KIDATO CHA NNE KULIPIA CHETI NI SAHIHI?

vyuoni wanafanya research sasa kama unajua research vile inafanywa kuna pahala hela itatumika.

sasa secondary wao wanafanya project, umeuliza project gani?
Hata mkuu wa shule hajui ni project gani mwanao labda anajua title ya project atakayofanya muulize maama yeye ndo anayechagua title (project wanafanya in groups)

Kuhusu hiyo elfu30 ya project mimi sioni sababu ya mkuu wa shule kukusanya hela wakati hafanyi yeye hiyo project, lakini pia kama elf30 ni kubwa mwambie mwanao afanye project ambayo bajeti yake ni ndogo inawezekana akatumia angalau elfu10 kila mmoja wakafanya project ikakamilika.
 
Gharama lazima ziwepo, wakikuambia lazima waende stationery ambayo ipo mbali na shule ilipo ujue hapo nauli lazima ihusike, kuprint na mengine jiongeze.
Hata kama ni kwenda stationery, page moja coloured unaprint kwa bei gani mahali ulipo? Huwezi kuprint page moja kwa shilingi elfu 8
 
Nmeshasema kwa Imani yangu ambayo ndo imani yake hatuna cheti cha dini kinacholipiwa
 
Usitoe kisha uone watafanya nini mwanak endapo atapewa adhabu nenda polisi kamshitaki uyo mwalimu kwa kosa la kumshambulia mtoto
 
Cheti kinachoongelewa hapo ni Leaving certificate si vibaya ukichangaia gharama kidogo maana siku hizi ada hakuna,hivyo shule haina vyanzo vya mapato kuandaa hizo leaving certificate
Changia tu mkuu si vibaya wala dhambi
 
It doesn't make Sense. Umemtoa kwenye shule za kata wewe mwenyewe. Halafu unakuja hapa kulalamikia michango iliyoko kwenye shule uliyochagua. Si ajabu hiyo nafasi uliipata kwa kutoa rushwa au kupewa upendeleo uliovunja sheria, maana katika taratubu za wizara ya elimu/Tamisemi hakuna uhamisho WA day kwenda bweni mpaka vibali maalumu vitolewe. Kama ulikuwa huwezi kukubaliana na taratubu za hiyo shule si ungemuacha alikopangiwa?
Halafu hiyo hela hapo ni ndogo, lipa. Acha kulalamika.
 
Cheti hakilipiwi.
Shule inapewa toka huko vitokako.

Shule haiprint vyeti vya kitaaluma.

Wazazi wa siku hizi ni legelege na hamfatilii maendeleo ya mtoto, mmeziachia shule acha wajilipe na wao kwa kuwalelea.
 
Kama hiyo shule ni ya serikali mchango wa cheti aio halali na una haki ya kutaarifu mamlaka husika yani wilaya au wizara

Swala la remedial na Project ilitakiwa wazazi mkubaliane kwenye kikao kama hakikufanyika kikao hio ni kinyume cha utaratibu pia unatakiwa kuripo.
 
Sijawahi lipia cheti,,ila nililipa michango mingne ya shule ili nipewe chet
 
Sio mbaya walimu nao wakipata malupulupu bwan😄😄
 
Mbona kama tayari umejijibu unatarajia nikukujibu tena, nimeuliza kulipia cheti ni halal, ndo utaratibu wa sasa? 2020 mwnangu wa pili alimaliza mzumbe kaenda kibaha sikuwahi kusikia kulipia cheti, mwingine kasoma private sikuwahi kusikia cheti, mara project, remedial nk.
Nashukuru umetambua huamisho unaweza kupatokana kwa Kibali maalum ama kinyume chake, si mada ya leo
 
Kama ni cheti ndio ni sahihi, si kinatengenezwa stationary? Huko wanatengeneza bure???

Hizo gharama nyingine nenda shule ukapate ufafanuzi
Cheti cha kuhitimu form four wameanza kulipia lini? Mbona kama sikuwahi kuona
 
Kuna michango bana huwa inatia hasira ni basi tu Watu wana mamlaka yao. Umenikumbusha enzi zile tulikuwa tunalipia ID halafu hazijawahi kuonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…