Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Wewe umemuona baba mzazi tu, kuna hadi paroko wa kanisa katoliki
 
Unachekesha na kufurahi sana ,thibitisha unayo yasema.
Mkuu amini nakuambua , kiini cha kila tatizo huwa kiko katika hali ya mtu kuchukua nafasi ya mtu mwingine au mtu mwingine nafasi yake kuchukuliwa na mwingine.

Mfano labda Mungu alimpangia mtu awe na nafasi ya kuwa mhudumu wa ndege halafu huyu mtu akalazimisha kuchukua nafasi ya urais . Hii nafasi ya urais siyo yake kiasili , ataikalia lakini atasababisha matatizo maana hatoshi kuendana na mpango wa Mungu kwake . Mtu huyu anaweza kuwa na utu akiwa kwenye nafasi ya mhudumu wa ndege lakini hawezi kuwa na utu akiwa kwenye nafasi ya urais.

Mfano Mungu alimpangia mtu awe na nafasi ya kuwa mwalimu halafu mtu huyu akalazimisha kuwa spika wa bunge labda . Hii nafasi ya spika wa bunge sio yake kiasili , ataikalia lakini atasababisha matatizo maana hatoshi kuendana na mpango wa Mungu kwake. Mtu huyu anaweza kuwa na utu akiwa kwenye nafasi ya kuwa mwalimu lakini hawezi kuwa na utu akiwa kwenye nafasi ya kuwa spika wa bunge.

Mfano Mungu alimpangia mtu awe na nafasi ya kuwa mwanajeshi halafu mtu huyu akalazimisha kuwa mchungaji au padre . Hii nafasi ya mchungaji au padre sio yake kiasili, ataikalia lakini atasababisha matatizo maana hatoshi kuendana na mpango wa Mungu kwake. Mtu huyu anaweza kuwa na utu akiwa kwenye nafasi ya kuwa mwanajeshi lakini hawezi kuwa na utu akiwa kwenye nafasi ya kuwa mchungaji au padre.

Mifano ipo mingi .
 
Kwa hyo Mungu anampangia mtu kila kitu?
 

Mkuu Jamii yetu bado ina amini katika nguvu za giza katika kujipatia kipato. Binadamu tumeishiwa utu, Binadam tunadhamini Pesa kuliko uhai wa mtu.

Hawa watu walipaswa kuuwawa kwa kunyongwa tena live na kipindi kinarushwa TBC, ITV, STAR TV ili kiwafikie wengi.

Unamuua malaika huyo, malaika hana hatia mbele ya Mungu kisa tu ufanikiwe mambo yako sijui uwe tajiri au uwe maarufu kisiasa.

Rais wetu Zuia waganga wote wa Kienyeji/wajadi hawa do chanzo cha mauaji haya.

Watu wanapenda Maisha ya Miujiza, Binadam wengi hatuna subira, Watu wanataka kufanikiwa kwa siku Moja kwa kumwanga Damu za wenzao.

Nakushukuru Mungu wangu kwa kile nilichonacho sababu ni Mali yangu ya Halali.

Viongozi wa Nchi wekeeni sheria kalii zidi ya Unyama huu. Watu wanadhurumiwa haki yao ya Kuishi kisa Pesa.

Usione Mtu ana Mali Mingi, asilimia kubwa watu hao wamemwanga Damu za watu, Watu hao wamedhurumu maisha ya watu, wamedhurumu haki za watu.

Kama hutoaminii, Tafuta stori ya Tajiri wa Kanda ya Ziwa (Bariadi) PAUL MWANI.
 
Dkt. Gwajima D
 
Yaani umuelimishe mzazi asiue mwanawe?.. dooh!.. mimi huyo muelimishaji akija kwangu kwanza naanza na yeye!... shenzy... unielimishe mimi? Si matusi ya nguoni kabisa hayo?
Huyu mzazi ni katili, sidhani kama kuna Elimu inahitajika ya kutomfanyia ukatili mtoto wako.
Anyway may be kuna umuhimu Jamiii ikumbushwe upendo Tour De France
 
Hili tukio limeniuma sana sana
 
Msemaji wa jeshi la Polisi kachemka na kwenye hili litamgharimu.
Aliyekamatwa siyo Paroko msaidizi na wala siyo Padre.
Ni mraibu ambaye Paroko msaidizi alisoma naye na aliamua kumchukua Parokiani ili aweze kusaidiwa.
Hivyo kumtaja kama Baba Padre ni watu kutokutimiza majukumu yao katika kufuatilia mambo .
Paroko anaitwa Deodatus Tibakwasa na msaidizi ni Fr.Mathias.
Kifupi.
 
Kweli kuna umuhimu wa kutunga Sheria kali kuhusu hawa Waganga wa kienyeji, wamekuwa tatizo, maumivu makali amepitia huyu malaika itmanager
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…