...ahsante mkuu. Nimekubali.
mchongoma huna tofauti na mwenda kuzimu, usituletee masihara watu tuna hasira za kweli. oohoo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...ahsante mkuu. Nimekubali.
Kama ni kweli alizikwa kikatoliki kama inavyodaiwa, kuna hatua ambapo padri huwa anamfunua uso maiti na kumnyunyizia "maji ya baraka". Sijui kama padri huyo alikwepa hatua hiyo? Inapaswa aulizwe, wenye nafasi huko tusaidieni hiyo kazi. Hii kitu kama inaisha vile lakini inaibuka upya mara kwa mara!
Mkuu Mtanzania,
Na wengine heshima mbele, mimi kama Mkristo safi hii ishu nimeinawa mikono, ninaomba tena kusema ninchojua na kilichonifanya ninamini na bado ninaamini kwa 100% kuwa Balali amefariki, lakini pia ninaheshimu sana mawazo ya wale wanaoamini kuwa yupo:-
Nina uhakika kuwa alifariki Jumapili nyumbani kwake, alishughulikiwa in one way or another katika hospitali ya George Washington University Hospital lakini sio kwa jina la Balali, na hili jina la Siriani mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kulitoa, na mpaka jina la kanisa la huyu padri mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kuyatoa, sasa ninashukuru kuwa kuna waliofuatilia kama nilivyoomba kule nyuma,
Ninaamini kuwa Balozi Sefue aliuona mwili, ndio akamuarifu rais na Membe, wakuu mimi as a Christian huu ni ushaidi tosha mbele ya Mungu wangu kuhusu kwa nini ninaamini kuwa amefariki, na ninaomba ninawe mikono hapa, lakini kwa yoyote anayetaka msaada zaidi nitampa kama nilivyowapa magazeti, katika kufanya uchunguzi zaidi, ila mimi dini yangu na Mungu wangu inanikataza kuendelea zaidi ya hapa nilipofikia na uchunguzi,
Lakini ninazisoma lines in the betweeen kwa makini sana, na ninawatakia heri wanaoendelea lakini akama kawa sina tatizo kutoa msaada kwa walio serious, pia nitoe respect kwa Majira na wengineo kwa msimamo imara wa kutoyumbishwa, that is waht we need kwa taifa letu.
Ahsante Wakuu!
jamani naomba huyu padri apigiwe tena simu aulizwe mambo zaidi, pengine tukagundua mengine, na vile vile huyu padri anaweza kuwa pia ni wa kuchonga. maana pesa iliyoliwa ni nyingi kiasi inaweza kufanya lolote lile,sintokaa niamini kifo hiki kamwe
Mkuu Kinepi,
Wewe unafaa kuwa mwandishi habari za uchunguzi.
Umeniacha hio na hio kazi ulioifanya...
::Habari za Tanzania Jumatatu Juni 09, 2008
Imetolewa mara ya mwisho: 08.06.2008 1519 EAT
Mchungaji aliyemzika Ballali anena
*Athibitisha aliumwa kwa muda mrefu
*Aeleza alivyoongoza ibada, maziko
Na Hassan Abbas
WAKATI Watanzania wakiwa bado katika hali ya sintofahamu kuhusu ukweli juu ya kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Daudi Ballali, Mchungaji aliyeendesha misa na hatimaye maziko yake nchini Marekani amekizungumzia kifo hicho na namna maziko yalivyokuwa.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili kwa njia ya mtandao, Mchungaji Klaus Sirianni wa Kanisa Katoliki la St. Stephen Martirs' lililoko District of Columbia, Washington DC, amelithibitishia gazeti hili kuwa Dkt. Ballali alikufa na yeye ndiye aliyeongoza misa na baadaye ibada ya maziko.
"Ni kweli Dkt. Daud T.S Ballali alifariki Mei 16, 2008 akiwa na baadhi ya wana ndugu zake hapa nchini Marekani," alisema Mchungaji Sirianni.
Kumekuwa na uvumi unaozidi kuenea nchini ambapo wengi wanahoji ukweli wa kifo cha Dkt. Ballali huku baadhi wakitaka kujua kama kweli kulifanyika ibada ya maziko mjini Washington kama ilivyokuwa imetangazwa.
Akithibitisha kufanyika kwa misa na ibada ya maziko ya Ballali, Mchungaji huyo ameliambia Majira Jumapili kuwa: "Misa iliyofanyika katika tamaduni za kikristo ya Dkt. Ballali ilifanyika kwenye Kanisa la St. Stephen Martyr, Washington, District of Columbia, kuanzia saa nne asubuhi, Mei 23, 2008."
