Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


MWK sio kwamba anasema Ballali hajafa...Nilivyoelewa mimi ni kwamba bado hajadhibitisha kama kweli kafa ama hajafa.
Alikuwepo kwenye mazishi kama wale wote waliokupa hizi data ambao nao walikuwepo kwenye mazishi.
Amekubali kuwa aliamini alipoambiwa pamoja na mambo ya msiba nk...Ila hawezi kusema kuwa kafa na vilevile hawezi kusema kuwa ni mzima na alihitimisha hivyo pale aliposema amekumbana na dead end.
So hapa tunaweza kuona ni wapi tofauti iko.
Pale unaposema 100% wakti na wewe uliambiwa na source unayoiamini kama ilivyo kwa MWK ndipo penye mushkel
 

Kwenye hiyo list ya majina kuna watoto wawili wa Ballali na Dada yake....kwenye watoto wake location zao ni za kweli well at least mpaka mara ya mwisho nilipokuwa na mawasiliano na mmoja wao..siku hizi wamebadilisha simu na email hawajibu.
 
Amesema anaamini 100%. Is there anything wrong to believe that Jesus is 100% the son of God? Acheni kutupotezea muda, tafutaneni au pigiaeni simu mmalizane acheni kutuzuga hapa.

Ahsante
 
Amesema anaamini 100%. Is there anything wrong to believe that Jesus is 100% the son of God? Acheni kutupotezea muda, tafutaneni au pigiaeni simu mmalizane acheni kutuzuga hapa.

Ahsante

Huwezi kufafanisha imani ya dini na huu mzozo wa kifo tata..Muulize MWK akwambie kwanini aligundua imani si neno dogo.
Kwa hiyo base on utata wa kifo plus yale ambayo hayakuonekana then unapata habari ambazo ni vigumu kuwa na imani nazo!
Kwa hiyo sasa Ballali ndio kawa Yesu?
Kuwa tuamini kafa ili kutukomboa?
 
MWKK mbona umechelewa kutoamini kuwa balali kafa!

tatizo la serikali ni inataka kuficha ukweli lakini imewaingiza watu wengi kwenye siri hii! imesahau kuwa hakuna siri ya watu wawili!

siri hii angefanya Anna Muganda peke yake kuwa balali amekufa, nna uhakika iisingekuwa vurumai la namna hii! tatizo ni kuwashirika mafisadi kadhaa kwenye siri hii, na ndo hapo unapopata information zisizoeleweka!

mara kafa boston, mara kafa sijui wapi, mara ni mtu huru na hatumhitaji, mara mama yake anapewa ulinzi kuliko wa rais mwenyewe, mara alikuwa mgonjwa, mara hawajui alilazwa hospitali gani! a total mess!

ushauri wa bure kwa mafisadi wengine: mkitaka kujulikana mmekufa wakati bado muhai, siri iwe ya mtu mmoja tu!
 
mara ya mwisho niliposoma gazeti mbowe alinukuliwa akisema kwamba chadema ina uhakika wa habari ya kifo cha ballali huku nccr mageuzi wakitilia shaka !

sasa mbowe mwenye family ties na ballali keshatoa maneno anayoamini na pia aliongelea kwa niaba ya chama chake chadema kusema kwamba ni kweli ballali kafariki !
 
Do you have enough information that make you believe that Jesus is the son of God or is the God? Death is not an option kama hajafa leo atakuwa baadaye. Sidhani kama ni good idea kupingana na familia yake kama serikali ilikuwa inamtafuta basi hapo tungehoji. Serikali ilitanganga hadharani kwamba haimtafuti. Just let the spirit of a good man rest in peace. Amen.
 
Mwafrika Wa Kike,

Ninaamini kuwa ni Balali mwenyewe, ndiye aliyewaambiwa viongozi wetu wakati anaondoka bongo kuwa anaenda Boston, na ninaamini kuwa aliwa-mislead kwa makusudi knowing kwamba haitachukua muda wataanza kumtafuta, hii ni imani yangu na ninaweza nikawa wrong!
 
kama nilivyouliza kwenye thread nyengine naomba majibu kwa watu wenye ufahamu mkubwa zaidi yangu juu ya haya
1) balali aliajiriwa BOT kama raia wa kawaida au kama expert aliyetolewa WB?
2) balali ana uraia wa nchi mbili ? ( marekani na tanzania) au ana Green Card au ana permanet visa ya Marekani pia?
3)balali alipopokonywa cheo cha gavana wa BOT, jee aliendelea bado kuwa muajiriwa wa serikali au ?
4) Balali alilazwa hosptali gani? na 'alifia' wapi?
 
majibu mengi pia yanaweza kutoka kwa mbowe aliyekubali uhakika wa kifo cha ballali ! je mmejaribu kumbana mbowe ??

kwa nini alikubali kwa uhakika kwamba ballali kafariki ?
alipata hizo habari lini ?
alitaarifiwa na nani ?
wana uhusiano gani ?

