Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

SASA kADA ngoja mimi niachane na wewe maana inaonekana unaanza kukosa busara hata wadhamini wako wataanza kukushangaa mkuu

kakindo wewe kuwa against na mimi ni kama entertainment kwangu na ndio maana nishawapasha hakikisheni msije mkakimbia. hiyo ya booty camp haikuhusu wewe kabisa, bali inamhusu mgaya na anajua mwenyewe kwamba anahitajika huko booty camp ! sasa hata usiondoke, wewe kaa hapa tuhakikishe mbowe anahojiwa juu ya kauli zake !

wewe huna haja ya kwenda booty camp, anayehitajika ni huyo shahiba wako mgaya ! wanamuhitaji as fast as he can ! tena akimbie huko !
 

Kada

Suala nililokwambia kwanini Mbowe ahojiwe?

Kwani mangapi yamefanyika Tanzania na hatupati majibu yake? Kuna meremeta, kuna tangold kuna migodi kibao ambayo yanamumaliza mtanzania(mzawa). Mimi sioni kama la mbowe lingetakiwa kuwa la kwanza kuna mengi bado hayajafanyika mkuu
 
SASA kADA ngoja mimi niachane na wewe maana inaonekana unaanza kukosa busara hata wadhamini wako wataanza kukushangaa mkuu

KUna wengi wanatamani hata hakuwa upande wao huko ccm ... yaani amekuwa kama REv wright kwa Barack Obama.

Yaani mimi napenda aendelee kujiabisha yeeye na mafisadi wenzake huko ccm.
 
hata wadhamini wako wataanza kukushangaa mkuu

Originally, Kada alikuwa Chadema au upinzani, baadaye akahamia upande wa pili baada ya kuudhiwa na watu huko, sasa eti amedhaminiwa na ccm? Kwa hiyo ina maana zamani alikuwa amedhaminiwa na upinzani?
 
HIVI HAMUONI HATA MEMBE MWENYEWE ALIISHIA KUKANUSHA KAMA MTU AMBAYE AMEFUMANIWA HALAFU ANADAI 'MBONA MMETUKUTA PEMBENI YA KITANDA CHA GUEST HOUSE TUKIWA TUMEVAA NGUO, HAKIKISHENI TULIKUWA TUNAZINI ' WAKATI HUO HUO UNASIKIA HARUFU YA KONDOM ZA CHOCOLATE CHUMBANI NA MASHUKA VURURUVURUVURU!!! NA WAFUMANIWA HAWANA NGUO ZA NDANI!! UNAHITAJI USHAHIDI GANI TENA?

TATIZO MEMBE YEYE MWENYEWE NI MWANASHERIA UCHWARA. ANADHANI WOTE NI WACHWARA KAMA YEYE. INABIDI UTMIE COMMON SENSE. HIVI KWA AKILI YAKE ANADHANI UTETEZI ALIOTOA UMEONDOA SHAKA KWAMBA SERIKALI NA CCM WAMEMUUA YULE MZEE? LAZIMA UWE KICHAAA KUAMINI MEMBE AMEFANIKIWA KWA HILO.

KAMA YEYE NI MWANASHERIA KUNA KITU KINA ITWA 'RES IPSA LOQUITUR' YAANI "The facts/thing speaks for itself". kwa maana kwamba kama si mkono wa hila kile kilichotokea kisingkuwepo. Kifo cha huyu mzee hakijatokea kwa mapenzi ya mungu bali mapenzi ya CCM na serikali yake. Membe mwenyewe anajua yanaweza kumkuta ya balali akileta uzuri. Ndiyo maana unaona anatetea hata ujinga huku akijua ni ujinga.

ndo taabu ya kuwa mwanasiasa. lazima uwe mjinga. Unaweza kula mavi ukaita uji hata kama daktari akapima maabara akathibitisha kuwa ni mavi, mwanasiasa atakwambia ni uji!!
 
Prof Baregu ataka Interpol wachunguze kifo cha Ballali

Na Jackson Odoyo

SIKU moja baada ya serikali kusema kuwa hakuna sababu ya kuchunguza kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini (BoT), Daudi Ballali, Mhadhiri Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwasiga Baregu amesema kuna haja ya tukio hilo kuchunguzwa.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, Profesa Baregu alisema serikali inatakiwa ku kubali kufanya uchunguzi juu ya suala hilo na kama wao hawawezi watumie wataalamu wa Polisi wa Polisi wa Kimataifa (Iterpol).