Akaongeza kuwa yeye ndiye aliyesimamia misa na baadaye maziko hayo. "Aliyeongoza misa na ibada ya maziko ni mimi Mchungaji Klaus Sirianni," alisema mchungaji huyo ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa parokia ya kanisa hilo.
Katika maziko hayo Mchungaji Sirianni amethibitisha kuwa wahudhuriaji walikuwa ndugu, jamaa wa karibu na watu waliowahi kufanyakazi na marehemu huku akimtaka mwandishi kwa maelezo zaidi kuhusu sababu za kifo hicho awasiliane na wanafamilia.
"Maziko yalifanyika kwenye makaburi ya kikatoliki ya Gate of Heaven yaliyoko eneo la Silver Spring, Maryland na kwa mara nyingine mimi ndiye niliyesimamia ibada hiyo tena."
Kinepi
Baada ya kusoma habari hii, nilinyanyua simu nikampigia Padri Klaus Sirianni wa kanisa katoliki mtakatifu Stephen Martyr, Washington, District of Columbia,
Maswali na majibu yalikuwa kwa lugha ya kiingireza ila nitachapa kiswahili.
swali. padri habari za leo
jibu: Nzuri
maelezo: mimi ni kinepi Mtanzania,Nimepata taarifa kuwa wewe ndiye ulieendesha misa ya marehemu Dr. Daudi Balali
jibu: Ndio
swali: utajali kama nikikuuliza maswali kuhusu misa ile na huduma yote kwa ujumla
jibu: hapana
Ndio, Balali alifariki na mimi ndie niliyeendeshasha ibada ile mpaka makaburini akazikwa.
Swali: Padri je katika huduma yako hiyo ulipata kuuona mwili wa DR. balali ???
Jibu: Hapana.sikuuona.
Swali: Je ulipata wasaa wa kufunguliwa jeneza hata mara moja?"
Jibu: Hapana jeneza halikufunguliwa, niliamini maneno ya ndungu za marehemu kwamba aliyeko humo kwenye Jeneza ni Balali.
Swali: Je si lazima kujua nini kipo ndani ya jeneza kabla ya kukiombea?
jibu: ni vyema ukauliza ndugu za marehemu kwa maelezo zaidi.
kinepi: asante padri kwa muda wako, kwaheri.
Kutoka ubalozini wanarushiana mpira kuwa ni nani aliuona mwili.
Mpaka sasa Kifo cha Balali ni kitendawili.
Ninafanya jitihada kujua ni hospitali gani alilazwa. Nikipajua tu au mtu yeyote kama ana info tafadhali anipatie lazima ni jue Balali yuko wapi.
Majibu ya wizi wa fedha zetu ni muhimu sana.
kwani hata wewe unashindwa kuhongwa? usichezwe na nguvu ya pesa bana .kwani hata hapo ulipo wewe si unahangaikia mkate wako wako wa kila ?sasa ikitokea ukaupata kwa njia ya mkato zaidi utaukataa?
Shikamoo Mzee ES...Hapa JF tunakataa haya ya kufikiria ndani ya box lako tu na kudhani ni lazima uwe ukweli wa wote wengine that is pathetic thinking!, leave a lone kuisema mbele ya hadhara duh!
Ukisikiliza kwa makini kinachosemwa hapa, ni kwamba Padre anakubaliana na sisi, kwamba jamani eeeeh! God knows what was inside that big box! I may be a Priest, but I can't see thru wood, and I couldn't tell ya!
Nikisema niliongea na Padri na kwamba alisema ndani ya jeneza kulikuwa na mbuzi nitakuwa ninasema ukweli au uongo? Wakuu tafuteni hoja nzito za kusimamia hoja yenu kuwa Balali yupo lakini sio hizi nyepesi nyepesi, unless kuna mwenye tape aliyomrekodi huyo Padri, hii mimi siikubali lakini sina tatizo kukubali mengine yenye more proof zaidi kuliko niliongea naye!
Kwenye hili hata hawa waandishi wanakuwa wajinga wajinga tu!
haya later......!
samahani maelezo ya mahojiano na Padri yamechelewa kidogo.
Bali Padri kwa kinywa chake amekiri hakuona mwili wa Balali.
Simu ya kanisa ni : 202 785 0982.
mwacheni mzee es apumzike jamani!!!
masharti ya kuomba dua ya mwisho, ni lazima uone mwili au inasaliwa kutokana na imani ?? huyu padre pengine ni MAFIA TU ! sasa maiti ya nini ? kama hakuona kwa nini aliisalia ? najua alisali kutokana na imani, sasa anasema hakuuona mwili iweje aliisalia "maiti" if it was a bad idea bila ya kuiona ? hamna lolote hapa !