Kifalsafa "kimantiki" Yesu hakutolewa Kafara. Dunia imedanganywa

Mkuu usiingize Imani za dini nyingine kwenye mada zetu tunajadili na theory ya kufufuka kwa yesu, acha kua mdini kuingiza wengine katika hili, leta hoja sio hasira mkuu.
Ni kwamba umeleta dharau mno au unajisahaulisha?
 
Ona hapa ulivyo mpumbavu zaidi inaonyesha hata maana ya mkristo hauijui sasa huyo papa si nikwa wakatoliki tu mbwa wewe?
Mkuu mbona unatukana tu umejaa hasira tupu, Papa ni kiongozi wa wakristo wa katoliki ambao ndo majority dunian kumbeza na kumkebehi ni utovu wa maadili.
 
1 Wakorintho 15:55-57 – Ewe mauti, u wapi ushindi wako? Ewe mauti, u wapi uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Lile tukio la Yesu lilibeba mambo mawili kwa wakati mmoja kwa maana ya kifo chake kilikuwa dhabihu ya upatanisho, na ufufuo wake ulikuwa uthibitisho wa ushindi wake dhidi ya mauti na dhambi.

Kitendo tu cha kumwaga damu tayari ni dhabihu hiyo ila kifo ni unyang'anyi wa yale yote ambayo yalikua yanamilikiwa na kile kilichotolewa kafara vibaki kwa mwenye kuifanya hiyo kafara (umiliki kamili).

Na ukiangalia Yesu alifanya hivyo kwa maana ya kufa pia alikufa kwahiyo hii tayari inamaanisha ule umiliki kamili ulipatikana kwa maana hata kafara ambazo umezizungumzia wewe hapo juu ni mauaji ya lazima na si ya kihatima kwahiyo Kila kafara iliyowahi kutolewa huwa inakufa tena baada ya ule muda wa hatima ya kifo chake kufikia na wakati huu unapofikia ile kafara iliyofanyika huwa inapoteza nguvu kwa maana ile mitetemo ya aliyetolewa kafara inakua tayari imeshafutwa kwenye ulimwengu(hapa ili uelewe vizuri chukulia mfano wa unapofuta file kwenye laptop yako, linaelekea kwenye recycle bin, ni kwamba halionekani pale ambapo lilikuwepo lakini lipo na kama recycle bin ingekua inahifadhi hizo files kwa muda fulani na baadae ile automatic deletion inatokea permanently basi ingekua ni sawa na asili ya kafara).

Kwahiyo Yesu angekufa tu bila kufufuka basi upatanisho pekee ndio ungekua umetimilizwa ila ule ushindi kamili dhidi ya dhambi na mauti ungekosekana, lakini pia hata kafara yake isingekua ya milele kwa maana kuna nyakati ile mitetemo yake ingefutwa kwenye uso wa Dunia ila kile kitendo cha ufufuo kinamaanisha ile mitetemo yake ipo na itaendelea kuwepo siku zote na hii ndio maana halisi ya ondoleo la dhambi na uzima wa milele.

All in all kifo na ufufuo wa Yesu ni moja ya mafumbo makuu yaliyomo ndani ya biblia, na hata kuzaliwa kwake pia ni fimbo lakini pia ni majibu ya maswali mengi ya agano la kale hasa kile kitabu cha Mwanzo.

Ndio maana Mimi huwa nawaambia watu ya kwamba biblia yote imeishia mwanzo moja hadi sita.

NB: kitendo cha kutumika kwaajiri ya hatima ya mtu au watu wengine kwa namna ya kafara au namna nyingine yoyote yenye kutia upofu upande wako wa kiroho kiasi cha kukufanya ushindwe kutimiza hatima yako ya kiMungu iliyofanya uwe hapa duniani huo tayari ni udhaifu na wala hakuna uhuisho kwa watu wadhaifu, na njia ya kuifanya mitetemo ya mtu fulani iendelee kubaki duniani ni uhuisho, kwahiyo Yesu alijiondoa kwenye huu mtego ili akupe wokovu kamili na wamilele.
 
