Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Paroko?
 
Mimi kuna jambo sjaelewa yaaani wameua mtoto kwa imani za kishirikina na kuanza kutafuta wateja wa kuwauzia viungo vya huyo mtoto Inamaana waliua kabla hawajapata mteja?,Lingine mbona wahusika ni wengi sana kiasi hicho?.
Ishu ya kukosea kutaja cheo cha mtu kumbe sio chake mbona kawaida tu,Mbona Samia Suluhu aliteua mtu kumbe alishafariki?.
 
Watu kama hawa wakikamatwa inapaswa wawe wananyongwa kihadhara tena tukio likirushwa live na television ya taifa.

Inatia ukakasi sana
 
Nilijua tu kanisa haliwezi kukubali aibu hii lazima watafute njia ya kujinasua
 
Jidanganye kuwa we ni Bingwa muuaji utayeua bila kukamatwa, dola haisinzii na damu ya Mtu ni nzito kuliko maji.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
ukiona hadi polisi wametangaza hivyo, jua wana uhakika, na paroko atakuwa ameminywa maeneo fulani akafunguka hadi kuonyesha ushahidi mwingine.hawawezi kukurupuka kugusa dini.

huwa nasema, ukiona mtu ana ujasiri wa kuua albino, jua sio mara yake ya kwanza, jua alishawahi kufanya na akapona, kwasababu hakuna mwenye akili timamu anayeaminikwamba atafanya hicho kitendo halafu asikamatike. hata wanaopona ni basi tu ila hakuna anayeweza kuua albino halafu polisi wasimkamate, hayupo. na wanaofanya hivyo jua walishawahi kufanay wakapona hivyo wanafikiri hawatajulikana kama walivyokwepa mkono wa sheria awali.
 
Mahakama itachunguza ukweli wote
Mahakama isiishie kwa hawa watuhumiwa tu wakibanwa korodani list inaweza kuongezeka, kawaida biashara yoyote huwa na mtandao, hapa ndo pa polisi kuanzia, hasa wakimning'iniza mganga wa jadi kichwa chini miguu juu huku korodani zimefungwa kilo kumi kumi kila moja mganga atataja wateja na waganga wenzake wote wenye madili hayo ya kuua albino. Waganga lazima wanajuana na kukutana.

Hapa inabidi mtandao mzima utafutwe na polisi tukio kama hili lisijirudie tena maana kuua albino ni laana na fedheha kwa nchi nzima. Hii dhambi hufika mbali hata tukienda uzunguni kuomba mikopo wazungu hawatavunga watasema ooh wewe unatoka Tanzania? Utasema ndiyo, kisha watasema, ile nchi inayoua albino kwa ujinga kama wa watu wa old stone age , utabaki kimya jicho litakutoka kodooo! Mikopo na safari za uzunguni bye bye!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…