Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
“Mwenye nacho huongezewa, asiye nacho hunyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”
- Mathayo 13:12 (Biblia).
Inaweza kuonekana kama isiyo na haki, lakini ndani yake imefichwa kanuni ya mafanikio, ukuaji wa ndani, na nguvu ya fikra.
- Mathayo 13:12 (Biblia).
Inaweza kuonekana kama isiyo na haki, lakini ndani yake imefichwa kanuni ya mafanikio, ukuaji wa ndani, na nguvu ya fikra.
Kwa nini Mwenye nacho huongezewa?…….
- Ana mtazamo wa kuthamini — hata kile kidogo alichonacho.
- Hutumia fursa anazopata kwa bidii na maarifa.
- Huendelea kujifunza, kukua, na kujiendeleza.
- Huwa na mtindo wa maisha wa kutoa thamani, si kulaumu au kulalamika.
- Anapopata kidogo, hukikuza. Kwa hiyo anavutia zaidi, anapewa zaidi!
Kwa nini asiye nacho hunyang’anywa hata kile kidogo alichonacho?………
- Hathamini kile alichonacho.
- Huishi kwa malalamiko badala ya shukrani.
- Ana hofu ya kujaribu, haoni fursa ndani ya changamoto.
- Hudharau hatua ndogo – anasubiri ajira kubwa, mtaji mkubwa, nafasi kubwa... akasahau: kubwa huanzia kwa dogo.
- Muda, akili, hata uhusiano mzuri – huupoteza kwa uzembe wa kiakili.
FIKIRIA HAYA,
- Una dakika 15 kila siku, je, unazitumia kujenga ndoto zako au kuporomosha ndoto za wengine?
- Una marafiki wachache wa kweli ,je, unawajenga au unawatumia?
- Una kipaji cha kuandika, kuimba, kuuza, kupika... unakitumia kweli au unakipuuzia?