Watu wengine bwana!!! Wakiweka wao "Dataz" humu basi wanataka kila mtu azikubali. Wakiweka wengine basi wataambiwa mpaka waweke video au sound recording ndio ziaminike.
Mkuu Heshima mbele, mimi ninapoweka dataz zangu huwa nina uhakika nazo 100%, na wewe unajua wazi kuwa hazijawahi kuwa batili au za uongo ndio maana huwa sihitaji tape record, na nikizitoa within siku tatu kuna watu hapa hujitokeza na kusema wamethibitisha, kwenye hii topic nimetoa dataz nyingi ambao zote zimethibitishwa kuwa ni kweli na nimesema wazi kuwa nimeshindwa kupata jina alilokuwa analitumia Balali akiwa Hospitali, halafu bado nina utata na tarehe aliyofariki na ni kwa sababu moja tu nayo ni kwamba Mkulu Wangu Mwanakijiji bado haridhiki na tarehe, kwa sababu ninamuaminia kwa dataz ni kakubali kuwa tarehe ina utata,
Otherwise, mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kwa taifa zima la bongo kutoa dataz za alipofia marehemu Ballali, atakapozikwa, jina la Pastor wa kumzika na kanisa lake, na mpaka Hospitali aliyofia, na nikasema kwa mara ya kwanza jinsi mama wa marehemu alivyoshambuliwa na "majambazi" jinsi mke wa marehemu alivyokwenda kumuuguza, je kuna any of this dataz ilihitaji tape record?
Now ninaomba tena niseme hivi, hapa wote ni watu wazima, niaamini kuwa hakuna watoto wadogo, unapoleta dataz zinazosema kuwa eti katika nchi ya USA tena mji wa DC, kuna Pastor wa Kanisa kubwa kama la St. Stephen , kwamba huyu Pastor aliendesha misa kubwa ya marehemu a former Gorvernor wa Bank Kuu ya Tanzania, lakini toka siku ya kwanza aliyofahamishwa kuhusu kifo, mpaka kuletwa maiti kanisani na kuombewa kabla ya kwenda kuzikwa kaburini, anapotokea mtu wa kusema kuwa eti Pastor yule amesema kuwa hakuuona mwili katika anytime ya hizi shughuli, hapo wakuu tunakuwa tumefika mbali sana na hizi dataz! Eti kwamba haya yote yametendeka USA na kweli kuna watu hapa JF wanakubali hiyo as a fact, basi CCM itatawala bongo milele!
Mkuu Mtanzania,
Ninaliheshimu sana gazeti la Thisday na Kulikoni, wao wamekataa kabisa kwa sababu hawana vithibitisho vyote, na ninawaheshimu kwa kukataa ku-speculate anything, that is the way to go lakini sio kuanza kulaumu watu au kulaumu tu bila mpango na kuanza kutafuta watu uchawi wa bure, it is not fair! Kwa wale wanaomamini hajafa basi watuletee dataz nzito, lakini sio hizi nyepesi nyepesi, mimi ninaamini kuwa Balozi Sefue, aliuona mwili kwa sababu asingeuona basi bosi wake wa kazi Membe asingethibitisha kifo hicho au hata rais pia, sidhani kama hili linahitaji elumu kubwa kuelewa na hata kuelezea watu wenye akili nyingi kama hapa JF!
Mkuu Mtanzania ninaheshimu sana your stand on this ishu, na wengine wote walio pamoja na wewe, ninachosema ni kuwa kwa sisi wenye msimamo tofauti na hasa inavyoonekana ni mimi peke yangu so far na sisi pia tuheshimiwe na pia haki yetu kuuliza ukweli wa dataz za kutoka huko kwenu pia iheshimiwe kama sisi tunavyoheshimu haki yenu mkuu, ndio maana ya demokrasia tunayoidai toka kwa serikali yetu, sasa hizi name calling na accusations kama kweli tuna hoja ni za nini? Watu wakubali kuwa hawaamini lakini hawana facts, lakini logic kwenye hii ishu haziwezi kutatua tatizo, JF tunaheshimika sana na taifa kwa dataz na ukweli wa ishus muhimu za taifa letu, lakini kwenye hili wakuu tunayumba sana na tumeyumba sana, sisi siku zote huwa ni watu wa majibu tena very serious ones, sasa tatizo kwenye hili ni nini hasa?
Kama tumeshindwa kupata ukweli, basi tusubiri tutakapoupata, lakini ku-specualte kama magazeti ya kina majira na kasheshe ambao wao pia wanategemea sisi ni waste of our time, mimi ninashindwa kuyaelewa magazeti yetu, tumewapa dataz za kutosha kwenye hiii ishu toka Balali alipoondoka tu, lakini mpaka leo wanachoandika hakieleweki? Wote tunajua jinsi Mwandishi Pearly alivyokufa kule Pakistan, akifuatilia kina Osama, sasa sisi Tanzania tulishindwa nini kutuma waandishi wa kufuatilia ishu ya Balali alll that time, sasa tunaanza kutafutana uchawi?
Ndio maana nilisema kule nyuma kuwa kwenye hili la Balali wa-Tanzania wote tuko guilty kwani wote tumeruhusu kutokea bila ya kufanya anything about it, pamoja na kwamba tulikuwa na all the facts kutokana na the past kwamba this was coming, sasa tutafute ukweli wa kile tunachoamini na tukiseme hapa, kama hatuwezi tusubiri huenda siku moja kuna ukweli zaidi utatokea, lakini tusiendeele kujishusha hapa na kutafuta umaarufu wa bure wakati ukweli hatuna!
Mkuu Wa Pwani, ndugu yangu usiwe na wasi na wasi mimi, mimi sina noma kwenye kuelimishana, maana ndio hasa kinachowaketa wananchi hapa JF huwa sichoki kwenye hilo na siku zote huwa sikimbii maswali ya wananchi, ninasema nipo na nitajibu anytime ikibidi,
Mkuu Ibambasi, ahsante mkuu kwa support lakini ninakuomba next time usifanye hilo tena la kunitetea maana utashambuliwa sana hapa, mimi ninabeba masalaba wangu mwenyewe tena bila tatizo, na the buck stops here, huyu jaama anayetaka kutuyumbisha hapa JF ninamjua na nimeshamuona na niko bega kwa bega naye ninakula naye sahani moja, na ninajua mbinu zake zote, unajua huwezi kupigana na adui ambaye hujui silaha zake, ana silaha nyingi sana na ninaona tayari watu wengi hapa wameanza kuupanda mkenge wake, lakini ninasema kuwa ni ukweli tu ndio siku zote utakaosimama hapa JF, na sio uongo na ni watu wakweli tu ndio watakaodumu hapa JF, na sio wahuni na wajinga wajinga, maana sisi tulikuja hapa JF kuyakwepa magazeti ya bongo, ambayo mimi nilikuwa mtu wa kwanza hapa kusema kuwa yote yalikuwa yamenunuliwa na mtandao!
Ahsanteni Wakuu!