Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 829
- 1,564
Wadau Eid Mubarak,
Niende kwenye mada nina mtoto wa mdogo wangu ambaye nimekuwa nikimsuport katika elimu yake ya Sekondari. Huyu binti anasoma shule moja SIJUI niite ya serikali au ya kijamii, ni shule zile amabazo zilijengwa mahususi kwa ajili ya jamii za kifugaji ili kuisaidia ukuaji wa elimu kwenye maeneo husika.
Binti huyu mwanzo alifaulu kwenda shule ya kata maeneo ya kijijini kwetu kutokana na mazingira nikaona nifanye ninavoweza kumtoa maeneo yale na akiwa kidato cha kwanza nilifanikiwa kumuamishia shule ya bweni, ilikuwaje hii si mada ya leo.
Kifupi hii shule ina michango mingi sana nadhani Headmaster anakula kutokana na urefu wa kamba. Sasa shule zilivofungwa kwa ajili ya likizo fupi kidato cha nne hawakufunga. Leo ndo nimetumiwa mahitaji kwa ajili ya kumalizia miezi michache iliyobaki. Mojawapo ya michango iliyonistua ni kama ifuatavyo:-
1. Kitambulisho shilingi 10,000/= (Hiki wakati mtoto anaanza fomu one alilipa na hakijawahi tolewa mpaka leo)
2. Project ambayo haitajwi shilingi 30,000/=
3.Remedial 20,000/=
4. Cheti shilingi 8,000/=
5. Mahafari ya shule 20,000/=
6. Mahafari ya dini 10,000/=
7. Bima ya afya 10,000/= hii bima nikauliza kuna bima ya elfu 10? jibu nikwamba wanaunganishwa watoto watano. Hapo pia sijaelewa.