Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
ngoja na huyo mama msikia amekufa kwa machungu ya mwanae!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sasa nipo upande wa CCM ,sababu hizi longolongo wanazotupakia VU (Vyama vya Upinzani) havina mwisho wenye kuleta matumaini kwa kila Mtanzania .Ukitazama CCM wametulia na wamejipanga wanaemuona mzigo wanamwambia arudi nyuma na kama alikuwa luteni anambiwa ajiuzulu abakie koplo.Mwiba
Sasa wewe umefanya nini hebu twambie?
Mimi sasa nipo upande wa CCM ,sababu hizi longolongo wanazotupakia VU (Vyama vya Upinzani) havina mwisho wenye kuleta matumaini kwa kila Mtanzania .Ukitazama CCM wametulia na wamejipanga wanaemuona mzigo wanamwambia arudi nyuma na kama alikuwa luteni anambiwa ajiuzulu abakie koplo.
Wapinzani wanaibua kila kitu wanachoona kiwaweza kuwasaidia mbele ya kuwavutia wananchi na pia kila wanachohisi kitawafanya wananchi waikatae CCM ,lakini wapinzani wakiwa wameshika kasi na kulipuwa wanayoyaita mabomu hawajaona kuwa hakuna matunda yeyote yanayopatikana hali ni ileile.
Nikionacho mbele ni kuwa haya mabomu mwisho yatawapasukia mikononi na yatawadhuru wenyewe. CCM wametoa uhuru wa kusema utakavyo wakijua kuwa faida inayopatikana itawasaidia wao kusonga mbele na kuwa na timu kabambe. Ili mabomu haya yawe na faida kwa wanaoyalipua ni lazima kama kufa kwanza waelekeze nguvu zao katika kudai katiba mpya na hakuna jingine litakalowasaidia.Tusidanganyane mchana kweupe.
ngoja na huyo mama msikia amekufa kwa machungu ya mwanae!!!
ngoja na huyo mama msikia amekufa kwa machungu ya mwanae!!!
ngoja na huyo mama msikia amekufa kwa machungu ya mwanae!!!
Mwanakiji Hivi hatuwezi kupata ripoti ya daktari kujua balali alikuwa anumwa na maradhi yapi?
BAsi naomba Mod aiunganishe huko..nilikuwa sijaiona na nimekuwa nikitafakari hii makala mpaka sasa sijapata jibuGembe,
Habari uliyotuma imejadiliwa mno kwenye thread ile nyingine ya Membe.
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13711
Aaah nao hao wanataka kutusumbua tu! sana sana wanaweza ishia kujinyonga!!!
Mwanakijiji kwa speculation bwana..
Mkuu ES,
Uzuri wa kuishi kwingi ni kuona mengi. Tuna mifano mingi tu ya watu walio fake vifo, hivyo
ni ngumu kuamini mpaka kuwe na ushahidi wa kutosha.
Mimi swali langu ni lile lile, kafia kwenye hospitali ipi? Tukishajua hospitali, mengine tutachunguza wenyewe.
Hawa waandishi wa habari wa Tz kwa kweli wamekosa kazi
*Watoa siku 30 wahusika kujisalimisha Luganga
*Waomba serikali iwaletee mchanga wa kaburi
Na Francis Godwin, Mufindi
WAKATI mwili wa aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Daud Ballali umezikwa Washington, Marekani Ijumaa iliyopita, baadhi ya wazee wa kabila la Wahehe wamekuja juu na kutoa siku 30 kwa yeyote aliyehusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho, kujisalimisha kijijini Luganga, Mufindi mkoani Iringa alikozaliwa gavana huyo.
Wazee hao kutoka kijiji cha Luganga na Mtwango, wameiomba serikali ifanye uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho na kufanya kila linalowezekana kuresha mwili huo nchini, ikishindikana ilete mchanga wa kaburi hilo ili wafanye mazishi ya kimila.
Wakizungumza na Majira jana kwa niaba ya wenzao, Mzee Samweli Kalinga (76) na Yohanes Kalinga (85), walisema wataamini kuwa mtoto wao amekufa baada ya kupata ufafanuzi wa kina kupitia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu kifo hicho.
Walisema wao kama wazee wa siku nyingi wa kijiji cha Luganga na Mtwango, wanashindwa kuamini kuwa mtoto wao amekufa, wataamini jambo hilo baada ya kuona maiti au picha yake akiwa amekufa.
Mzee Samweli alisema taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari hazitoshelezi kuamini kuwa ni kweli mtoto wao kipenzi, Dkt. Ballali amekufa hivyo ameiomba serikali kuunda tume haraka kuchunguza mazingira ya kifo cha gavana huyo wa zamani.
Alisema moja ya sababu inayowafanya waendelee kuamini kuwa Dkt. Ballali bado mzima ni mazingira ya sasa ya nyumbani kwao kijijini Luganga na nyumbani kwa baba zake wadogo eneo la Ziroziro, Mtwango.
" Nimeishi Mtwango tangu utoto wangu sijawahi hata siku moja kuona nyumba yenye msiba haina waombolezaji", alisema Mzee Samweli
Alisema kwa mujibu wa taratibu za kihehe, msiba unapotokea huombolezwa siku tatu mfululizo ama zaidi ambapo kwa muda huo, majirani hukusanyika nyumbani kwa wafiwa kuwafariji.
Alisema inawezekana ni kweli, Dkt. Ballali amekufa kama ilivyothibitishwa na baadhi ya ndugu zake lakini wao kama wazee wakihehe, wanasubiri serikali itoe taarifa rasmi ya kina ikiambatana na uchunguzi kamili wa kifo hicho.
"Tunaomba kuelezwa ugonjwa uliosababishia kifo cha mtoto wetu na jitihada zilizofanywa na serikali kuokoa maisha yake... Tunashindwa kuelewa serikali inapotoa pole wakati iliwahi kusema Ballali hajulikani alipo", alisema Mzee Samweli.
Kwa upande wake Mzee Yohanes alisema wanafanya mpango kukutana na ndugu wa marehemu kufanya tambiko la aina yake la kifo hicho na kuomba dua maalum kulaani kifo hicho kama kimetokana na 'mkono wa mtu'.
Mzee huyo, alisema wametoa siku 30 kwa watu waliohusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho kujisalimisha kijijini hapo, vinginevyo watu hao hawatadumu kwenye nyadhifa zao.
Alisema iwapo kifo hicho kimetokana na mapenzi ya Mungu basi wanamshukuru kwa kutimiza matakwa yake na kama ni kwa mipango ya shetani na wanadamu, basi itashughulikiwa ipasavyo.
Pamoja na mwili huo kuzikwa Marekani, wazee hao wameiomba serikali kufanya kila linalowezekana kuurejesha nchini, ikishindikana waletewe mchanga wa kaburi lake ili wafanye mazishi kwa mujibu wa mila za kihehe, Luganga alikozikwa baba yake mzazi Mzee Timoth Ballali aliyefariki dunia Aprili 3 mwaka 2000.
" Hata kama imeshindika kuleta mwili wake basi wasafirishe mchanga wa kaburi tuje tufanye mazishi kwenye makaburi ya Luganga alipolala baba yake mzazi. Kumzika Marekani ni sawa na kumtenga na familia yake", alisema Mzee Yohana.
http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6779