................
...........................
 


mzee mwenzangu, angalia source yako kuhusu niliyopigia mstari. Kama inakuthibitishia kwa asilimia 100 ni kweli, basi mimi na wewe itabidi tuamie kambi ya mwafrika wa kike. M. M.
 
Jamani, tuacheni ujinga hapa. Huyu jamaa kafa au hajafa? Sioni ugumu wala sababu yoyote uhai wa mtu uwe ni jambo lenye utata. Which is which, kafa au hajafa? I'm really getting tired of this.....
 
Jamani, tuacheni ujinga hapa. Huyu jamaa kafa au hajafa? Sioni ugumu wala sababu yoyote uhai wa mtu uwe ni jambo lenye utata. Which is which, kafa au hajafa? I'm really getting tired of this.....

kama ni kuangalia taarifa rasmi jibu ni jepesi... which is..
 
Nilivyoelewa dhana ya Mwafrika wa Kike ni kuwa ya Balali aachiwe Balali kwani ndio amini usiamini ameishakufa ,ila kwa madai yake ni kuwa alichokuwa nacho Balali ni kidogo tu ,ila yale majina aliyoyatokeza mwisho yamebeba siri nzito na huenda akaiweka hadharani katika toleo la pili akiambatanisha na vielelezo ,mara nyingi imesikika Balali akisema hakuwahi kunyofoa wala kutoa ruhusa ya uchotaji wa feza za WaTanzania ,kama Balali alikufa sawa ila kama aliuliwa basi waliomuua itakuwa wamekwenda mchomo wakidhani mambu yao ndio yameshajificha na Balali amezikwa na nyaraka zote na kutokuwa na hakutapatikana ushahidi.
Sasa Mwafrika waKike inaonyesha amepata kile ambacho mafisadi wakikiogopa kwa Balali.
Let us wait & see the next episode of Balali's mysterial death.
 
Hii naona inaonyesha sana jinsi vyombo vyetu vya habari havichambui kabisa mambo yasemwayo. Msomi kama Profesa Baregu kukaa na kusema maneno kama hayo bila hata ya kuyaangalia, inasikitisha sana kwa upande wake. Na hao wenye gazeti nao, wakaichukua hiyo habari kama ilivyo na kuibandika gazetini mwao bila ya hata kuangalia.
Hivi wakati analizungumzia suala hili, kuna mtu yeyote aliyemuuliza kuwa anajua nini anachoongea? Anaelewa jinsi gani vyombo vya kimataifa kama Interpol vinavyofanya kazi? Au almuradi leo Profesa Baregu kaongea, basi tuweke gazetini....Tunakebehisha fani za watu jamani....
 


Mtakumbuka nilikuwa naandika kwa msisitizo hili neno nalibold na kuliweka rangi nyekundu nakuliweka font kubwa zaidi ya yote (nitalirudia hilo neno baada ya maelezo yangu)

Niliuliza kwa kushangaa hapa iweje serikali na watanzania wote tukubali habari toka kwa ANNA MUGANDA kuwa Balali kawa ikiwa ANNA ni mmoja wapo wa watuhumiwa??? nilipoiluza kwa kusema kuwa ANNA MUGANDA kawanikuwa kulidanganya taifa na serikali yaku kunamtu hapa alinionya kwa kuniambia chonde chonde, nilipouliza chonde ni ya nini siku jibiwa

sasa natangaza rasmi kuwa napenda kuungana na MWafrika wa kike kwa kusisitiza tena kuwa BALALI HAJAFA
 
Hili kali sana, serikali imeshalikoroga na wanaendelea kulichanganya kwa statement zao zisizorandana kila siku.
 
yaani, tangu kifo cha balali sijawahi ku comment anything kuhusiana na hili, lakini imebidi ni comment katika hii twist, nimesoma post maelfu kuanzia uvumi hadi ilipokuja kuwa open kuwa balali is allegedly dead, sasa my mind is tired, au ndo lengo la 'watu' kutochosha akili tushindwe ku concentrate, if there is somebody out there with evidence plz help kutuliza akili yangu (ni ombi) but i believe the truth will eventualy come out, naendelea kuwa mvumilivu katika hili kama nilivyokuwa siku zote.
 

Jasusi,

Kama unaweza nisaidie kujibu swali langu, je Balali kafia kwenye hospitali gani? Kama alifia nyumbani ni hospitali gani ambayo ilithibitisha kifo chake.

Nafikiri ni swali rahisi na haliingii ndani kutaka kujua mgonjwa alikuwa anaumwa nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…