Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Wandugu Balali amefariki......na tuamini hivyo!

Mkuu FD,

Ndio maana Waafrika tunadanganywa mara nyingi, ni wepesi wa kuamini yasiyoaminika.

Mimi shuleni nimefundishwa usiamini kitu bila kuwa na data, unaweza kushindwa kupata ukweli lakini sio sababu ya kuamini. Ndio maana kwenye kiingereza kuna msemo wa the jury is still out.

Sasa kama mtu utaamini tu kwasababu mke wa marehemu kasema bwanake kafa wakati
info zingine zote zinazoongozana na mtu kufa hazipo, basi ni hiari yamtu kuamini. Sisi wengine ni Engineers, hatuamini maneno, tunaamini data, info.

Hata wanasheria wanaamini jambo kulingana na shahidi, sasa kama shahidi ni mama Muganda ambaye hata hawezi kutoa tarehe sahihi ya bwanake kufa na mahali alipofia, ingelikuwa mahakamani, mashahidi kama hao ni kutupwa nje. She is definately not a reliable witness, do you want me to trust her? Do I trust her? The answer is: unequivocally, undubiously NO. On this one, I would rather be a Thomaso than be taken for a ride by fisadi jike.
 
Ahaaaaa umenifurahisha Mtanzania.

Jamaa amefariki kweli. Amini amini nakwambia. Mimi naamini kuwa Balali hakuwa na tatizo hata kwenye utendaji kazi wake. Tatizo ni VIONGOZI WETU waliokuwa wanaamuru hela zichotwe!. Hebu fikiria, kwanini serikali ilikuwa haimtaki arudi?, ukishalijibu hilo utapata mwanga. Na jibu ni kuwa alikuwa hatari kwa usalama wa taifa. Angeweza kumwaga "Kuku wengi kwenye mtama"(sic).

Mungu amlaze mahali pema peponi. Aaamin
 
FD,

Kwi kwi kwi kwi!!!!!

Si ndio maana usalama wa taifa wamempa vitambulisho vipya ili apotee kimoja na asiwe hatari kwao tena?

Mimi nasubiri dossier tuliloahidiwa, changa lingine la macho!
 
Ahaaaaa umenifurahisha Mtanzania.

Mimi naamini kuwa Balali hakuwa na tatizo hata kwenye utendaji kazi wake. Tatizo ni VIONGOZI WETU waliokuwa wanaamuru hela zichotwe!.

Hili ndio tatizo lenyewe ambalo ni kubwa kuliko kuiba kwenyewe. Amini usiamini, kuanguka kwa Afrika yetu kunachangiwa sana pia na wataalamu wetu. Kama wewe ni mtaalamu na unakubali kufanya jambo ambalo mwanasiasa anakwamba na ukijua kabisa kwamba halijakaa sawa, hapo wa kumlaumu sio mwanasiasa tena, ni huyu mtaalamu. Kama kweli Balali aliamuriwa kuchota pesa na huku akijua kuwa ni haramu lakini akaendelea kukubali, tunatakiwa tumlaani milele bila kujali kama yupo dunia hii au la.

Na wewe ndugu yangu FD, kama kweli unafanya kazi huko serikalini, heshimu sana utaalamu wako kabla ya kitu kingine. Dunia ya leo sio ya ku-compromise profession maana kila mtu anawajibika kwa matendo yake. Ukiharibu hakuna atayekuelewa eti wanasiasa walikuamuru.
 
Kitila,

Tuangalie real situation hapa. Chukua mfano wa genge la majambazi. Wamekuajiri huku hujui ni majambazi wakakupa uweka hazina na kuwatunzia fedha zao. Mkuu wa genge akakwambia tunataka kiasi kadhaa kwa ajili ya usalama.

Ukapewa barua kabisaa kuwa mlipe huyu kwa vile ni espionage sio vizuri zikaonekana zinaenda wapi. ukabisha, mkuu akakupigia simu. Utafanyaje?

Ukisema uache kazi upotee..kumbuka ni genge la majambazi yatakutafuta na kukukolimba. Vilevile hapo unafikiria AJIRA PIA.
Mwishoni ukaona aahhaa kwa vile ni mkuu mwenyewe kasema hamna neno atanilinda tu.

Baadaye mambo yakaharibika, ukatolewa mbuzi wa kafara. Wewe ungefanyaje ktk situation kama hiyo?
 