Alisema suala la uchunguzi wa kifo cha Ballali bado lina umuhimu kwasababu yawezekana serikali haikuhusika, lakini watuhumiwa wengine katika suala lake wakahusika ili kupoteza ushahidi, kwa sababu walifahamu kuwa Balali alikuwa shahidi muhimu katika suala la Akaunti ya ya Madeni ya Nje (EPA).

Alisema suala hilo likipuuziwa litasababisha watuhumiwa hao wazidi kujificha kwani baadhi ya wananchi wanaamini kuwa Balali hakuchuwa fedha peke yake katika sakata hilo na amekufa kabla hajajibu tuhuma zilizo kuwa zikimkabili.

�Serikali haiko makini katika suala hili, kwa sababu kama kweli wanadai kuwa hawakuhusika, kwanini wasitoe hata historia ya ugonjwa kuanzia alipokuwa BoT hadi alipoondoka kwenda kutibiwa,� alisema Profesa Baregu

Alisema kitendo cha serikali kuendelea kuzuia uchunguzi wa kifo chake, inazidi kupoteza ushahidi juu ya suala la EPA na kwamba ikiendelea na ukimya huo itadhahirisha kuwa wanaohusika katika sakata hilo wataendelea kuneemeka na fedha hizo na hazitapatikana na kabisa .

Profesa alisema kutokana na uzito na unyeti wa suala hilo wananchi hawataacha kuhoji na kuendelea kupoteza imani na serikali yao, jambo ambalo ni hatari kwa mfumo wa utawala.

Juzi serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilitoa kauli zilizozidisha utata juu ya suala la kifo cha Balali kwamba, haina sababu ya kufanyia uchunguzi wa kifo cahe kwa kuwa alikuwa mgonjwa siku nyingi.


Nafikiri yupo sahihi..
 
Last edited by a moderator:
duh maskini Dr BALLALI,yaani almost 5days tokea amefariki watu bado wanashindana tu.
i wish atujie ndotoni wana JF sote kwa pamoja usiku mmoja na atueleze KISA NA MKASA yalomfika mpaka akafariki dunia hapo itakuwa mwisho wa maongezi
.
 
Nimejaribu bila mafanikio kuipata link ya hii post... aliyeiweka naomba ajikumbushe maana huu ndio wakati mwafaka....

 
Na mimi naanza kukumbuka japo waligusia gusia na hii habari sehemu kubwa ya source ilikua ni JF, turudi nyuma tutaanza kupata picha angalao kidogo kidogo. Membe anapozungumza haya naona kama ANAWEWESEKA

http://www.raiamwema.co.tz/08/01/02/3.php

 
Serikali inajikanganya kifo cha Ballali - Slaa

2008-05-27 10:23:48
Na Simon Mhina

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amesema hoja za Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Benard Membe kwamba serikali haihusiki na kifo cha Dk. Daudi Ballali, hazijaisaidia serikali, badala yake zimezidi kuleta mkanganyiko.

Alisema yeye pamoja na wapinzani wengine, walijenga hoja kwamba ni kwa nini wanaihusisha serikali na kifo hicho, tofauti na Bw. Membe ambaye amekanusha bila kujibu hoja zao na wala hakutoa maelezo ya msingi.

Dk. Slaa, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, alisema waziri huyo amezidisha kiwango cha wasiwasi walichonacho watanzania, pale aliposhindwa kutoa maelezo kwamba Dk. Ballali alikuwa amelazwa hospitali gani na ugonjwa gani
Alisema hoja ya Bw. Membe kwamba wanaotoa tuhuma dhidi ya serikali wanafanya hivyo kwa hisia, haina msingi na inadhihirisha jinsi waziri huyo anavyobabaika.

``Yaani ugonjwa wa mtu mkubwa mwenye tuhuma nzito kama Ballali, umefichwa, kifo chake kimefichwa, mazishi yake yamefichwa, hata Maiti yake haikuonekana, halafu anasema tuhuma zetu ni hisia? Huu ni upotoshaji mkubwa na kuzidi kujikanganya,`` alisema.

