Mkuu Wangu Mwafrika Wa Kike,
Naomba nikupe heshima kubwa sana, na ninaheshimu sana the fact kwamba hapa JF tunakuwa na hoja tofauti on the ishu bila kutishana wala matusi, ninaomba kusema yafuatayo kulingana na uchunguzi wangu kuhusu kifo cha Balali, niliyoyagundua
1. Balali ninaamini 100% kuwa amefariki na kuzikwa majuzi kule Silver Spring, walioruhusiwa kuona maiti ni balozi Sefue, ndugu wa karibu, na maofisa wachache toka IMF, mwili wa marehemu haukuchomwa ila ulizikwa kama ulivyo. Hakuna laiyekuwa akiuliza kadi za kualikwa kuanzia kanisani mpaka kwenye mazishi, hivyo kupelekea watu wengi ambao hawakualikwa ku-gate crash, mke wake wa zamani alikuwepo so was watoto wake wawili wa mke wa kwanza, na pia mke wa sasa alikuwepo na mtoto wa mke ambaye sio wa Balali alikuwepo pia, Balali na mama wa sasa aliyemuacha hawakuwa na mtoto.
2. Hapa niweke marekebisho makubwa kwa kauli zetu nyingi sana, Balali hakuwahi kuwepo Boston hata wakati mmoja au wowote ule, Marehemu hakuwahi kufanya kazi World Bank kama wengi tulivyoaminishwa, aliwahi kufanya kazi IMF, akiwa na level ya juu sana iliyokuwa inampa nafasi ya kuwasiamia ma-Gavana wote wa Afrika kimashauriano, kwa hiyo alipochukua kazi ya u-Gavana wetu, wakuu huko IMF walishitushwa sana.
3. Niendelee zaidi na uchunguzi wangu ni kwamba Balali, ni kweli alikuwa na nyumba huko DC eneo la Bethesda, mahali panapoitwa Potomac, ambako pia balozi wetu anaishi, lakini aliporudi bongo aliipangissha ile nyumba , na kununua nyumba nyingine mahali panapoitwa Foggbottom, Washington DC eneo wanalosihi watu wakali kama Condy Rice na Bob Dole na wengineo, na ndipo alipofia yaani nyumbani kwake hapo, na hiyo nyumba ipo karibu na Watergate Hotel au apartments.
4. Balali aliondoka mara ya mwisho akielekea US kutokea Dodoma, alianza kupata maumivu makubwa ya tumbo, aliunganisha na kwenda US ambako alikuwa akitbiwa na baadye alipona na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake, ambako alikufa ghafla, siku ya Jumapili iliyopita.
5. Mara baada tu ya kuondoka kwa Balali, na habari zake kuanza kutoka kwenye media na kila mahali, kuna kundi la "Majambazi" lillilokwenda nyumbani kwa Mama wa Balali na kumpa kipigo kikali sana na kuipekua nyumba nje ndani, kule Boko na kuondoka na somethings, lakini haijulikani ni watu gani hawa kama ni majambazi kweli au "Majambazi", mke wa sasa wa Balali ilibidi arudi nyumbani kumuuguza mama mkwe, na ndio chanzo cha kuwekewa walinzi kwenye nyumba hiyo, kama ni wa serikali au wa binafsi hilo sikuweza kuthibitisha.
6. Ninaomba kusema hivi, kuwa serikali haijawahi kuwa ana habari yoyote ya uhakika na hii ishu, zaidi tu ya kuokoteza okoteza hasa hapa JF, hii ni kwa maoni yangu binafsi na mengi ninyoyajua.
Kwa hayo machache, ninaomba kusema kuwa ninaamini 100%, kuwa Balali amekufa, lakini pia ninaheshimu sana hoja ya Ndugu yangu Mwafrika Wa Kike kuwa anaamini kuwa hajafariki. Ningewaomba ndugu zangu wengine humu kuwa tujaribu kutafuta ukweli wa hii habari ili tuweze kuelimishana, hayo niliyoyasema nimeyafanyia kazi kubwa sana ikiwa ni pamoja kutembelea miji yote mitatu ya Boston, Dc, na Louisiana na bado ninaendelea lakini sio kwa kasikubwa tena kama mwanzoni,
Na pia ninaomba niwaombe radhi sana wanafamilia wa marehemu, kuwa sina nina ya kuendelea kuwaumiza na never ending stories on hiki kifo, lakini ni vyema tukweka record straight.
Ahsanteni Ndugu Zangu! JF mbele Zaidi!