Kifalsafa "kimantiki" Yesu hakutolewa Kafara. Dunia imedanganywa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
KIFALSAFA "KIMANTIKI" YESU HAKUTOLEWA KAFARA. DUNIA IMEDANGANYWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Angalizo: Mada hii inaweza isiwafae watu wote hasa watu wale wenye Itikadi na hisia Kali za kidini. Hivyo kama Taikon Master kwa kulijua Hilo, nashauri wewe kama ni wale wenye Itikadi Kali au Imani Kali Basi unaweza kupuuzia Mada hii na kuidharau ukaishia tuu hapahapa. Kuendelea kusoma itahesabika kutumia Uhuru wako kuchagua Jambo litakaloweza kukuumiza . Hivyo maumivu hayo Mimi sitahusishwa.

Tuendelee.
Tangu tukiwa watoto Wakristo tumekuwa tukifundishwa kuwa Yesu Kristo alikufa kwaajili yetu, alitolewa Kafara ili binadamu Wapate uzima na sio uzima tuu Bali uzima wa MILELE.

Yohana anatuambia hivi:
Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Aya nyingi ndani ya Biblia hasa katika vitabu vya Injili vinaeleza kuwa Yesu Kristo alikuwa ni Kafara kwaajili ya ondoleo la dhambi za wanadamu.

Waandishi wa Biblia wamejitahidi Sana kumpa Uhusika wa ajabu Yesu na kubwa zaidi ni Hilo la Kujitoa Kafara, Kufa kwaajili ya wanadamu.
Na mwisho Kabisa Kufufuka katika Wafu.

Mimi sina tatizo na Yesu Kujitoa Au kutolewa Kafara kwa Sababu wapo watu wengi waliojitoa Kafara na hata hivi Leo wapo watu wanaojitoa Kafara kwaajili ya Familia Zao na mataifa Yao.

Akili yangu inaanza Kupata shida pale ambapo Mtolewa Kafara amefufuka.

Tukio la Kufufuka kwa Yesu kama ilivyoripotiwa katika vitabu vya Injili ndilo linaloondoa dhana zima ya KAFARA ya Yesu Kristo.

Ili kitu au Jambo lisemwe limetolewa Kafara lazima lipotee na lisipatikane Tena na hakuna namna nyingine ya kulirejesha tena Jambo hilo.

Kafara ni kutoa na kupoteza Jambo la thamani Sana ili mtu apate Jambo jingine la muhimu au la thamani zaidi.
Mfano mtu anaweza kutoa Kafara Muda wake ili apate Jambo Fulani.
Kafara iliyotolewa haiwezi kurudi.

Kafara za uhai.
Unakuta mtu anatoa uhai wake kwaajili ya Familia au taifa lake. Uhai uliotolewa hauwezi kurudishwa tena. Hiyo inaitwa Kafara.

Kafara inayoweza kurudishwa haiitwi KAFARA inaweza kupewa jina jingine.

Kuna visa vya watu waliowatoa Kafara wazazi au watoto wao ili wajipatie Utajiri au vyeo. Hizo ni Kafara na zile Kafara haziwezi kurudi kamwe. Unapomtoa mzazi au mtoto Kafara haitarajiwi na haiwezekani mtoto au mzazi huyo kurudi tena. Yaani ndio umempoteza hivyo ili wewe upate utajiri au cheo Fulani. Hiyo ni KAFARA.

Tukirejea kwenye Kafara na dhabihu za wakati wa Musa. Wanyama waliokuwa wakitolewa Kafara au dhabihu ndio ilikuwa ntolee hiyo. Huwezi kumrudisha kondoo au mbuzi aliyejinjwa kwaajili ya Kafara.

Yesu alipokufa na kusulubishwa kwaajili ya wenye dhambi kama ilivyoripotiwa kwenye Injili. Ingekuwa Kafara kama angekufa Moja Kwa Moja bila ya Kufufuka tena.
Hiyo kwa kweli ingestahili kuitwa KAFARA.
Kwa sababu hapo itahesabika ni kweli kama Yesu ni mwana kipenzi cha Mungu kama alivyoripotiwa alitolewa Kafara na habari yake iliishia hapo.
Ingekuwa ni rekodi ya kueleweka kimantiki.

Lakini kusema Yesu alijitoa Kafara kwaajili yetu huku akijua atafufuka au kufufuliwa ni kinyume na MSINGI wa KAFARA. Hiyo haiwezi kuitwa KAFARA.
Huo ni utapeli, ujanjaujanja ambao hata kwenye siasa za wanadamu tunaziona kila siku.

Kwenye siasa za ulaghai ni Jambo la kawaida kiongozi Fulani kutolewa Kafara na viongozi wenzake au Kujitoa Kafara kwaajili ya viongozi wenzake kwa Nje watu wanamuona alitolewa au kujitoa Kafara lakini kwa ndani kumbe ni drama, igizo ambalo watu wamepanga kumtoa au ajitoe kafara alafu baada ya muda fulani watampa cheo kingine. Au kumhamisha sehemu nyingine ya Kazi.
Au awe hafanyi Kazi lakini yupo kwenye payroll ya serikali. Huo ni utapeli, ujanjaujanja.