Kitila,

Bahati mbaya mimi ni mfanyabiashara wa hardware hapa Mbagala. karibu sana ndugu yangu ununue Cement na mabati.
 
FD,

.......haya bana tumekusikia......mi nitakuja kununua cement kwako hivi karibuni
 
Kitila,

Tuangalie real situation hapa. Chukua mfano wa genge la majambazi. Wamekuajiri huku hujui ni majambazi wakakupa uweka hazina na kuwatunzia fedha zao. Mkuu wa genge akakwambia tunataka kiasi kadhaa kwa ajili ya usalama.

Ukapewa barua kabisaa kuwa mlipe huyu kwa vile ni espionage sio vizuri zikaonekana zinaenda wapi. ukabisha, mkuu akakupigia simu. Utafanyaje?

Ukisema uache kazi upotee..kumbuka ni genge la majambazi yatakutafuta na kukukolimba. Vilevile hapo unafikiria AJIRA PIA.
Mwishoni ukaona aahhaa kwa vile ni mkuu mwenyewe kasema hamna neno atanilinda tu.

Baadaye mambo yakaharibika, ukatolewa mbuzi wa kafara. Wewe ungefanyaje ktk situation kama hiyo?

Mkuu FD,
Hivyo ndio visingizio vya wataalamu wetu kuhalalisha kuvurunda kwao.

Hakuna cha mtu Kukukolimba wala nini, badala yake ni woga usio na maana yoyote na pia
sababu za kuficha ujambazi wao.

Tatizo letu ni ubinafsi na ujambazi. Hayo mambo mengine yote ni visingizio tu.

Ballali alikuwa na uwezo kabisa wa kusema NO na kujirudia zake USA kuchapa kazi. Mtu kama Ballali akishindwa, vipi watu kama FD ambao japo hamna kwingine kwa kukimbilia?

Lakini pia hata baada ya kufanya makosa, alitakiwa atoke clean na kuacha kuendelea kudanganya , anaenda mpaka bungeni kwenda kuwadanganya wabunge.

Ukiangalia EPA, wale watu wengi waliopewa hizo pesa ni wajanja wa mjini tu, ambao waliona opportunity na uzembe wa maofisa wa BOT na wakaitumia. Huwezi kusema cases zote za EPA ni usalama wa taifa kumlazimisha Ballali. Ingelikuwa hivyo yale ya Meghji na Ballali yasingelikuwepo.
 
katika "pita pita yangu".. nimekutana na source inayosema kuwa kuna video na audio files za Ballali kuelezea kilichojiri EPA na madudu mengine... (sijui ni lini vilirekodiwa hivi na kama vilikuwa mbele ya wakili)...

Mkapa nasikia alikuwa achepukie DC kidogo "kusalimia" jamaa kwani hili wazo kuwa Ballali yawezekana kuwa ameacha "maelezo" ya kina kuhusu kilichojiri linamsumbua sana..
 
Kama wewe ni mtaalamu na unakubali kufanya jambo ambalo mwanasiasa anakwamba na ukijua kabisa kwamba halijakaa sawa, hapo wa kumlaumu sio mwanasiasa tena, ni huyu mtaalamu. Kama kweli Balali aliamuriwa kuchota pesa na huku akijua kuwa ni haramu lakini akaendelea kukubali, tunatakiwa tumlaani milele bila kujali kama yupo dunia hii au la.

Kitila, kama wanataaluma wetu wangekuwa na mtazamo huu, Tz tungesonga mbele. Tatizo wanataaluma nao wameacha taaluma zao na kuvamia siasa. Hatufiki.
 
Kitila,

Tuangalie real situation hapa. Chukua mfano wa genge la majambazi. Wamekuajiri huku hujui ni majambazi wakakupa uweka hazina na kuwatunzia fedha zao. Mkuu wa genge akakwambia tunataka kiasi kadhaa kwa ajili ya usalama.

Ukapewa barua kabisaa kuwa mlipe huyu kwa vile ni espionage sio vizuri zikaonekana zinaenda wapi. ukabisha, mkuu akakupigia simu. Utafanyaje?

Ukisema uache kazi upotee..kumbuka ni genge la majambazi yatakutafuta na kukukolimba. Vilevile hapo unafikiria AJIRA PIA.
Mwishoni ukaona aahhaa kwa vile ni mkuu mwenyewe kasema hamna neno atanilinda tu.