Mbunge huyo alisema kitu ambacho kingeweza kuinasua serikali katika tuhuma hizo, ni Bw. Membe kutaja sehemu aliyokuwa amelezwa Dk. Ballali.

``Tangu lini hospitali ikawa ni sehemu ya siri, kwa nini hawataki kusema?`` Alihoji.
Alisema madai aliyotoa waziri huyo kwamba mwenye vielelezo toka kwa daktari vinavyoonyesha kwamba Dk. Ballali alikufa kwa sumu avitoe, au yanaonyesha kwamba kweli kifo cha Gavana huyo wa zamani wa BoT kilipangwa.

``Mtanzania wa kawaida atawezaje kumpata daktari aliyemtibu Ballali wakati hata hospitali alipokuwa amelazwa panafichwa? Kumbe wameficha kwa makusudi ili Watanzania washindwe kupata vielelezo?`` Alihoji na kuongeza: ``Serikali haihitaji vielelezo, bali ndiyo iliyofanya njama za kuhakikisha hakuna kielelezo chochote ambacho kinahusiana na kifo hicho kinachoweza kupatikana.``

Alisema kama kweli serikali inasisitiza kwamba haihusiki, itaje hospitali ambayo Dk. Ballali alikuwa akitibiwa na ugonjwa uliomsibu.

``Bw. Membe anasema mwenye vielelezo apeleke? Kazi yake kama waziri wa Mambo ya Nje ni ipi hasa?

Yeye ndiye alitakiwa azungumze na Balozi wetu kule Marekani ili aeleze habari za ugonjwa na baadaye kifo chake, kama mtu mkubwa kama Ballali anaweza kufikwa na kifo nchi za nje bila watu kujua, sembuse mtu wa kawaida?`` Alihoji.

Dk. Slaa alisema ili serikali ijisafishe, ni vizuri ikasema ni kwa nini hata hapa mjini, matanga ya marehemu huyo yalikuwa ya siri na majirani walikatazwa kuingia huku waandishi wa habari wakifukuzwa.

``Tunataka iundwe tume huru ya kuchunguza kifo hicho, kwa vile hadi sasa serikali haijatoa maelezo yanayojitosheleza. Tunataka tume kwa vile pesa za EPA bado ziko mikononi mwa mafisadi, ambao huenda ni marafiki wakubwa wa serikali,`` alisema.

* SOURCE: Nipashe
 

Mkuu....Uchunguzi ni muhimu katika suala hili, lakini kuihusisha Interpol....Sidhani, kwani hakuna kipengele katika katiba ya Interpol kinachosema kuwa wanaweza kufanya hivyo; wao shughuli zao ni tofauti kulinganisha na suala la Balali lilipofikia.

Kuhusiana na serikali kutoa historia ya ugonjwa wa Balali, nayo pia sio rahisi, nina imani tuna kitu kinachoitwa "Privacy Act" serikali haiwezi kukurupuka tu na kutoa medical records za mtu kisa wanataka kujivua lawama.
But tunaweza kuishinikiza Serikali itupe zaidi ya inachotoa kuhusiana na habari hii, nina imani wanajua zaidi ya wanavyosema.....
 
Watulizane..wao wenyewe waliwahi kusema hana msaada wowote na wala hawataki kusikia...au ndio mtu akifa yanaisha yote???
 
Mamaye Ballali alindwa

na Kulwa Karedia

HALI ya ulinzi mkali imeimarishwa nyumbani kwa mama mzazi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) marehemu Daudi Ballali.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana nyumbani kwa mama huyo Boko, Dar es Salaam, zinasema kuwa ulinzi huo umewekwa na serikali kupitia BoT tangu kutangazwa kwa kifo cha Ballali wiki iliyopita.

“Tumesikia ulinzi huu umewakwa na serikali kwa kushirikiana na BoT kwamba hakuna mtu yeyote kuingia hapa, tunashangaa sana kuona hata sisi ambao tumekuwa naye hapa tumebaki kuwa watazamaji tu,” alisema Seif Omar, mkazi wa Boko.

Alisema kitendo kilichofanywa na serikali si cha kiungwana, kutokana na ukweli kwamba msiba huwa hauchagui maskini au tajiri wa kwenda kuzika mwenzake au jirani yake.

