Kidini Israel na Trump wapo sahihi, kisheria Wapalestina wapo sahihi

Sheria ipi hiyo inayowapa uhalali wa Palestina kung'ang'ania nchi ya watu?

Dini kwako ni nini?

Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).

Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.

Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.

Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.

Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu.

Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.

Makala hii ni kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya 1, Uk 10.

0715865544/0755865544

View attachment 649590
 
Wanasema israel ni kitovu cha dini tatu uyahudi, ukristo na uislam, kwani uislam ulianzia israel?
Kuna vitu pia sivielewi vizuri sana kuhusu hizi Dini. Kwa mfano marufuku ya trump ilivyotoka ya kuzuia baadhi ya mataifa ya kiislam. Mataifa mengi ya kiislam yalipinga sana. Ss unajiuliza kwn pale maka kuna u lazima gani kwenda ktk nchi ya unayemuita kafiri? Tena unasema anakugombanisha kwa makusudi ili akuuzie silaha ...si kheri usiende na ww mpge marufuku asije kwako
 
Tatizo huu mgogoro wanatajwa waislam na wayahudi tu ila wakristo hawatajwi sijui ni kimkakati au bahati mbaya, nataka kujua wakristu walioa maeneo hayo ya Jerusalem wapo upande upi, wa Israeli au Palestinia?
wao wapo kiroho zaidi ,sisi tunaamini katika yerusalem ya kiroho usijerudia kututaja kwenye mambo yenu ya ukambo
 
Wanasema israel ni kitovu cha dini tatu uyahudi, ukristo na uislam, kwani uislam ulianzia israel?
Uislam ulianzia Saud Arabia na akina Mohamad
Mohamad anazaliwa, anatambaa, ana anza kuongea na kutembea Wayahudi na Wakristo wana muangalia
 
Achen kuzaa wtt nje ya ndoa Ishmael Alitangulia Kaanan lkn ulikuwa nje ya Agano Hvyo nchi si yake Yakobo mbalikiwa ndiye mmiliki halali hao wengine watafute pa kwenda angalizo usinchukie Mimi muulize MUNGU aliye juu
 
Wafilisti siyo uzao wa Ismail. Msisome maandiko kwa kupapasa kwa nje.
 
Solomon and the Queen of Sheba

The hoopoe dropped the letter in front of the queen and flew away to hide. She excitedly opened and read it: "Verily! It is from Solomon, and verily! It reads: 'In the Name of Allah, the Most Beneficent, and Most Merciful; be you not exalted against me, but come to me as Muslims (true believers who submit with full submission).'" ( Ch 27:30-31 Quran).

And Solomon said: "Knowledge was bestowed on us before her, and we were submitted to Allah (in Islam as Muslims before her)."

She said: "My Lord! Verily, I have wronged myself, and I submit (in Islam), together with Solomon, to Allah, the Lord of the Alamin (mankind, jinns, and all that exists)." (Ch 27:20-44 Quran)
Aya za uwongo kabisa. Mtu aje karne ya 6, ashushiwe qur an, halafu eti Sulemani alikuwa Muslim. Kwani Sulemani si Myahudi? huko kwenu kwa wenye dini yao Waarabu hamna manabii. Kwa mnang'ania manabii wa Mayahudi wakati huo huo mnawachukia wayahudi?
 
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).

Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.

Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.

Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.

Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu.

Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.

Makala hii ni kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya 1, Uk 10.

0715865544/0755865544

View attachment 649590
Sijakuelewa mkuu, inamaana dini siku zote iko kinyume na sheria?
Umenikumbusha hadthi Moja ya Rabin, alikuja mwanamke mmoja kwa Rabin kumshitaki mume wake jinsi anavyo mtesa, mwanamke akasimulia baada ya kumaliza Rabin akamwambia mwanamke uko sahihi kabisa.
Baada ya kuondoka mwanamke tu na Manamme na akaja kumshitaki mkewe kuwa yeye ndie mkosa, Baada ya Kumaliza kuelezea Rabin akamwambia mwanamme na wewe uko Sahihi. Kumbe wakati anazungumza nao wale watu kuna msaidizi wake mmoja alikuwa kajificha anasikiliza, Baada ya kuondoka akaja kumlaumu Rabin kwa nini watu wawili Kila mmoja anamwambia mwenzake ndio mkosa na wewe Unawambia wote wawili kuwa wako sahihi.
Rabin akamjibu msaidizi wake na wewe uko sahihi
Haiwezekani Pande mbili kwa wakati mmoja zikawa sahihi lakini zikakinzana
 
asilimia 90 ya manabii katika uislam ni wayahudi,baada ya wayahudi kuanza kuua manabii wa Mungu na kukufuru,unabii ukahamishiwa kwa Muarabu.
Hakuna mwarabu nabii wa Mungu. Mohammad ni Anti-Christ aliyetabiriwa miaka 600 kabla ya hajaanzisha dini yake. Mohammad ni mtumishi wa Baali (habal) ambaye nyie mnamwita Allah. Baali ni Shetani ndo maana hata majini na mapepo huko kwenu ni viumbe wazuri.
 
