Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).
Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.
Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.
Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.
Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.
Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu.
Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.
Makala hii ni kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya 1, Uk 10.
0715865544/0755865544