Kama Yesu alijua atafufuliwa au atafufuka haikuwa na maana ya Yeye kusema atajitoa uhai au mungu amemtoa mwanaume mpendwa ampendaye kwaajili ya wanadamu wakati huohuo hakumtoa Bali alimfufua na alipaa kukaa Mkono WA kuume wa Babaye.

Hivi kuna Kafara ya namna hiyo kweli?
Kafara ni kupoteza Jambo Fulani lenye thamani mazima. Yaani hutolipata tena. Una umefanya hivyo kwaajili ya Upendo ili upate Jambo zuri au uweka Hali ikae Sawa..

Mtu anakuambia Yesu katolewa Kafara au alikufa kwaajili yake alafu Muda huohuo anakuambia yupo mbinguni. Huo kama sio Mchezo wa kuchezeana akili ni kitu gani?

Yaani mtu upate uchungu wa Mtu aliyejitoa Kafara ambaye alijua atafufuka😂😂 Kweli.

Kwa minajili hiyo ni aidha Yesu alisulubishwa akafa na hakufufuka. Ili iitwe Kafara na ndio hayupo Mbinguni.
Au Yesu hakufa msalabani ila alipalizwa kama baadhi ya maandiko yanavyoripoti ikiwemo Quran.

Kwa sababu kama alifufuka Basi haikuwa Kafara.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Yaani mtu upate uchungu wa Mtu aliyejitoa Kafara ambaye alijua atafufuka[emoji23][emoji23] Kweli.

Kwa minajili hiyo ni aidha Yesu alisulubishwa akafa na hakufufuka. Ili iitwe Kafara na ndio hayupo Mbinguni.
Au Yesu hakufa msalabani ila alipalizwa kama baadhi ya maandiko yanavyoripoti ikiwemo Quran.

Kwa sababu kama alifufuka Basi haikuwa Kafara.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Ukisoma mat 15: 24 Yesu huyu huyu anausikaje na sie Wa kerewe wa Tanzania, kama sio upotoshaji mtupu, stori ya Yesu nzima ni myth haina ukweli wowote.
 
Watibeli tumeelewa ..na kama ulivyotahadharisha mapema waliwao na wasio na utambuzi wataleta ubishi..

Nalichunguza jambo hili kiundani..ila yesu hakufa naipa point zaidi..wafu wazikane yesu hakuwahi kufa yu hai hata sasa..na yeye ndo mwanzo wa uhai wa Mungu (roho na nafsi kinyume ya mwili)

KWa heri
 
We John kwa imani hiyo wewe unavunja misingi ya kikuristo, inaonekana wewe sio mkuristo unajiita tu.
 
Ukisoma mat 15: 24 Yesu huyu huyu anausikaje na sie Wakarewe wa Tanzania, kama sio upotoshaji mtupu, stori ya Yesu nzima ni myth haina ukweli wowote.
Mbona unaishia njiani endelea na hicho kisa uone baadae ilikuwaje....halafu baadae unijibu kabla Mohammad hajasilimu alikuwa dini gani?
 
We John kwa imani hiyo wewe unavunja misingi ya kikuristo, inaonekana wewe sio mkuristo unajiita tu.
Whatever nitakavaoamini lakini kubwa nikatimiza Yale ayatakayo Mungu tufanye na nikaepuka mabaya..si nitakuwa upande wa faida bado
 
unaonekana una chuki mno na ukristo na wakristo kiujumla hadi unaandika mkuristo mara kikuristo
 
Ni lazima uheshimu imani hiyo inao kuunganisha kwa Mungu wako, utafikaje kwa Mungu wakati unapinga misingi ya ukuristo na papa mtakatifu.

Ukristo umejengeka kwenye "trinity" (utatu) na theory ya utatu kuna kufa kufufuka na kupaa tena kulejea kwa huyu huyu alio paa.....usipo heshimu hivo na kuamini wewe sio mkristo tena.
 
Wewe ni idiot chuki iko wapi hapo kama mada iko juu ya uelewa wako ka pembeni, mleta mada sio mimi ni mkristo.
 
Ni lazima uheshimu imani hiyo inao kuunganisha kwa Mungu wako, utafikaje kwa Mungu wakati unapinga misingi ya ukuristo na papa mtakatifu.

Ukristo umejengeka kwenye "trinity" (utatu) na theory ya utatu kuna kufa kufufuka na kupaa tena kulejea kwa huyu huyu alio paa.....usipo heshimu hivo na kuamini wewe sio mkristo tena.
Ona hapa ulivyo mpumbavu zaidi inaonyesha hata maana ya mkristo hauijui sasa huyo papa si nikwa wakatoliki tu mbwa wewe?
 
Back
Top Bottom