Unapaswa kuelewa vizuri alichofanya Yesu Kristo, na kwanini alifanya hivyo na kwasababu gani kafara au vizuri zaidi SADAKA ya Yesu inasemwa kuwa ilitolewa mara moja tu tofauti na kafara/sadaka nyingine.Kafara ni kupoteza Jambo Fulani lenye thamani mazima. Yaani hutolipata tena. Una umefanya hivyo kwaajili ya Upendo ili upate Jambo zuri au uweka Hali ikae Sawa..
Yesu alikufa msalabani ili kuukomboa ulimwengu. Kufa kwa ajili ya kusudio flani na sio kufa kwa uzee au ugonjwa. Manake ni kwamba aliweza kutoa kitu kikubwa zaidi ya kitu kingine, yaani uhai wake mwenyewe. Kwa vile Yesu ni Mwana wa Mungu na asiye na doa lolote, basi sadaka yake ilikuwa ya upeo wa juu kabisa na hakuna mwanadamu anaweza kufikia hata akijitolea kufa kwa ajili ya watu.
Nini kilitokea baada ya Yesu kufa msalabani. Alikwenda kuzimu (himaya ya giza na makao ya shetani). Kutokana na nguvu ya kafara alilolitoa kwa damu yake na uhai wake mwenyewe, aliweza kumnyang'anya shetani zile kamba au funguo alizokuwa anazitumia kuwatesa na kuwaangamiza wanadamu.
Kazi imekwisha au anavyosema mwenyewe; Yametimia au yamekwisha. Alipomaliza kazi hiyo kubwa na akiwa sasa na ameshanunua na kulipia haki zetu kwa damu yake, aliweza sasa kwa uwezo wa Kimungu kurudi na kuonekana katika ulimwengu wa kawaida, lakini sasa akiwa na mwili wa utukufu au hali ya kiroho. Ila kama ni kafara aliitoa na maisha yake hayakuwa tena yale yale ya kale, bali alibadilika kabisa na kwenda kwenye maisha mapya, hata baada ya kufufuka hakuishi tena maisha ya kawaida, ya kale yalikwisha kabisa sio tu kwake bali hata kwa wale aliowatolea maisha yake.