Baba nakuomba ujadili habari zingine.. Haya mambo ya Kiroho naona yamekuzidi kimo.. Utajiaibisha..
 
Bajeti ya huu utafiti ilikuwa ni kiasi gani cha pesa?
 
Kumbe we ni mfia dini. Unapangia watu la kujadili badala la kumuelewesha huna hoja?
Humuwezi huyo Yesu wewe.. Walimshindwa waliomuona utanuweza wewe uliyesikia tu habari zake..?? Yesu ni zaidi ya unavyodhani.. Yesu ni uzima wa milele..
 
Yaani jamani watu wana chuki na Dini fulani mpaka watakufa kweli kweli loh!!
Chuki wanayo waislamu angalia mfano mdogo tu ulivyoita wewe...njoo huku mtwara,lindi jambo la kwanza ukiwa mgeni kabla ya yote utaulizwa wewe dini gani
 
"Kwa sababu kama alifufuka Basi haikuwa Kafara"

Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana, na hujawahi elewa Biblia na concepts zake!

Unafikiri kwa nini Yesu alikuwa Duniani na kusulubishwa kama ilivyoandikwa kwenye Biblia?

Je kitu ulichokitoa Kafara unaweza kukipata tena na ikawa Kafara?
 
Kafara ni nini?
Yesu alikuwa Kafara au hakuwa?
Je ukikitoa kitu Kafara unaweza kukipata tena?
kujitoa kafara ni kubeba mzigo wa wengi, ili wao wawe salama, wanaume wamejitoa kafara hata kuingia sehemu hatarishi ili familia zao ziwe salama, Askari wamejitoa kafara kulinda mipakani ili taifa libaki salama
 
Sijui levo yako ya uelewa kuhusu biblia,Mungu n yesu,sijui pia uelewa wako kuhusu utatu mtakatifu(father,son and holy spirit)na kuhusu huyo yesu pia,sijui uelewa wako kuhusu umungu mwana wake,sijui kama huwa wailewa Ile yohana 1-...,Kwa kifupi nahisi huelewi mengi kuhusu hiyo dhana uloiandika hapo,hakuna maandiko yoyote yanayosema Ili kitu kiwe kafara lazima kipotee kabisa kama vile hakuna maandiko yoyote yanayosema kitu chochote anachokalia mtu ni kiti,hizo zote ni perceptions(opinion) tulizokaa nazo muda mrefu na sio fact,kifupi ukisoma yohana 1---,utagundua yesu ni Mungu,yesu ni mwana wa Mungu,yesu ni roho(neno) na yesu pia ni mwanadamu,hivyo basi Mungu na neno haviwezi kufa,ila huo ubinadamu ndo ulikufa,maana maandiko yanasema kupitia adamu dhambi iliingia hivyo ilihitajika mwili wa nyama(mwana Adam) kutoa hiyo dhambi, kasome yohana 1---uongeze kufikiria Kwa kutumia ubongo na sio kamasi.
 

Hayo uliyoeleza yapo Sawa.

Tuseme Yesu ni Mungu kwa MUKTADHA WA Biblia.
Je Mungu hakumtoa Yesu Kafara? Yaani hakumpoteza Yesu kwaajili ya wanadamu?

Unajua maana ya Kafara lakini?
Au ukisikia mtu katolewa Kafara au katoa Kafara kitu au Jambo Fulani nini kinakuja kwenye Akili yako?

Kama Mungu hawezi kufa, kwa nini imeandikwa Yesu alikufa kwaajili yetu? Unamanisha hakufa?
Kwamba alidanganya?

Ikiwa Kufa kwaajili yetu ilikuwa ndio Kafara. Umuhimu wa Kafara hiyo unatoka wapi ikiwa Yesu yu hai(Yule aliyetolewa Kafara)

Ibrahim alitaka Kumtoa Isaka Kafara. Yaani kumpoteza Isaka kwaajili ya Kumpenda Mungu.
Lakini hakumtoa Kafara Isaka. Kwa sababu hakumpoteza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…