Hivi hiyo ni akili kweli?
Tupime kwa kuchakata hizi taarifa kumekwa na upotoshaji mkubwa sana.
 
Aman iwe nanyi watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU

Zaid ya watahiniwa laki tatu wa kidato cha nne hawajulikan walipo, wakati mitihan ikianza kesho

Changamoto

Kuna uwezekano zaid ya watu million wamepoteza maisha siku ya uchaguzi

MWENYEZI MUNGU tupiganie

SAYUNI BOY
 
Back
Top Bottom