Baadaye mambo yakaharibika, ukatolewa mbuzi wa kafara. Wewe ungefanyaje ktk situation kama hiyo?

Huwezi kufurukuta tu kama umefungwa pingu. Haya sasa hiyo ya yeye kuogopa kukolimbwa yamemsaidiaje? Mimi naamini kabisa isingekuwa kusaidia kwake katika ujambazi wa fedha za EPA, Balali angekuwa bado mzima (assuming sasa hivi kweli ametangulia mbele za bwana).

Nakukuhakishia FD wataalamu wengi wetu ni woga kuliko hali halisi; wanaogopa mambo ambayo hayapo. Kwa uzoefu wangu mdogo wa ku-deal na wanasiasa matapeli kama wale wa CCM ni kwamba wanaheshimu na kumuogopa sana mtu mwenye msimamo madamu usiyumbe katika msimamo wako. Tatizo la wataalamu wetu wengi wanauma na kupuliza; wanataka kutunza profession zao na hapohapo wanataka hela za harakaharaka. Bahati mbaya professional intergrity and quick money do not go together, at least in the real world.
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele bro, nilisema toka last two weeks kuwa Balali ameacha live video na Tape records, swali ni je hizi zitakuwa na nini cha maana kuliko angekuwepo mwenyewe, kwa sababu kama kuna interest ya kutaka ushahidi wake, walikuwa wapi akiwa mzima na akiwa Dodoma, sasa leo hayupo ndio waazne ku-hype video zake, that does not make a sense unless kama kuna something nina-misss!
 
FMES,
Kinachonishangaza mimi ni resort ya Balali, kwanini aliona bora kuacha vedio tapes na tape records kuliko kuuleza umma LIVE? Sidhani kama aliitendea haki Tz.
 
FMES,
Kinachonishangaza mimi ni resort ya Balali, kwanini aliona bora kuacha vedio tapes na tape records kuliko kuuleza umma LIVE? Sidhani kama aliitendea haki
Tz.
Hivi ulimwona alipokuwa hai? Ulijua alikuwa katika hali gani?
 
Hivi ulimwona alipokuwa hai? Ulijua alikuwa katika hali gani?

Kwa hiyo ame shoot hiyo video akiwa kitandani sio? Labda mwenzangu umeshaiona, tueleze.

Assuming alishoot hiyo movie akiwa mahututi, hivi unataka kusema kwamba Balali hakujuwa kilichokuwa kinamjia hadi alipokuwa taabani?
 
I'd rather play drums under water than continue this debate.
 
I'd rather play drums under water than continue this debate.

You said this a hundred times before. But you keep wading back into it, full throttle.

Jasusi, as much as you may sympathize with Ballali's family and find our discussions absurd, you may not wish this thing away. It's not as negligible to everybody else as you would like to think.

I believe that most conspiracy theories are simply absurd. The idea that Anna Muganda has feigned his husband's death, that she planted a phantom body in the casket and took it to church, and lied to her friends and Government officials about all this thing, I think is extremely far-fetched, if not preposterous. I just don't fall for such home-made "dataz" without sensible substantiation.

Indeed, if I was in Anna Muganda's shoes, and truly believed that my husband had been smeared and scapegoated by some vicious corrupt officials, I probably wouldn't even invite the Ambassodor to the funeral, let alone tell him. I appreciate all that aspect of Muganda's possible thinking.

However, this is no ordinary death, and the whole thing is shrouded in mystery, and you know it. Ballali was not a regular Chumvi na Nyonzo. A central Bank was robbed of national treasure under his charge, before he eased off the face of the earth to "a hospital." We, the People, I think, and you will be kind to agree, have every right to ask questions regarding this dark death. The government is so secretive it would not tell us who they were paying to treat the ex-governor in America. Anna Muganda has orchestrated this secret band of obfuscation and confusion. So the people go about piercing together every little information they can get - on their own. And in such giddy desperation for information, every source of "dataz" becomes an insider authority. The good, the bad and ugly.

Anna Muganda knew that her decisions would engender such invasive, probing, and often besmirching speculations. And she can, and should, do everything to protect her privacy from our inquiry. Just as you can not fault her for exercising her prerogative to protect herself, you can not blame us for exercising our civic responsibility, human responsibility, to protect what belongs to us. And it begins with searching for the truth as to what transpired at BOT so it won't happen again.

Somebody broke into the bank in broad daylight and stole national treasure, and we are out to get him or her!
 
Back
Top Bottom