Tanzania Daima jana ilipofika nyumbani kwa mama huyo anayeishi nyumba namba BNJ/BOKO/1081, ilishuhudia hali ya ulinzi mkali, kitendo kilichosababisha hata mwandishi wa habari hizi kuzuiwa kuingia ndani.

Baada ya kuwasili nyumbani, mmoja wa walinzi wa Kampuni ya Regimental Security aliyekuwa getini, alikataa katakata kufungua geti hilo kwa madai kuwa amepewa maelekezo kutoka ngazi za juu serikalini na BoT.

“Nikusaidie nini, unaitwa nani na una shida gani ndugu…tafadhali nionyeshe kibali chako cha kuingia humu ndani kutoka BoT, na kama huna, nakuomba uondoke eneo hili,” alisema mlinzi aliyekataa kutaja jina lake.

Alisema yeye amepewa maelekezo hayo na maofisa wa juu wa BoT, ambao hakuwa tayari kuwataja majina na kusisitiza kuwa anatekeleza majukumu yake ya kazi.

“Nashindwa jinsi ya kuwasaidia…jamani nawaomba sana muondoke hapa,” alisema mlinzi huyo na kuendelea kufunga geti hilo, kitendo kilichoashilia kuna shinikizo kutoka juu.

Juhudi za gazeti hili kumuona mama mzazi wa Ballali ziligonga mwamba kutokana na hali ya ulinzi iliyopo.

Wakati huo huo, baadhi ya wananchi waliohojiwa na Tanzania Daima kuhusiana na kauli ya serikali juu ya kifo cha Ballali wamesema serikali inapaswa kueleza ukweli baada ya kuuficha.

“Tumeshangazwa na kauli ya serikali, tunaelewa wazi kwamba Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, atakuwa ameelewa ukweli, sasa kwa nini atufiche?” alihoji Dickson Juma.

Alisema kama kifo hicho kisingekuwa cha siri, kwanini serikali ilipata kigugumizi kusema ukweli kuanzia ugonjwa wake hadi anafariki, jambo ambalo linazua maswali mengi.

“Sisi tunasema umefika wakati sasa wa kuelezwa ukweli na kama sivyo, basi iundwe tume haraka kabla ya mambo haya hajapoa, maana tunajua yakipoa, ndiyo yamekwisha,” alisema Juma.

Naye Mwanakombo Hussein alisema kitendo cha serikali kushindwa kushiriki katika mazishi ya Ballali kinaonyesha wazi kwamba kuna matabaka ndani ya viongozi wa serikali.

Aliwataka wananchi wote kuungana na kuishinikiza serikali ili kuhakikisha inaunda tume huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina na majibu yatolewe haraka.

Marehemu Ballali alifariki dunia Mei 16 jijini Washington, Marekani, alikokuwa akipata matibabu tangu mwaka jana, baada ya kufukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kuhusishwa na ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambako zaidi ya sh bilioni 133 zinadaiwa kupotea.

 
Kazi kweli kweli!!!! mambo mengine moto!!!! Kudadadeki!!!!
 
tunao kesho hawa tunao!!!! sehemu ya kwanza ya kuwabana ni kesho.... whistling... wamelikoroga wenyewe.. wajiandae kulinywa!
 
tunao kesho hawa tunao!!!! sehemu ya kwanza ya kuwabana ni kesho.... whistling... wamelikoroga wenyewe.. wajiandae kulinywa!

Hapa nilipo nimeaandaa muziki utakaocheza kwenye background na sound effects zote muhimu kwa ajili ya second episode ya hii series...

muziki mupya utakuwa...

taratata ta nta tata ta ta ta.... tarantata ta nta nta tatatata....
 
BOT na serikali yao ni wapotoshaji......
hivi balali amekufa huru, hakuwa mshutumiwa wala serikali haikuwana haja nae, lakini leo nyumba ya mama yake inalindwa kwa ulinzi ulioidhinishwa na BOT ( kwa mujibu wa magazeti)....jee huyu mama ni muhimu kuliko balali mwenyewe? au ndio mama analindwa kuficha siri nyengine?
yangu macho na masikio tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…