Uislamu umekuja miaka ya 600 AD , sasa wakajipendekeza kwa wayahudi na kudai ibrahimu alikuwa muislamu, kitu ambacho sio kweli, before 600AD hakuna historia,wala mabaki ya chembe ya historia yanayoonesha paliwahi kuwepo din inaitwa uislamu,

Waarabu walikuwa. Wanaabudu jiwe jeusi na kufanya ibada kwa mungu allah,
Ndio tamadun alizokuja kuzichukua muhamad na kuziboresha kisha kusema huu utakuwa UISLAMU

lakin uislamu hauhusiani hata kidogo na MANABII WAYAHUDI ,

HATA QURAN inataja neno ISRAEL lakini haijui nini maana ya israeli, lkn BIBLIA inakuambia mwanzo na chimbuko la neno ISRAEL,

Quran haitaji neno YERUSALEM , Lakin biblia imelitaja mara 5000 ,

Waislamu wanaongopewa kuwa YERUSALEMU NI YAO , wakati hapo Yerusalemu palijengwa HEKALU NA MFALME SULEMAN, hilo hekalu muundo wake , na vitu vilivyokuwepo ndani haviendan na UISLAMU hata kidogo,

Leo pamejengwa msikit wa Al aqsa, miaka ya karibuni, lakin bado kuna waislamu wanadanganywa HUO MSIKITI ALIJENGA SULEMAN
Uislamu upo tangu enzi za Adam we tulia tu, neno Uislamu ni "Amani" AMANI ikitawala kwenye nafsi yako unapata utulivu wa kuabudu, na utambue Israeli ni jina lilopachikwa kwenye ardhi ya wapalestina msukumo wako usikufanye yakutoke yasiyo bayana ukashindwa kuelewa, hata dini yako ni Uislamu na hujui tuu
 
Acha kudanganywa , hujui hata uisamu umeanza lini,

Eti kuwa na aman tu ni uislamu,

Nitakufundisha chanzo cha uislamu

Tatizo umemezeshwa matangopori madrasa
 
Tatizo huu mgogoro wanatajwa waislam na wayahudi tu ila wakristo hawatajwi sijui ni kimkakati au bahati mbaya, nataka kujua wakristu walioa maeneo hayo ya Jerusalem wapo upande upi, wa Israeli au Palestinia?
Israel
 
Your
Uislamu umekuja miaka ya 600 AD , sasa wakajipendekeza kwa wayahudi na kudai ibrahimu alikuwa muislamu, kitu ambacho sio kweli, before 600AD hakuna historia,wala mabaki ya chembe ya historia yanayoonesha paliwahi kuwepo din inaitwa uislamu,

Waarabu walikuwa. Wanaabudu jiwe jeusi na kufanya ibada kwa mungu allah,
Ndio tamadun alizokuja kuzichukua muhamad na kuziboresha kisha kusema huu utakuwa UISLAMU

lakin uislamu hauhusiani hata kidogo na MANABII WAYAHUDI ,

HATA QURAN inataja neno ISRAEL lakini haijui nini maana ya israeli, lkn BIBLIA inakuambia mwanzo na chimbuko la neno ISRAEL,

Quran haitaji neno YERUSALEM , Lakin biblia imelitaja mara 5000 ,

Waislamu wanaongopewa kuwa YERUSALEMU NI YAO , wakati hapo Yerusalemu palijengwa HEKALU NA MFALME SULEMAN, hilo hekalu muundo wake , na vitu vilivyokuwepo ndani haviendan na UISLAMU hata kidogo,

Leo pamejengwa msikit wa Al aqsa, miaka ya karibuni, lakin bado kuna waislamu wanadanganywa HUO MSIKITI ALIJENGA SULEMAN
Your Right
 
Suggestion yangu hawa watu waachwe tu, mmoja achukue ardhi au wakubaliane wachukue wote.
Kwa sababu ni ujinga kutumia dini ku-justify kugombania ardhi.
Kuna sehemu nyingi ina migogoro ya maeneo kwa kila mtu kuwa na hoja zake.
Wengine wanakubaliana na matokeo, wengine hutafuta suluhu, na wengine huendelea kupigana mpaka the last ones standing.
Huwezi ukadai walipewa na Mungu tu. Hiyo haitoshi, maana throughout history watu wamekuwa wakipinduana kuchukua ardhi.
Em tutafute a common ground ku-solve hili suala.
Kila mtu ana makazi pale, sasa kwa nini tunaona ni bora mmoja aondoke... Illogical.
 
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).

Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.

Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.

Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.

Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu.

Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.

Makala hii ni kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya 1, Uk 10.

0715865544/0755865544

View attachment 649590

HATA KIDINI WAYAHUDI NA TRUMP WAKO WRONG

ANGALIA HII DOCUMENTARY YA BBC

shida yenu mnaridhika na madrasaat. Mlinalishwa vifa vya uongo weeeee! manridhika. Palestina imaeanza kutamkwa miaka mingi sana baada ya jina Israel kuwepo Duniani. Kingdom of Israel na United Kingdom Of Israel zilikuwepo Duniani miaka zaidi ya 3000 iliyopita. walahakujawahi kuwa ni nchi inaitwa Palestina.
 
Back
Top Bottom