Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
You said this a hundred times before. But you keep wading back into it, full throttle.
it can't be truer, you probably chose the best option among the infinity
Huyu jamaa bdo hajapatikana
Yote yalipitaSiko peke yangu karibu na Ukweli!....
Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.
"Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti," alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.
Aliongeza Warioba: "Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.
"Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.
"Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.
"Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.
" Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika."
Haya mamafia hayawezi shindwa kitu...yanaweza zika hata mbuzi yakasema ni BalaliTaarifa za kifo hapa marekani ni public info!
Na si familia inayotoa habari hizo kama wanavyodai kina Kishoka!
Habari hizo hutolewa na coroner kwenda kwenye magazet and so forth!
Na hao wenye hiyo funeral home nao wasiwasi sana kwasababu hata wao walitakiwa wawe na database yao ili tuweze kusearch watu waliokufa kama vile funeral home nyingine zinavyofanya!
Habari hizi tayari zingeshakuwa public hadi sasa!
Kwanini zinazuiliwa isivyo kawaida?
Hiyo funeral home nayo tutaichunguza tu!
![]()
Ni kweli jambo la ku-fake vifo sio geni hapa duniani. Lakini kwa hili ni vigumu sana kuamini vinginevyo. Si Balali tulikuwa tunamjua kwa sura, mliopo Washington hakikisheni hamkosi kwenye mazishi.
Hata hivyo, ni muhimu sasa kwa kuwa habari hizi zimeshakuwa wazi, watoa habari wetu hapa JF watupe source za habari zao. Hili ni muhimu kwa sababu njia za kupata taarifa ni muhimu sana katika ku-judge credibility ya hizo taarifa. Nami najiuliza yale mafumbo yote ya MKJJ wakati alijua ukweli yalikuwa ya nini hasa?
Then, kitendo cha FMES kukanusha kwa dhati kabisa habari za kifo cha Balali nacho kinazidi kutia kiwingu maana huyu bwana anaheshimika kwa kupata habari nyeti. Mimi bado naendelea kuamini kwamba huyu bwana alishaanza. Sasa kwa nini habari hizi zimetoka five days baada ya kifo hili ni swali ambalo inawezekana tusipate jibu lake milele!!