Ameshaitwa asiye nacho, hicho kidogo ni kidogo alichonacho ni kinini?.... Asante kwa ujumbe mzuri mkuuasiye nacho hunyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”
Noted“Mwenye nacho huongezewa, asiye nacho hunyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”
- Mathayo 13:12 (Biblia).
Inaweza kuonekana kama isiyo na haki, lakini ndani yake imefichwa kanuni ya mafanikio, ukuaji wa ndani, na nguvu ya fikra.
Kwa nini Mwenye nacho huongezewa?…….
- Ana mtazamo wa kuthamini — hata kile kidogo alichonacho.
- Hutumia fursa anazopata kwa bidii na maarifa.
- Huendelea kujifunza, kukua, na kujiendeleza.
- Huwa na mtindo wa maisha wa kutoa thamani, si kulaumu au kulalamika.
- Anapopata kidogo, hukikuza. Kwa hiyo anavutia zaidi, anapewa zaidi!
Kwa nini asiye nacho hunyang’anywa hata kile kidogo alichonacho?………
- Hathamini kile alichonacho.
- Huishi kwa malalamiko badala ya shukrani.
- Ana hofu ya kujaribu, haoni fursa ndani ya changamoto.
- Hudharau hatua ndogo – anasubiri ajira kubwa, mtaji mkubwa, nafasi kubwa... akasahau: kubwa huanzia kwa dogo.
- Muda, akili, hata uhusiano mzuri – huupoteza kwa uzembe wa kiakili.
FIKIRIA HAYA,
Kumbuka;Usipotumia kile ulichonacho, dunia haitakisubiri , itakinyakua na kumpa mwingine anayekithamini.
- Una dakika 15 kila siku, je, unazitumia kujenga ndoto zako au kuporomosha ndoto za wengine?
- Una marafiki wachache wa kweli ,je, unawajenga au unawatumia?
- Una kipaji cha kuandika, kuimba, kuuza, kupika... unakitumia kweli au unakipuuzia?
Kwa iyo madem wanatumia ipasavyo.“Mwenye nacho huongezewa, asiye nacho hunyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”